ACT Wazalendo yateua Jina la Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

ACT Wazalendo yateua Jina la Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

Maridhiano lazima yahusishe makundi yote muhimu kwenye jamii kama vyama vya siasa, asasi za kiraia, viongozi wa dini zote, wananchi wa kawaida n.k
Tufanye hivi makundi hayo yamekutana! watajadili nini na kati ya nani na nani.
 
Chama cha ACT Wazalendo kimetangaza kufanya uteuzi wa jina la mwanachama anayependekezwa kushika nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Uteuzi huo umefanywa na Kamati ya Uongozi Taifa ya chama hicho katika kikao maalumu kilichoketi jana, Jumatano, Septemba 16, 2026, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya Chama, iliyopo Vuga mjini Unguja.

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa leo, Septemba 17, 2026, na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, uteuzi huo umezingatia Matakwa ya Ibara ya 72(3)(f) ya Katiba ya Chama hicho

Zaidi Soma Othman: ACT Wazalendo itaingia SUK kama haya yametekelezwa

Taarifa hiyo imeeleza kuwa jina la mteule huyo litawasilishwa rasmi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ili kukamilisha utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, Ibara ya 39(1), (2) na (3)

Safi kabisa
Huu ni utekelezaji wa ushauri huu
1789675866409.jpeg
https://www.jamiiforums.com/threads...majina-ya-suk-kususa-hakusaidii-kitu.2413666/

P
 
Una hakika wamefuata ushauri wako huo au ni "mpango kazi" unafuatwa!!??
Ukishauri kitu fulani, halafu kile ulichoshauri, kikaja kutekelezwa kwa jinsi ile ile ulivyoshauri, una haki ya kusema ni ushauri wako, hata kama imetokea tuu coincidentally, na sio ushauri wako, unakula point 3 za bure za mezani.
P
 
Othman Masoud Othaman wala si jina la kuficha maana tayari alifanya kazi na Rais Hussein Mwinyi. Kama mnahofia kwamba mteuzi atashindwa kumteua si mnapiga chini SUK kila mtu ashike 50 zake.
 
Othman Masoud Othaman wala si jina la kuficha maana tayari alifanya kazi na Rais Hussein Mwinyi. Kama mnahofia kwamba mteuzi atashindwa kumteua si mnapiga chini SUK kila mtu ashike 50 zake.

Juhudi za Jussa safari hii zimelipa. Wanapokezana tu hawa Wazenji.
 
Maridhiano lazima yahusishe makundi yote muhimu kwenye jamii kama vyama vya siasa, asasi za kiraia, viongozi wa dini zote, wananchi wa kawaida n.k
Hiyo haitoshi kama yanamunufaisha mhalifu anayepaswa kuwajibika, na ndiye hasa atakuwa msimamizi wa hayo maridhiano FEKI, kama utawala wake ulivyo FEKI.

Hayo kamwe hayawezi kuwa ni maridhiano kwa namna yoyote ile.

Aje/waje watu wenye heshima na wenye kuaminika wasimamie hayo maridhiano, na hayo makundi uliyoyataja wewe hapo.
 
Kuna raia waliuawa,kuumizwa na chama kikubwa cha Upinzani kususia uchaguzi wa Mwaka 2025.

Njia ya kututoa hapa tulipokwama ni maridhiano tu
Kirahisi tu hivyo?

Kwamba "kuna raia waliuawa, kuumizwa"

Kwamba "chama kikubwa cha upinzani kilisusia uchaguzi"

Kwa sababu hizo, kuna muhimu wa kuwepo na "MARIDHIANO"?

Na watakaohitajika katika maridhiano hayo ni kama ulivyowataja hapo juu!

Naomba unisamehe, mkuu 'Proved' nikisema kuwa you're not serious.
Au labda niseme umetingwa sana na mambo mengine kulipa tafakuri sahihi swala hili zito sana.

Ni kama unachoeleza hapa ni kuwa unakubali Samia na Genge lake kunufaika na uhalifu waliowafanyia waTanzania

watu wamesababisha maovu kwa mipango yao waliyojuwa itasababisha matatizo, sasa wanakuja kutafuta njia ya kujisafisha ili waendelee, kana kwamba hakuna baya lililosababishwa na maamuzi yao mabovu tokea mwanzo kabisa, tena kwa kiburi waziwazi.
Hii dharau ya waTanzania inatoka wapi hasa? Inatokana na kuwa na hii mitutu ya bunduki?

Sasa tukikataa kuwa sehemu ya kuwasafisha damu waliyomwaga, watatuua wote?
 
Back
Top Bottom