GE2025 ACT Wazalendo wamteua Luhaga Mpina kama mgombea Urais wa chama hicho

GE2025 ACT Wazalendo wamteua Luhaga Mpina kama mgombea Urais wa chama hicho

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Wakuu,

ACT Wazalendo wana jambo lao leo. Kaa karibu na uzi huu kupata updates mbili tatu


View: https://youtube.com/live/eLJsZyyV4DU?feature=share



Hali ilivyo kwenye Ukumbi wa Mkutano Mkuu wa ACT Wazalendo unaofanyika leo Agosti 6, 2025, Mliman City Jijini Dar es Salaam, katika Mkutano huo inatarajiwa Chama hicho kitapata jina la mgombea Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama hicho, leo Agosti 6, 2025, amesema kuna wimbi kubwa la Watu wanaotaka kujiunga nao wakitokea CCM na Vyama vingine vya upinzani na kwamba wao wanawakaribisha.

Chama cha ACT Wazalendo kimesema imeshaa kamilisha utaratibu wa kuwapata wagombea wa ubunge na udiwani kwa upande wa tanazania bara na visiwani, Ado Shaibu akizungumza katika mkutano maalum wa kumpata mgombea urais kupiia chama hicho Agosti 6, 2025 jijini Dar es salaam
1754475252306.png
​

Mwenyeki wa chama cha ACT Wazalendo Othuman Masoud amefungua rasmi mkutano mkuu Maalum wa kusimamishwa mgombea Urais leo Agosti 6, 2025 jijini Dar es Salaam.

NAIBU Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza alipopewa nafasi ya kuzungumza kwenye Mkutano Maalum wa chama hicho leo, Agosti 6, 2025 alianza kwa kuwasalimia ''Nawasalimu kwa jina la Jumhuri ya Muungano wa Tanzania." mwitikio wake haukuwa vile alivyotarajia.

WhatsApp Image 2025-08-06 at 13.52.00_6e01ac04.jpg

WhatsApp Image 2025-08-06 at 13.51.59_3d015464.jpg

Mpina akiwa ndani ya ukumbi wa Mlimani City katika mktano maalum wa ACT Wazalendo wakumpata mgombea urais.



Mwenyekiti mstaafu wa chama ACT Wazalendo zittoZuberi Kabwe ameseama kuwa miezi mitatu ijayo wanatarajia kubali mfumo mzima siasa katika taifa hili.

​
 

Attachments

Natamani HK nae aje ACT tuone kama nani atapewa urais
 
Back
Top Bottom