Msajili wa Vyama vya Siasa amekiandikia barua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) (barua ya tarehe 07 Mei, 2026 yenye kumbukumbu namba HA. 322/362/16A/22) akikitaka kijieleze kwa nini kisisimamishwe usajili wake au kutozwa faini kwa kile alichokieleza kuwa ni 'ukiukaji wa sheria ya vyama vya siasa".
Hatua hii si ngeni kwa Msajili, kuviandama vyama vya upinzani makini vinavyotekeleza wajibu wake kwa umma kikamilifu. Mara zote, makosa anayoyatumia Msajili kuviandama vyama vya upinzani ni masuala ya kawaida ya kisiasa isipokuwa huonekana kuwa na shida pale tu Chama cha Mapinduzi au Serikali yake inapoguswa.
Wakati vyama vya upinzani vinaandamwa kwa vitisho na kutakiwa kujieleza Msajili hajawahi hata kwa bahati mbaya kukionya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho baadhi ya viongozi na wanachama wake wako kwenye rekodi ya kukiuka si tu sheria ya vyama anayojinasibu Msajili kuisimamia, bali sheria na maadili mengine ya nchi yetu.
Tumewasikia viongozi wa CCM kwa nyakati tofauti wakitamka hadharani kuwa watateka na kuwapoteza watu. Wakati kauli za namna hiyo zikitolewa na hatua zozote kutochukuliwa, Watanzania wameshuhudia wananchi kwa mamia wakitekwa, kupotea na kuuawa kama panya!
ACT Wazalendo tunasikitishwa na mwenendo huu wa Msajili unaolenga dhahiri kuvihujumu vyama vya upinzani na kukipendelea CCM. Wajibu wa Msajili si 'kushughulikia vyama vya upinzani. Wajibu wa Msajili ni kusajili vyama na kuviwezesha viweze kutekeleza wajibu wake wa kisiasa ili kukuza na kuimarisha demokrasia. Hata hivyo, Msajili amepindua wajibu huo, na sasa anatekeleza wajibu wa kuua vyama na kuangamiza demokrasia ya vyama vingi. Jambo hili halikubaliki na tunalipinga kwa nguvu zote.
Tunatoa wito kwa wanademokrasia na wananchi wote nchini kuunganisha nguvu pamoja kulinda demokrasia yetu dhidi ya mashambulizi haya. Mashambulizi dhidi ya mmoja wetu ni mashambulizi dhidi yetu sote. Gharama ya kutoweka kwa demokrasia katika nchi yetu ni kubwa, lazima tuilinde.
Pia soma: Msajili wa Vyama vya Siasa Ailima barua CHADEMA na kuipa Siku 13 Kujieleza Dhidi ya Tuhuma za Ukiukwaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa
Tunamtaka Msajili afute barua yake kwa CHADEMA na akiache chama hicho kitekeleze wajibu wake bila vikwazo. Msajili aache kuwa wakala wa CCM wa kupambana na vyama vya upinzani. Aache CCM ishindane kisiasa na vyama vya upinzani.
Nchi yetu inastahili haki, uadilifu na usawa. Mwenendo wa Msajili unakandamiza vyama, unaondoa haki na hatendi kwa usawa dhidi ya vyama. Ukosefu wa misingi ya haki ni hatari kwa utulivu, amani na mshikamano wa kitaifa. Tuwakumbusha CCM na Msajili, watanzania si wajinga. Tuna hakika, watanzania hawatakaa kimya kuona CCM na vyombo vyake vikihujumu demokrasia na kukandamiza haki katika nchi yao.
ACT Wazalendo, Taifa kwanza leo na kesho