ACT yaipongeza Tume ya Haki za Binaamu kutangaza kuchunguza mauaji yaliyotokea Kaskazini 'A' Unguja

ACT yaipongeza Tume ya Haki za Binaamu kutangaza kuchunguza mauaji yaliyotokea Kaskazini 'A' Unguja

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
WhatsApp Image 2025-01-11 at 10.07.29_0bb2883b.jpg
TAARIFA KWA UMMA

ACT Wazalendo tunaipongeza Tume ya Haki za Binaamu na Utawala Bora (THBUB) kwa taarifa yake iliyotoa kwa umma kwamba inafuatilia matukio mawili ya mauaji yaliyotokea hivi karibuni hapa Zanzibar, tukio la kwanza lililotokea Kidoti, Wilaya ya Kaskazini 'A' Unguja tarehe 09/11/2024 na kupelekea vifo vya watu 3 na tukio la pili la hivi karibuni lililotokea Kiungoni, Wilaya ya Wete, Pemba tarehe 24/12/2024 na kupelekea vifo vya watu 2.

Pia soma ~ Tume ya Haki za Binadamu (THBUB) yachunguza mauaji ya vifo vya Watu wawili vilivyotokea Pemba

ACT Wazalendo, kama chama makini cha siasa, tumetiwa moyo, nguvu na tumepata faraja kuona Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora (THBUB), imeyachukulia kwa uzito mkubwa matukio haya mawili ambayo kama Chama tuliyatolea kauli za kulaani na kukemea hadharani, huku Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa Katibu wake wa Idara ya Itikadi na Uenezi Zanzibar, wakiamua kuchagua upande wa kutetea mauaji hayo.

ACT Wazalendo tunaamini kwamba Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora (THBUB) itafanya uchunguzi huru na wa haki na baada ya kukamilisha uchunguzi wake itaweka taarifa yake hadharani na wote watakaobainika kuhusika na mauaji hayo watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Imetolewa leo,
tarehe 11/01/2025 na,

Hamad Mussa Yussuf,
Msemaji wa Ofisi, Kamati ya Wasemaji wa Kisekta - Zanzibar
 
Back
Top Bottom