Ada na gharama za kumsomesha mtoto English medium kwa miaka 4 ni milioni 10. Atachoambulia huko unakipata kwa Ras Simba kwa mwezi mmoja tu kwa laki 2

Aseeh niwe mkweli....... watoto waliosoma English medium sijui ama private zinaelewa zinafanya watoto wake kwenye kuongea aseeh humkamatii .........

Nina mifano tele...... nimemaliza karibuni tuu chuo lakini utakuta kwenye presentation mnatafuta wanao flow fluent english regardless hajui lakini lazima muwaandae ili kuonekana vizuri 👊

St kayumba fluent English ujitoe kweli kwanza honestly mtu umesoma uchagani form one mpk fom four..... Japo masomo ni English lkn ukitoka hapo ni kichaga tuu ........ ama kii raqw ama kisukuma sana sana tunaweza kiingereza cha ku ji defend kwenye mtihan Ila tufanye seriously convo ndo tunaishia yeah..... no

wakati hizo hazitakiwi kujua english ni jambo jingine na kupata maarifa ya shuleni ni jambo jingine.....

kama english sio kivutio mweke hapo mtoto wa feza primary na bunge primary magogoni uone shoo......

Kikubwa mtoto apate elimu nzuri kwa uwezo ulionao basii....
 
100% Fact.

" Somesha mtoto shule nzuri sio shule ya gharama"

Very powerful
 
Ni ulimbukeni wa baadhi ya wazazi mkuu na sasa hivi watanzania wengi wamejanjaruka hawawapeleki tena watoto wao shule za EMs na wale walio kuwa wamewapeleka shule hizo wanawarudisha Kayumba kwa wingi.

Ndio maana shule hizo zina watoto wachache sana hazina tena mvuto

Hawa wanao jifanya kukuponda hapa wanaujua ukweli ila na wao ni walimu wa shule za EM wanaogopa kufa njaa
 
100% Fact.

" Somesha mtoto shule nzuri sio shule ya gharama"

Very powerful
Shule nzuri lazima iwe ya gharama ambazo ni international na baadhi English medium tofauti na hizi za kajamba nani Kwa kiufupi kayumba school ambazo huduma yake 99%ni mbovu.
 
Acha ubahili mkuu tafuta pesa wanao wasome shule nzuri za wadosi mfano Feza n.k...hapati elimu tu bali exposure na future connections. Sijui umenielewa?....Usituone sisi tunaolipia mili 50 kwa mwaka akafikiri ni wajinga shauri yako.
 
Baadhi ya Shule zinatoa elimu nzuri sana kwa watoto sijui huko unakoishi wewe. Fuatilia shule za Roman, KKKT,Sabath utaona watoto walivyo na uelewa mzuri na kujengwa kimaadili.
 
Msimu wa kuanza shule watoto na kulipa ada mnaanza kuleta visingizio hapa ili ukajustify maamuzi yako ya kijinga.

Somesha mtoto achana na mambo ya kufuatilia maisha ya watu wengine na mambo ya Ras Simba ndugu. Shule tofauti zina exposure tofauti na hii inasaidia kwenye real life sio huko Secondary wala vyuoni.
 
January hii mnapata shida sana maana nyuzi za kulalama kuhusu hizi shule mnazifungua kwa wingi kweli
Uzuri hushikiwi bunduki kulazimishwa umpeleke mtoto kwenye hizo shule hivyo ka hela huna mtoe tu umpeleke kwa ras simba.
 
Alikuwa anaona raha kuchanganya mbegu akajizima data kuwa kila mtoto anakuja na riziki yake matokeo ndiyo hayo mtu anafungua nyuzi kibao za kulalama kuhusu kulipia elimu
 
Kwahiyo we unawahurumia wenye pesa zao kama unawatafutiaga 🤣🤣 aya peleka mtoto manzese sc na mwingine apeleke KEMEBOS tuone kama watafanana
 
Shule nzuri lazima iwe ya gharama ambazo ni international na baadhi English medium tofauti na hizi za kajamba nani Kwa kiufupi kayumba school ambazo huduma yake 99%ni mbovu.
According to kingwendu
 
Baadhi ya Shule zinatoa elimu nzuri sana kwa watoto sijui huko unakoishi wewe. Fuatilia shule za Roman, KKKT,Sabath utaona watoto walivyo na uelewa mzuri na kujengwa kimaadili.
Unazungumzia shule hizi hizi ambazo watoto wanafundishwa kuchukia watu wa dini nyingine?


Mwalimu ana waambia watoto, watoto mnaiona hii chocolate?

Hii ni ya Yesu mmesikia watoto wazuri?

Watoto: Ndioooo.


Halafu anawaonyesha mavitu mabaya mabaya kisha anawaambia mnaona hii? HII ni ya Mtume hii.

Hayo ndio maadili bora?
 
Sina uhakika na hayo? Pengine ni katika baadhi ya Shule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…