ACT Wazalendo waibwaga CCM Konde, Mohamed Said Issa ashindi kiti cha Ubunge

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Konde, Abdallah Said Hamad amemtangaza Mgombea wa ACT-Wazalendo, Mohamed Said Issa kuwa mshindi wa Ubunge kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo uliofanyika leo 09 Oktoba, 2021



Mohamed Said Issa amepata kura 2,391 dhidi ya 794 za mgombea wa CCM, Mbarouk Amour Habib. Mgombea wa AAFP, Hamad Khamis Mbarouk amepata kura 55 na Salama Khamis wa CUF amepata kura 98

 
Mohamed Said Issa (ACT Wazalendo), ametangazwa mshindi katika uchaguzi mdogo wa Jimbo Konde kwa kupata kura 3408.

Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo Abdallah Said Ahmed amemtangaza leo Jumamosi Oktoba 9, 2021 katika kituo cha majumuisho cha Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Katika matokeo hayo, Issa amefuatiwa na mgombea wa CCM, Mbarouk Amour Habib aliyepata kura 794 kati ya kura 3,338 zilizopigwa.

Mgombea mwingine katika uchaguzi huo Salama Khamis Omar wa CUF alipata kura 98 na Hamad Khamis Mbarouk (AAFP) akipata kura 55.
 
Kwa hiyo ule wa kwanza ulikuwa ni uporaji au? Kura zote hizo? Yule aliyejiuzulu alishindaje?
 
Ingekuwa enzi ya lile zee, mkurugenzi wa uchaguzi hana kazi...
 
Mshindi amepata kura elfu mbili na kitu, na CCM kapata kura mia saba na kitu, hilo jimbo au mtaa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…