ACT Wazalendo: Tunataka chunguzi kutekwa, kuteswa na kujeruhiwa kwa Edgar Mwakabela

ACT Wazalendo: Tunataka chunguzi kutekwa, kuteswa na kujeruhiwa kwa Edgar Mwakabela

Acha ujinga ndiyo maana kukawa na mahakama
Hujaona sasa hivi jamaa wamemtengenezea zengwe kwamba alikua na mahusiano na mke wa mtu. Alikanywa hakuskia akatukana mwenye mke.
Wanafanya relevance ya matusi aliyokuwa nayo na spinning ya kuungamanisha na ishu ya mahusiano.
Tayari kuna influencers uchwara wamelipwa kumchafua ili asipate haki yake.
Uchunguzi wa polisi utakuja na ishu za mapenzi.

Watch and Learn. Bongo ishakua ya hovyo sana.
 
Huku tukisubiri tar 20 tuwakere watu na uzi wa "Kwanini Mshahara wa January umechelewa?"
Hii ndo hoja ya maana, ikifika tarehe 19 unanitag tunaanza kuulizia yamebaki masaa mangapi tupate chetu tukamwagilie moyo.
 
Kuna Clip moja Mr Bean alimpiga jambazi risasi ya kifua jamaa likazimia na kuwahishwa hospital kwa ajili ya upasuaji wa kutoa risasi,

Wakati madaktari wamemzunguka mgonjwa theater kwa ajili ya operation mara jambazi anazinduka na kupata fahamu Ile kuangaza huku na huku kwenye jopo la madaktar waliomzunguka anamuona Mr Bean naye ni miongoni mwa madaktari watakaomfanyia operation mara jamaa akazimia na kupoteza fahamu kwa mara nyingine.
Unamaanisha inawezekana watakao mwekea ulinzi ni baadhi ya wahusika
 
ACT Wazalendo wamekemea vikali tukio la kutekwa, kuteswa na kuumizwa vibaya kwa kijana Edgar Mwakabela, ambaye mtandaoni anajulikana kama Sativa. Mwakabela alipatikana tarehe 27 Juni, 2024 huko Mkoani Katavi akiwa amejeruhiwa vibaya. Kijana huyu, mkazi wa Mbezi, Dar es Salaam, alitafutwa na ndugu zake bila mafanikio baada ya kutoonekana kwa siku tatu tangu Jumapili tarehe 23.

Chama cha ACT Wazalendo wamesema kuwa "Watanzania wameanza kuingiwa na hofu kutokana na kuongezeka kwa matukio ya wananchi kupotea, kuteswa, na kuuawa kwa kasi hivi karibuni. Inasikitisha kuona Jeshi la Polisi kutochukua hatua za haraka dhidi ya wahusika wa matukio hayo. Tunalaani kwa nguvu zote kuongezeka kwa matukio haya bila hatua madhubuti kuchukuliwa."

Aidha wameongeza kwa kusema "Wananchi wamechoshwa na kutowajibika kwa Jeshi la Polisi au kuhusishwa kwao katika matukio ya kuwaumiza, kuwatesa, na kuwakandamiza badala ya kutekeleza wajibu wa kuwalinda pamoja na mali zao. ACT Wazalendo tumechukua hatua za kumrejesha Dar es Salaam kwa ndege kijana Mwakabela ili aweze kupatiwa matibabu haraka na ya kibingwa. Hata hivyo, tunataka uchunguzi wa haraka ufanyike ili kubaini watu waliohusika na utekaji wa Ndg. Edgar Mwakabela"
 
Alafu anawaonyesha na Sura kabisa anajiamini nini kwamba analindwa na ulinzi mkali au 😂
SATIVA ni mmea ambao unampa hali ya kujiamini mtuamiaji wake, unakuondolea uoga wa kuogopa watu ovyo ovyo.

Maana yake ni BANGI.
 
SATIVA ni mmea ambao unampa hali ya kujiamini mtuamiaji wake, unakuondolea uoga wa kuogopa watu ovyo ovyo.

Maana yake ni BANGI.
Jamaa anatukana matusi noma sana kweli Bange haina faida kabisa ona sasa kilichomkuta kumbe mibange, sasa atabakia anaimba tu Bange Bange Bange zimesababisha nitupwe msituni Katavi X 7
 
ACT Wazalendo wamekemea vikali tukio la kutekwa, kuteswa na kuumizwa vibaya kwa kijana Edgar Mwakabela, ambaye mtandaoni anajulikana kama Sativa. Mwakabela alipatikana tarehe 27 Juni, 2024 huko Mkoani Katavi akiwa amejeruhiwa vibaya. Kijana huyu, mkazi wa Mbezi, Dar es Salaam, alitafutwa na ndugu zake bila mafanikio baada ya kutoonekana kwa siku tatu tangu Jumapili tarehe 23.

Chama cha ACT Wazalendo wamesema kuwa "Watanzania wameanza kuingiwa na hofu kutokana na kuongezeka kwa matukio ya wananchi kupotea, kuteswa, na kuuawa kwa kasi hivi karibuni. Inasikitisha kuona Jeshi la Polisi kutochukua hatua za haraka dhidi ya wahusika wa matukio hayo. Tunalaani kwa nguvu zote kuongezeka kwa matukio haya bila hatua madhubuti kuchukuliwa."

Aidha wameongeza kwa kusema "Wananchi wamechoshwa na kutowajibika kwa Jeshi la Polisi au kuhusishwa kwao katika matukio ya kuwaumiza, kuwatesa, na kuwakandamiza badala ya kutekeleza wajibu wa kuwalinda pamoja na mali zao. ACT Wazalendo tumechukua hatua za kumrejesha Dar es Salaam kwa ndege kijana Mwakabela ili aweze kupatiwa matibabu haraka na ya kibingwa. Hata hivyo, tunataka uchunguzi wa haraka ufanyike ili kubaini watu waliohusika na utekaji wa Ndg. Edgar Mwakabela"
Na Ile mitusi yake sasa itakuaje? Unakula mabange yako huko sababu una kismatifoni chako cha laki basi unaanza tu Bange zimekolea unaanza kuporomosha mitusi unawatukana watu, unajua kuna wengine hawajui kuvumilia matusi sasa inategemea unaemtukana sio unatukana tukana tu mitusi tena unajimwambafai poromosha mitusi ya nguoni lakini wengine mboni wanavuta Bange na hawapo km huyu au ni beginner wannabe? Bange hizi ni za Wapi?
20240627_190439.jpg
 
Na Ile mitusi yake sasa itakuaje? Unakula mabange yako huko sababu una kismatifoni chako cha laki basi unaanza tu Bange zimekolea unaanza kuporomosha mitusi unawatukana watu, unajua kuna wengine hawajui kuvumilia matusi sasa inategemea unaemtukana sio unatukana tukana tu mitusi tena unajimwambafai poromosha mitusi ya nguoni lakini wengine mboni wanavuta Bange na hawapo km huyu au ni beginner wannabe? Bange hizi ni za Wapi?View attachment 3028313
Hahaha dah! Kwani sativa ni nini?
 
View attachment 3027737
Tunataka chunguzi kutekwa, kuteswa na kujeruhiwa kwa Edgar Mwakabela

ACT Wazalendo tunalaani na kukemea vikali tukio la kutekwa, kuteswa na kuumizwa vibaya kwa kijana Edgar Mwakabela, mtandaoni (X) anajulikana Sativa. Mwakabela amepatikana leo tarehe 27 Juni, 2024 huko Mkoani Katavi akiwa amejeruhiwa vibaya.

Kijana huyu ni mkazi wa Mbezi, Dar es Salaam alitafutwa na ndugu zake bila mafanikio baada ya kutoonekana kwa siku 3 tangu Jumapili tarehe 23.

Watanzania wameanza kuingia tena na hofu kukithiri kwa matukio ya wananchi kupotea, kuteswa na kuawa kwa kasi siku za hivi karibu. Inasikitisha pia kuona Jeshi la Polisi kutochukua hatua za haraka kwa wanaohusika na matukio hayo.

Tunalaani kwa nguvu zote kuongezeka kwa matukio hayo bila hatua madhubuti kuchukuliwa. Wananchi wamechoshwa na kutowajibika kwa Jeshi la Polisi au kuhusishwa kwao katika matukio ya kuwaumiza, kuwatesa na kuwakandamiza kila uchao badala ya kutekeleza wajibu wa kuwalinda pamoja na mali zao.

ACT Wazando tumechukua hatua za kumrejesha Dar es Salaam kwa Ndege kijana Mwakabela ili aweze kupatiwa matibabu haraka na ya kibingwa.

Hata hivyo, tunataka hatua za haraka za uchuhguzi zifanyike ili kubaini watu waliohusika na utekaji wa Ndg. Edgar Mwakabela.

Ndg. Dahlia Majid,
Waziri kivuli wa Mambo ya Ndani
27 Juni, 2024.
YAANI CCM WAJICHUNGUZE? TANGU LINI?
 
Back
Top Bottom