ACT Wazalendo wataka kamati ya maadili ya bunge kuwashughulikia wabunge waliowakashifu na kukejeli wanaharakati wa Kenya

ACT Wazalendo wataka kamati ya maadili ya bunge kuwashughulikia wabunge waliowakashifu na kukejeli wanaharakati wa Kenya

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Chama cha ACT Wazalendo kimeitaka Ofisi ya Spika wa Bunge la Tanzania kuwajibika kwa kuwaita na kuwahoji wabunge katika Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, kufuatia kauli zilizotolewa na baadhi yao kutozingatia maadili ya uongozi, utu wala heshima ya chombo hicho muhimu cha kutunga sheria.

Kwa mujibu wa chama hicho, baadhi ya wabunge walitumia lugha ya kashfa na kejeli, huku wengine wakipongeza hatua zilizochukuliwa na vyombo vya ulinzi dhidi ya wanaharakati wa Kenya,

Kauli hiyo imekuja baada ya Mei 28,2025 Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kuwakanya wabunge wanapochangia bungeni wasivunje kanuni, Katiba na Sheria licha ya kuwepo kwa uhuru wa kujieleza.

Akizungumza leo Mei 29, 2025, Mwenyekiti Ngome ya Wanawake wa chama hicho, Janeth Rithe amesema kitendo kilichofanyika ni ukiukwaji wa mikataba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

"Tunaitaka Kamati ya Maadili ya Bunge, kupitia Ofisi ya Spika, iwafikishe mbele ya kamati wabunge wote waliotoa kauli za chuki, dharau na dhihaka dhidi ya wanaharakati waliokumbwa na mateso wakiwa nchini Tanzania. Kauli zao si tu zinadhalilisha waathirika, bali pia zinaichafua taswira ya Bunge letu kwa wananchi na kwa jumuiya ya kimataifa,"amedai Rithe.

"Tunasisitiza kwamba, heshima ya Bunge haitatokana na majengo au vyeo, bali na tabia na kauli za wale wanaolihudumia. Tunatarajia kuona Bunge likichukua hatua za wazi, siyo kufumbia macho madhambi ya baadhi ya wabunge wake.”

Source: Mwananchi
 
ACT kuna muda dishi linakaa sawa muda mwingine linayumba
 
Sio ajabu hao Wabunge Mama akawateua kuwa Mawaziri😭😭😭
 
Back
Top Bottom