ACT Wazalendo: Tunataka chunguzi kutekwa, kuteswa na kujeruhiwa kwa Edgar Mwakabela

Acha ujinga ndiyo maana kukawa na mahakama
Hujaona sasa hivi jamaa wamemtengenezea zengwe kwamba alikua na mahusiano na mke wa mtu. Alikanywa hakuskia akatukana mwenye mke.
Wanafanya relevance ya matusi aliyokuwa nayo na spinning ya kuungamanisha na ishu ya mahusiano.
Tayari kuna influencers uchwara wamelipwa kumchafua ili asipate haki yake.
Uchunguzi wa polisi utakuja na ishu za mapenzi.

Watch and Learn. Bongo ishakua ya hovyo sana.
 
Huku tukisubiri tar 20 tuwakere watu na uzi wa "Kwanini Mshahara wa January umechelewa?"
Hii ndo hoja ya maana, ikifika tarehe 19 unanitag tunaanza kuulizia yamebaki masaa mangapi tupate chetu tukamwagilie moyo.
 
Unamaanisha inawezekana watakao mwekea ulinzi ni baadhi ya wahusika
 
ACT Wazalendo wamekemea vikali tukio la kutekwa, kuteswa na kuumizwa vibaya kwa kijana Edgar Mwakabela, ambaye mtandaoni anajulikana kama Sativa. Mwakabela alipatikana tarehe 27 Juni, 2024 huko Mkoani Katavi akiwa amejeruhiwa vibaya. Kijana huyu, mkazi wa Mbezi, Dar es Salaam, alitafutwa na ndugu zake bila mafanikio baada ya kutoonekana kwa siku tatu tangu Jumapili tarehe 23.

Chama cha ACT Wazalendo wamesema kuwa "Watanzania wameanza kuingiwa na hofu kutokana na kuongezeka kwa matukio ya wananchi kupotea, kuteswa, na kuuawa kwa kasi hivi karibuni. Inasikitisha kuona Jeshi la Polisi kutochukua hatua za haraka dhidi ya wahusika wa matukio hayo. Tunalaani kwa nguvu zote kuongezeka kwa matukio haya bila hatua madhubuti kuchukuliwa."

Aidha wameongeza kwa kusema "Wananchi wamechoshwa na kutowajibika kwa Jeshi la Polisi au kuhusishwa kwao katika matukio ya kuwaumiza, kuwatesa, na kuwakandamiza badala ya kutekeleza wajibu wa kuwalinda pamoja na mali zao. ACT Wazalendo tumechukua hatua za kumrejesha Dar es Salaam kwa ndege kijana Mwakabela ili aweze kupatiwa matibabu haraka na ya kibingwa. Hata hivyo, tunataka uchunguzi wa haraka ufanyike ili kubaini watu waliohusika na utekaji wa Ndg. Edgar Mwakabela"
 
Alafu anawaonyesha na Sura kabisa anajiamini nini kwamba analindwa na ulinzi mkali au 😂
SATIVA ni mmea ambao unampa hali ya kujiamini mtuamiaji wake, unakuondolea uoga wa kuogopa watu ovyo ovyo.

Maana yake ni BANGI.
 
Wanasiasa wanachukua point 3 hapa
 
SATIVA ni mmea ambao unampa hali ya kujiamini mtuamiaji wake, unakuondolea uoga wa kuogopa watu ovyo ovyo.

Maana yake ni BANGI.
Jamaa anatukana matusi noma sana kweli Bange haina faida kabisa ona sasa kilichomkuta kumbe mibange, sasa atabakia anaimba tu Bange Bange Bange zimesababisha nitupwe msituni Katavi X 7
 
Na Ile mitusi yake sasa itakuaje? Unakula mabange yako huko sababu una kismatifoni chako cha laki basi unaanza tu Bange zimekolea unaanza kuporomosha mitusi unawatukana watu, unajua kuna wengine hawajui kuvumilia matusi sasa inategemea unaemtukana sio unatukana tukana tu mitusi tena unajimwambafai poromosha mitusi ya nguoni lakini wengine mboni wanavuta Bange na hawapo km huyu au ni beginner wannabe? Bange hizi ni za Wapi?
 
Hahaha dah! Kwani sativa ni nini?
 
YAANI CCM WAJICHUNGUZE? TANGU LINI?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…