PostGE2025 ACT Wazalendo yalaani Mauaji ya Raia yaliyofanywa na Polisi Oktoba 29

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
KAULI YA ACT WAZALENDO KUFUATIA MAUAJI YA TAREHE 29/10/2025 NA SIKU ZILIZOFUATA BAADA YA UCHAGUZI

Chama cha ACT Wazalendo, kupitia kikao cha Kamati ya Uongozi Taifa, kilanaani vikali ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliofanywa dhidi ya wananchi kuanzia tarehe 29 Oktoba 2025, katika maeneo mbalimbali nchini.

Taarifa mbalimbali zimeonyesha wananchi waliouawa kwa risasi, waliojeruhiwa na wengine kupotea hadi leo wanatafutwa na familia zao.

Aidha, tunalaani kwa nguvu zote vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vilivyofanywa dhidi ya wanachama na wagombea wetu katika mchakato wa Uchaguzi. Kama vile kuuawa kwa Mgombea wetu wa udiwani wa kata ya Sirari Jimbo la Tarime (Mkoa wa Mara) Ndg. Dafroza Jacob, ambaye ameuwawa katika mikono ya Polisi baada ya kukamatwa na kupewa mateso hadi kupelekwa kifo chake tarehe 5 Novemba, 2025.

ACT Wazalendo, tunatoa pole za dhati kwa familia za waliopoteza wapendwa wao, na tunawaomba majeruhi wote wapone haraka. Taifa letu limepoteza ndugu, watoto na wazazi ambao walikuwa na ndoto za kulitumikia taifa kwa namna zao. Maumivu haya ni yetu sote.

ACT Wazalendo inaunga mkono wadau na taasisi zote za ndani na nje ya nchi zilizotoa tamko la kulaani matukio haya na kutoa mapendekezo mbalimbali. Katika hili ACT Wazalendo inatoa msimamo ufuatao;-

  1. Tunataka uchunguzi huru wa kimataifa kuhusu matukio ya tarehe 29/10/2025 na siku zilizofuata.
  2. Tunataka wote waliohusika — waliotoa amri, waliotekeleza, au waliokaa kimya kuficha ukweli wawajibishwe kwa mujibu wa sheria.
  3. Tunaitaka Serikali ikomeshe mara moja matumizi ya nguvu dhidi ya raia na ianze safari ya majadiliano ya kitaifa kwa kusikiliza kila sauti ya wananchi.
  4. Madai yote ya mageuzi ya kikatiba, kisheria, kiutawala, kimfumo na kitaasisi ambayo yamekuwa yakitolewa na kupaziwa sauti tokea kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi yafanyiwe kazi haraka ikiwa ni sehemu na hatua za msingi zinazohitajika kurejesha taifa letu pamoja.
Kwa niaba ya Kamati ya Uongozi ya Chama Taifa,

(sahihi ya saini)
DOROTHY MANKA JONAS SEMU
KIONGOZI WA CHAMA

6/11/2025
1762423125643.png
 
Inaumiza sana lakini Act pia nyie ni wakulaumiwa mliombwa na wenzenu msishiriki uchaguzi huu mkashupaza shingo eti hamuwezi kumuachia fisi zizi wazi, kikowapi sasa? Oooh wananchi jitokezeni kwa wingi mkapige kura, hizo kura zenyewe ziko wapi? Nadhani mmjieona wenyewe.
 
kutoshiriki kwao kungezuia mauaji yalliyotokea?
 
Tayari CHADEMA wametangaza siku saba za maombolezo kwa mauaji ya kutisha yaliyofanywa na Serikali ya CCM dhidi ya wananchi

James Mbatia Mwenyekiti halali wa NCCR MAgeuzi ameshatoa salamu zapole

Profesa Lipumba mwenyekiti wa CUF ameshatoa salamu za kulaani mauaji hayo nchini.

Ila ACT Wazalendo ambayo Mwenyekiti wa chama hicho ni Othman Masoud mpaka sasa hakijatoa salamu yoyte ya kulaani mauaji ya kutisha ya wananchi simply kwa sababu ya kudai uchaguzi huru na haki. Hii ituonyeshe hii ACT ni chama cha namna gani.
 
KAULI YA ACT WAZALENDO KUFUATIA MAUAJI YA TAREHE 29/10/2025 NA SIKU ZILIZOFUATA BAADA YA UCHAGUZI

Chama cha ACT Wazalendo, kupitia kikao cha Kamati ya Uongozi Taifa, kilanaani vikali ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliofanywa dhidi ya wananchi kuanzia tarehe 29 Oktoba 2025, katika maeneo mbalimbali nchini.

Taarifa mbalimbali zimeonyesha wananchi waliouawa kwa risasi, waliojeruhiwa na wengine kupotea hadi leo wanatafutwa na familia zao.

Aidha, tunalaani kwa nguvu zote vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vilivyofanywa dhidi ya wanachama na wagombea wetu katika mchakato wa Uchaguzi. Kama vile kuuawa kwa Mgombea wetu wa udiwani wa kata ya Sirari Jimbo la Tarime (Mkoa wa Mara) Ndg. Dafroza Jacob, ambaye ameuwawa katika mikono ya Polisi baada ya kukamatwa na kupewa mateso hadi kupelekwa kifo chake tarehe 5 Novemba, 2025.

ACT Wazalendo, tunatoa pole za dhati kwa familia za waliopoteza wapendwa wao, na tunawaomba majeruhi wote wapone haraka. Taifa letu limepoteza ndugu, watoto na wazazi ambao walikuwa na ndoto za kulitumikia taifa kwa namna zao. Maumivu haya ni yetu sote.

ACT Wazalendo inaunga mkono wadau na taasisi zote za ndani na nje ya nchi zilizotoa tamko la kulaani matukio haya na kutoa mapendekezo mbalimbali. Katika hili ACT Wazalendo inatoa msimamo ufuatao;-

  1. Tunataka uchunguzi huru wa kimataifa kuhusu matukio ya tarehe 29/10/2025 na siku zilizofuata.
  2. Tunataka wote waliohusika — waliotoa amri, waliotekeleza, au waliokaa kimya kuficha ukweli wawajibishwe kwa mujibu wa sheria.
  3. Tunaitaka Serikali ikomeshe mara moja matumizi ya nguvu dhidi ya raia na ianze safari ya majadiliano ya kitaifa kwa kusikiliza kila sauti ya wananchi.
  4. Madai yote ya mageuzi ya kikatiba, kisheria, kiutawala, kimfumo na kitaasisi ambayo yamekuwa yakitolewa na kupaziwa sauti tokea kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi yafanyiwe kazi haraka ikiwa ni sehemu na hatua za msingi zinazohitajika kurejesha taifa letu pamoja.
Kwa niaba ya Kamati ya Uongozi ya Chama Taifa,

(sahihi ya saini)
DOROTHY MANKA JONAS SEMU
KIONGOZI WA CHAMA

6/11/2025
Zitto Kabwe alikuwa hataki taarifa hiyo itolewe
 
Inaumiza sana lakini Act pia nyie ni wakulaumiwa mliombwa na wenzenu msishiriki uchaguzi huu mkashupaza shingo eti hamuwezi kumuachia fisi zizi wazi, kikowapi sasa? Oooh wananchi jitokezeni kwa wingi mkapige kura, hizo kura zenyewe ziko wapi? Nadhani mmjieona wenyewe.
Si sahihi kulaumiana wakati huu. ACT waliona waliyokuwa wakiyafikiria wakati huo ndiyo sahihi. Kwa sasa wamebadilisha mawazo baada ya kuona yaliyotokea. Hakuna tija kuwasimanga. Kauli walizotoa baada ya kuona yaliyotokea ni sahihi kabisa. Tuwakaribishe tu kwa kuongoka kwao na kutuunga mkono kimawazo, bila kujali yaliyopita. Yaliyopita si ndwele. Tugange yaliyopo na yajayo.
 
Sahihi, ndiyo maana nilianza na neno "inauma sana" hata kukumbushana tulipokosea na njia ya kutusahihisha. Sijawasimanga kwa nia mbaya wala kuwakebehi hapana.
 
kutoshiriki kwao kungezuia mauaji yalliyotokea?
Vyama vyote vikubwa vya upinzani (ambavyo sio proxy wa CCM) vingeungana kususiaa uchafuzi, hakika naamini CCM wangekubali kukaa mezani na haya mauaji yasingetokea.

Kwa nini damu zimwagike kisa/kwenye chaguzi!!??
 
Kitendo cha CCM kuuwa watu zaidi 1000 kibabe ni uthibitish kuwa kwenye suala zima la kuachia madaraka yao hawapo tayari kabisa na kwa njia yoyote ile. Musiwachukulie poa kabisa hao jamaa.
 
Back
Top Bottom