Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
CHAMA cha ACT Wazalendo kimesema kitaendelea kushawishi sera mbadala za kuondoa watu kwenye umasikini ikiwemo ya Hifadhi ya Jamii kwa wote itakayohakikisha kunakuwa na Bima ya Afya kwa wote.
Chama hicho kimesema haikubaliki kuwa asilimia 61 ya watu masikini nchini Tanzania wapo mikoa ya Magharibi na Kanda ya ziwa na kwamba asilimia 33 ya watu wote masikini hapa nchini wapo mikoa ya Geita, Kagera, Simiyu na Mwanza.
Akizungumza kwenye mkutano uliofanyika mjini Kahama Kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe amesema chama hicho kinahitaji uchumi wa waTanzania ukue kwa kasi ya wastani wa 8% kwa mwaka, kwa miaka miaka 10 mfululizo ya mwanzo na kasi isipungue asilimia 6 kwa miaka mingine 10 hadi kufikia 2050.
Ameeleza kuwa kwa miaka10 ya mwanzo, kilimo kinapaswa kuwa sekta kuu ya kuchochea ukuaji isiwe chini ya asilimi 6 hadi 8 kwa hiyo miaka 10 mfululizo kwa kufanya hivi tutafuta umasikini nchini.
Zitto amesema Tume ya Mipango inatakiwa irudi ili kuongoza mwelekeo huo mpya wa kisera na kwamba sio sawa kuwa Miaka 60 baada ya Uhuru karibu nusu ya watu wanaishi chini ya mstari wa umasikini.