ACT Wazalendo ndani ya GNU: Mamlaka ya Makamu wa Kwanza wa Rais na athari kwa siasa za Muungano

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
SUK 1.png

Zanzibar. Uamuzi wa ACT-Wazalendo kuingia katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) Zanzibar umefungua ukurasa mpya wa siasa za visiwani na kwa kiwango fulani umeibua maswali kuhusu namna hatua hiyo inavyoweza kuathiri siasa za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hususan Tanzania Bara.

Mjadala huo umeongezeka baada ya Mwenyekiti wa Taifa wa ACT-Wazalendo, Othman Masoud Othman, kurejea katika nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, hatua inayorejesha muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa uliowekwa kupitia marekebisho ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010.

Soma: Othman Masoud: Vyama vya Siasa vinaweza kuwa sababu ya kurejesha nyuma nchi na kuweka misingi ya vurugu

Hata hivyo, katika kutathmini nafasi hiyo, ni muhimu kutenganisha mamlaka ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na mamlaka ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2010, Makamu wa Kwanza wa Rais ni sehemu ya mfumo wa uongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Nafasi hiyo ilianzishwa katika mazingira ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa na ina uhusiano wa moja kwa moja na ushirikishwaji wa chama cha pili katika Serikali.

Katiba inampa Makamu wa Kwanza wa Rais nafasi ya kuwa mshauri mkuu wa Rais wa Zanzibar na kutekeleza majukumu mengine atakayopangiwa na Rais. Hivyo, anaweza kuwa na nafasi muhimu katika uendeshaji wa Serikali ya Zanzibar, lakini mamlaka yake hayawezi kuchukuliwa kuwa ni mamlaka juu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Kwa maana hiyo, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar hawezi, kwa nafasi hiyo pekee, kutoa maelekezo kwa wizara za Muungano, Serikali za mikoa ya Tanzania Bara au taasisi nyingine zilizo chini ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Hii ni tofauti na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, ambaye kwa mujibu wa Katiba ya Muungano ni msaidizi mkuu wa Rais katika mambo ya Muungano na ana majukumu yanayohusiana na ufuatiliaji wa shughuli za kila siku za Serikali katika eneo hilo.

Tofauti hii ni muhimu kwa sababu kuingia kwa ACT-Wazalendo katika GNU hakumaanishi kwamba chama hicho kimeingia katika Serikali ya Muungano. Ushiriki wake ni katika Serikali ya Zanzibar, kwa mamlaka yanayotokana na Katiba ya Zanzibar.

SUK 2.png

Hata hivyo, hatua hiyo ina umuhimu mkubwa kisiasa.

Mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar ulitokana na marekebisho ya Katiba ya mwaka 2010, yaliyolenga kuweka utaratibu wa ushirikishwaji wa chama cha siasa kilichoshika nafasi ya pili katika uchaguzi wa Rais wa Zanzibar, endapo kingetimiza masharti yaliyowekwa na Katiba.

Lengo mojawapo lilikuwa kupunguza mpasuko wa kisiasa uliokuwa umejitokeza Zanzibar kutokana na ushindani mkali wa uchaguzi na kuunda mazingira ya vyama vinavyoshindana wakati wa uchaguzi kushirikiana katika uendeshaji wa Serikali baada ya uchaguzi.

Kwa ACT-Wazalendo kuingia tena katika mfumo huo, siasa za Zanzibar zimepata mfano mpya wa chama cha upinzani kushiriki katika Serikali huku kikiendelea kuwa chama tofauti na CCM.

Hapo ndipo athari zake kwa siasa za Bara zinaweza kuonekana, si kwa upande wa mamlaka ya kikatiba, bali kwa upande wa mjadala wa kisiasa.

Hatua hiyo inaweza kuongeza mjadala kuhusu uwezekano wa kutumia mazungumzo, maridhiano na ushirikishwaji kama njia za kupunguza migogoro ya kisiasa Tanzania Bara. Hata hivyo, hilo halimaanishi kwamba mfumo wa Zanzibar unaweza kuhamishiwa moja kwa moja Bara, kwa sababu mazingira ya kikatiba, kisiasa na kimuundo yanatofautiana.

Pia, uzoefu wa GNU utakuwa na umuhimu katika kutathmini uhusiano kati ya chama tawala na chama cha upinzani ndani ya Serikali. ACT-Wazalendo sasa inakabiliwa na changamoto ya kushiriki katika uendeshaji wa Serikali huku ikiendelea kulinda utambulisho wake wa kisiasa na nafasi yake ya kukosoa pale inapohitajika.

Kwa upande mwingine, CCM na ACT-Wazalendo zimeingia katika ushirikiano ambao unaweza kuibua mijadala kuhusu mageuzi ya kisiasa, uchaguzi, Katiba, utawala wa sheria na namna ya kujenga mazingira ya ushindani wa kisiasa yenye amani.

Kwa hiyo, kipimo cha GNU hakitakuwa tu idadi ya nafasi ambazo ACT-Wazalendo itapata ndani ya Serikali. Swali kubwa litakuwa iwapo makubaliano ya kisiasa yatatafsirika kuwa hatua za utekelezaji katika maeneo yaliyokubaliwa.

Katika mazingira hayo, nafasi ya Othman Masoud inakuwa ya kipekee. Kwa upande mmoja, ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, mwenye wajibu wa kikatiba ndani ya Serikali ya Zanzibar. Kwa upande mwingine, ni Mwenyekiti wa Taifa wa ACT-Wazalendo, chama chenye shughuli na mtazamo unaovuka mipaka ya Zanzibar.

Mchanganyiko huo unaweza kuifanya nafasi yake kufuatiliwa kwa karibu katika siasa za kitaifa. Hata hivyo, mipaka kati ya nafasi hizo mbili inahitaji kutazamwa kwa kuzingatia Katiba na majukumu ya kila ofisi.

Kwa ujumla, kuingia kwa ACT-Wazalendo katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni zaidi ya mabadiliko ya nafasi za uongozi Zanzibar. Ni jaribio la kurejesha mfumo wa kisiasa uliowekwa kupitia marekebisho ya Katiba ya mwaka 2010 na wakati huo huo ni tukio linaloweza kuathiri mjadala mpana kuhusu maridhiano na ushirikishwaji katika siasa za Tanzania.

Athari zake kwa Serikali ya Muungano, hata hivyo, hazitoki moja kwa moja katika mamlaka ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. Zitatokana zaidi na namna uzoefu huo utakavyobadilisha mjadala wa kisiasa, uhusiano wa vyama na mitazamo kuhusu maridhiano katika Jamhuri ya Muungano.
 
View attachment 3676321

View attachment 3676322

kwani serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar imeanza jana na OMO kua makamu wa kwanza wa SMZ?

In fact,
katiba ya Zanzibar iko wazi kabisa kuhusu namna ambavyo serikali hiyo ya umoja wa kitaifa inavyoweza kuundwa, na kwakweli ACT wazalendo na OMO wajichelewesha mwenyewe tu kuingia kwenye serikali hiyo kikatiba, na nafasi zao zilikua wazi zikiwasubiri wajicheleweshe zaidi. Na itakua hivyo hata baada ya uchaguzi mkuu wa 2030 na chaguzi zote zijazo mpaka pala labda tena katiba hiyo ya Zanzibar itakapobadilishwa. Na kwa maana hiyo, hakuna athari zozote zile za kisiasa serikali hiyo ya umoja wa kitaifa Zanzibar inaweza kuzileta Tanzania au kwenye serikali madhubuti sana ya CCM katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na,
maridhiano ya hiyari miongoni mwa waTanzania wote, yapo na yangekuwepo tu, hata kama pasingekuwepo na serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar, kwasababu haidhuru au kuathiri chochote kulingana na matakwa ya wananchi.

Kumbuka,
maridhiano ya hiyari miongoni mwa waTanzania wote, yanalenga tu kujenga na kuweka msingi imara na muhimu sana kuelekea mchakato wa kupata katiba na si vinginevyo.🐒
 
Back
Top Bottom