ACT Wazalendo wakosoa Machinga kuondolewa mjini

ACT Wazalendo wakosoa Machinga kuondolewa mjini

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1686647098507.png

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimesema hakikubaliani na uamuzi wa kuwaondoa wafanyabiashara wadogo (machinga) katikati ya mji badala yake serikali inatakiwa kutenga maeneo ambayo yana watu wengi kwa ajili ya kundi hilo kufanya biashara.

Katika mkutano uliofanyika jijini Mwanza jana, Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe, amesema kuwaondoa katikati ya miji machinga kumesababisha baadhi yao mitaji kuisha na wengine kukwama kulipa mikopo, hivyo kuzalisha umaskini kwa kundi hilo.

“Kwa hiyo, pendekezo letu ACT-Wazalendo ni kwamba miji inaweza kutumika na wote kwa maslahi ya wote na ni lazima machinga wa Mwanza watengewe eneo katikati ya mji,” amesema.

Zitto pia amesema chama hicho kimepokea malalamiko ya kuwapo ‘utitiri’ wa tozo katika uvuvi, jambo ambalo linachangia kuwarudisha wavuvi katika umaskini.

“Mkulima akiwa na trekta, hana leseni hatozwi. Mvuvi akiwa na boti au mtumbwi, wanamtoza leseni wakati ndio chombo chake cha uzalishaji. Haya yote tunapendekeza yaondolewe ili mvuvi afanye shughuli zake na kuondoka katika umaskini,” amesema.
 
Wamachinga wangetafutiwa mazingira yao wavunje hata uwanja wa fisi😀
 
Back
Top Bottom