ACT Wazalendo yateua Jina la Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Chama cha ACT Wazalendo kimetangaza kufanya uteuzi wa jina la mwanachama anayependekezwa kushika nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Uteuzi huo umefanywa na Kamati ya Uongozi Taifa ya chama hicho katika kikao maalumu kilichoketi jana, Jumatano, Septemba 16, 2026, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya Chama, iliyopo Vuga mjini Unguja.

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa leo, Septemba 17, 2026, na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, uteuzi huo umezingatia Matakwa ya Ibara ya 72(3)(f) ya Katiba ya Chama hicho

Zaidi Soma Othman: ACT Wazalendo itaingia SUK kama haya yametekelezwa

Taarifa hiyo imeeleza kuwa jina la mteule huyo litawasilishwa rasmi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ili kukamilisha utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, Ibara ya 39(1), (2) na (3)

photo_2026-09-17_16-06-58.jpg
 
kwamba kuna mTanzania alikua anadhani kwamba ingetokea tofauti na hivyo?

sasa muda woooote walikua wanajivunga nini?

Walidhani Dr.Hussein Ali Mwinyi angeshindwa kuleta maendeleo Zanzibar pekeyake, mpaka awe na huyo kiburi?🐒
 
Kuna raia waliuawa,kuumizwa na chama kikubwa cha Upinzani kususia uchaguzi wa Mwaka 2025.

Njia ya kututoa hapa tulipokwama ni maridhiano tu
Swali ni kwamba waridhiane kuhusu nini? waliosusia uchaguzi ni shauri yao , vyama 16 vilishiriki
Nani anaridhiana na hao Wananchi
 
Taifa lina nyufa hili, zisipozibwa itatugharimu huko mbeleni.

Yaliyofuata baada ya Uchaguzi (mauaji ya kinyama) hatuwezi kupotezea kama hakuna kilichojiri.
 
Sawa! swali ni kwamba ni akina nani wanakaa mezani na kuridhiana? na wanaridhiana kuhusu nini!
Maridhiano lazima yahusishe makundi yote muhimu kwenye jamii kama vyama vya siasa, asasi za kiraia, viongozi wa dini zote, wananchi wa kawaida n.k
 
Back
Top Bottom