Pre GE2025 ACT Wazalendo: Wizara ya Elimu iwache kuwatumia wanafunzi katika shughuli za CCM

Pre GE2025 ACT Wazalendo: Wizara ya Elimu iwache kuwatumia wanafunzi katika shughuli za CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
WhatsApp Image 2025-01-24 at 11.01.55_7c3b5282.jpg

WhatsApp Image 2025-01-24 at 11.01.55_c0061e92.jpg

TAARIFA KWA UMMA

Wizara ya Elimu iwache kuwatumia wanafunzi katika shughuli za CCM

ACT Wazalendo tunalaani vitendo vinavyoanza kushamiri kwa kasi vya kuwashirikisha wanafunzi katika shughuli za siasa wakati wa muda wa masomo, jambo ambalo ni kinyume na miongozo ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Zanzibar.

ACT Wazalendo tunazo taarifa za walimu kulazimishwa kuwatoa wanafunzi madarasani ili kushiriki katika shughuli za siasa ikiwa ni pamoja na mapokezi, mikutano na makongamano ya Chama cha Mapinduzi. Kufanya hivi ni kuwakosesha wanafunzi haki yao ya elimu, jambo ambalo linaweza kuathiri ufaulu wa wanafunzi hao na ufanisi wa walimu katika majukumu yao ya kila siku.

Juzi tarehe 22/01/2024, tumeshuhudia Wizara ya Elimu ikitumikia maslahi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwapanga wanafunzi katika barabara inayotoka Uwanja wa Ndege (Airport) kuelekea Mjini ili kumpokea Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar. ACT Wazalendo, tunaona kufanya hivi ni kuishiwa kisiasa kwa CCM kwa kukosa watu wa kuwaunga mkono na kuanza kuwalazimisha wanafunzi ambao walitakiwa kuwa madarasani kuendelea na masomo na kushiriki katika shughuli zao.

Kutokana na tukio hili la kuwatoa walimu na wanafunzi kushiriki katika shughuli za siasa kitendo kinachochangiwa na uongozi wa Wizara ya Elimu kutofahamu mipaka yao, tunaitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kutekeleza yafuatayo:-

1. Tunawataka viongozi wa Wizara ya Elimu kuacha mara moja tabia ya kuwalazimisha wanafunzi kushiriki katika shughuli za kisiasa, wanapokuwa skuli, hasa katika muda wa mosomo.

2. Tunamtaka Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, ikiwa ana hamu ya kushiriki siasa aache utumishi wa umma ili ashiriki shughuli za Siasa. Kitendo cha yeye kuonekana akiwa amevaa sare za CCM ni kinyume na taratibu za Utumishi wa Umma kwa mujibu wa Sheria Nambari 2 ya 2011 na Sheria Nambari 3 ya 2003.

3. Tunawataka walimu wa skuli za serikali na wamiliki wa skuli za binafsi kutoruhusu wanafunzi wa skuli wanazozisimamia kutumiwa na vyama vya siasa na wanasiasa, huku wakiwakosesha wanafunzi hao haki yao ya msingi ya kupata elimu.

4. Tunaitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kutoa mwongozo, mahsusi kwa wanafunzi kushiriki katika shughuli za kisiasa ikiwa wanahisi miongozo iliyopo imepitwa na wakati na kwamba sasa ipo haja ya vyama vya siasa kuwatumia wananfunzi hao katika shughuli zao za siasa.

Chama cha ACT – Wazalendo, hakitasita na kuendelea kuwa sauti ya Wazanzibari kwa kuisimamia Serekali juu ya masuala yote yanayofanywa kinyume na kanuni, taratibu na sheria za nchi kwa maslahi ya wanachi wa Zanzibar.

Imetolewa leo, tarehe 24/01/2025 na,
Dkt. Mohammed Ali Suleiman
 
Jamani msiwe na wivu. Wanafunzi watadoma tu. Unaaagizwa ujaze watu mkutanoni, watu mkutano uliopita uliwaambia saa 4 kiongozi kaja saa 9, mkutano unaofuata responce inakuwa ndogo sana. Ndipo kwa nia njema kabisa wanafunzi husaidia kuongeza idadi ya washiriki wa mkutano. Changamoto kubwa ipo mijini na vijiji vyenye upinzani.
 
Wale wa International School of Tanganyila huwa na wao wanaenda kwenye mikutano ya CCM? au ni wa kajamba nani tu?
 
Back
Top Bottom