Tufanye hivi makundi hayo yamekutana! watajadili nini na kati ya nani na nani.Maridhiano lazima yahusishe makundi yote muhimu kwenye jamii kama vyama vya siasa, asasi za kiraia, viongozi wa dini zote, wananchi wa kawaida n.k
Safi kabisaChama cha ACT Wazalendo kimetangaza kufanya uteuzi wa jina la mwanachama anayependekezwa kushika nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Uteuzi huo umefanywa na Kamati ya Uongozi Taifa ya chama hicho katika kikao maalumu kilichoketi jana, Jumatano, Septemba 16, 2026, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya Chama, iliyopo Vuga mjini Unguja.
Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa leo, Septemba 17, 2026, na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, uteuzi huo umezingatia Matakwa ya Ibara ya 72(3)(f) ya Katiba ya Chama hicho
Zaidi Soma Othman: ACT Wazalendo itaingia SUK kama haya yametekelezwa
Taarifa hiyo imeeleza kuwa jina la mteule huyo litawasilishwa rasmi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ili kukamilisha utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, Ibara ya 39(1), (2) na (3)
Safi kabisa
Huu ni utekelezaji wa ushauri huu View attachment 3672925 https://www.jamiiforums.com/threads...majina-ya-suk-kususa-hakusaidii-kitu.2413666/
P
🤣🤣Sawa! swali ni kwamba ni akina nani wanakaa mezani na kuridhiana? na wanaridhiana kuhusu nini!
Ukishauri kitu fulani, halafu kile ulichoshauri, kikaja kutekelezwa kwa jinsi ile ile ulivyoshauri, una haki ya kusema ni ushauri wako, hata kama imetokea tuu coincidentally, na sio ushauri wako, unakula point 3 za bure za mezani.Una hakika wamefuata ushauri wako huo au ni "mpango kazi" unafuatwa!!??
Mapandikizi hayo......Yanazuga eti mapinzani mchana, usiku yanakutana huko yanalamba asali
Othman Masoud Othaman wala si jina la kuficha maana tayari alifanya kazi na Rais Hussein Mwinyi. Kama mnahofia kwamba mteuzi atashindwa kumteua si mnapiga chini SUK kila mtu ashike 50 zake.
Usiniambie zile kelele za wiki mbili huko nyuma ni kwa ajili hiyo nafasi ya kwenda kuwasifisha wauajiJuhudi za Jussa safari hii zimelipa. Wanapokezana tu hawa Wazenji.
Usiniambie zile kelele za wiki mbili huko nyuma ni kwa ajili hiyo nafasi ya kwenda kuwasifisha wauaji
Hii habari imenipita pembeni...too easy.
..too soon.
Hiyo haitoshi kama yanamunufaisha mhalifu anayepaswa kuwajibika, na ndiye hasa atakuwa msimamizi wa hayo maridhiano FEKI, kama utawala wake ulivyo FEKI.Maridhiano lazima yahusishe makundi yote muhimu kwenye jamii kama vyama vya siasa, asasi za kiraia, viongozi wa dini zote, wananchi wa kawaida n.k
Kirahisi tu hivyo?Kuna raia waliuawa,kuumizwa na chama kikubwa cha Upinzani kususia uchaguzi wa Mwaka 2025.
Njia ya kututoa hapa tulipokwama ni maridhiano tu