Ada na gharama za kumsomesha mtoto English medium kwa miaka 4 ni milioni 10. Atachoambulia huko unakipata kwa Ras Simba kwa mwezi mmoja tu kwa laki 2

Ada na gharama za kumsomesha mtoto English medium kwa miaka 4 ni milioni 10. Atachoambulia huko unakipata kwa Ras Simba kwa mwezi mmoja tu kwa laki 2

Hizo private hata sioni umuhimu wake NOTE. Tusomeshe watoto wetu kwenye zile shule ambazo tuna uwezo nazo achen kuiga kila January itakuwa mbaya
 
Hapo ulitakiwa uandike English fluency.
Kwa uandishi huo, bado haujakijua Kiingereza, na usijifariji kuwa mlikuwa sawa. Hapo ni wewe, achana na watoto wako ambao nao utawapeleka baadaye kwa Ras Simba
Utakosoa sana lakini ukweli unabaki palepale kuwa shule za serikali ni mbovu.english medium za binafsi wanajitahidi.
 
Ada tuweke 1.5 m

Uniforms, usafiri na vikorokoro vingine tuweke 1ml . Jumla milioni 2.5, mara 4 ni milioni 10. Hiyo ni minimum.

Hapo hatujagusa hizi International schools ambapo kwa miaka 4 hamna hamna milioni 20 inakwenda.

Form one mpaka form four nimesoma shule ambayo kulikuwa na wanafunzi wachache waliosoma English medium schools, walichotupita ni debate tu hasa ile debate ya awali kabisa.

Wale watoto hata kumi bora ilikuwa huwezi kuwakuta. Baadaye level of English fluent tukawa sawa.

Nimeenda advance nimekutana na wanafunzi ambao primary na secondary wamesoma kwenye shule za private, hawakuwa na maajabu.

Chuo nako vilevile, hajulikani aliyesoma royal schools wala hizi mushroom schools.

Kwa ambao wamemaliza sekondari au chuo kikuu na hawajui kuongea Kiingereza vizuri Ras Simba anaweza kuwanoa kwa gharama ndogo sana chini ya laki 5 kwa muda mfupi tu.

Hata mwezi mmoja unatosha kabisa.

Sasa tuseme nini ?

English medium schools ni kwaajili ya watoto vilaza au ni kwa ajili ya wazazi wasio na uelewa?”
Kwa Ras lion kuna maabara na practical tools/apparatus?

Kwa Ras lion kuna Mwl. wa hesabu,kiswahili,sayansi,uraia,historia n.k.?

Kwa Ras lion kuna Mwl. wa nidhamu,michezo,patron na matron?

Kwa hiyo jibu ni kwamba wewe ndio hauna uelewa.
 
Baadhi ya Shule zinatoa elimu nzuri sana kwa watoto sijui huko unakoishi wewe. Fuatilia shule za Roman, KKKT,Sabath utaona watoto walivyo na uelewa mzuri na kujengwa kimaadili.
Kuna team kataa shule nzuri hapo JF kwa hizo ulizowatajia lazima wazikatae
 
Utakosoa sana lakini ukweli unabaki palepale kuwa shule za serikali ni mbovu.english medium za binafsi wanajitahidi.
Hahaha naona unapigania ugali wako mwalimu wa English Medium. Wabongo wameshastuka now wanawatoa watoto huko Ems wanawaleta Kayumba.

Eti Elimu bora. Elimu bora my foot. Elimu bora unaijua wewe?
Yani wewe ndio umpe mwanangu elimu bora?
 
Hizo private hata sioni umuhimu wake NOTE. Tusomeshe watoto wetu kwenye zile shule ambazo tuna uwezo nazo achen kuiga kila January itakuwa mbaya
🤣🤣🤣🤣
 
Kwa Ras lion kuna maabara na practical tools/apparatus?

Kwa Ras lion kuna Mwl. wa hesabu,kiswahili,sayansi,uraia,historia n.k.?

Kwa Ras lion kuna Mwl. wa nidhamu,michezo,patron na matron?

Kwa hiyo jibu ni kwamba wewe ndio hauna uelewa.
January hii shule zinafunguliwa wiki ijayo watu washakula ada now vichwa vinawaka moto na unakuta mtu hakujipanga now kichwa kinawaka moto tena wa welding oxyacetylene gas na kila akigusa pa kukopa riba 20% kwa mwezi matokeo yake mtu anafungua nyuzi za kumsifia ras simba na kuponda shule za private
 
Kuna siku nimemtembelea jamaa yangu Mmoja, ambaye anawasomesha watoto wake hizi hizi shule zenu mnazoziita English mediums.

Yaani watoto ninawauliza Moja jumulisha Moja jibu ni ngapi???... Wananitolea macho tu, hawajui wajibu Nini..

Ila nilivyoanza kuwauliza one plus one... Two plus two.... Wow walifurahi hao, wakaanza kutiririka tu majibu.

Kwa hiyo nilichokiona pale, huko kwenye hizo English medium schools kubwa zaidi watoto wanachofundishwa ni kuzoea matumizi ya lugha ya kingereza tu basi... Hakuna kingine Cha maana, na elimu Bora haiko hivyo
 
Gharama za kumiliki gari kwa mwezi ni laki 3 za mafuta, wakati unaweza kupanda daladala kwenda na kurudi kila siku buku mbili jero na kwa mwezi 30,000 tu. Mawazo yako hayajatofautiana sana na haya.
🤣Kila mtu ashinde mechi zake
 
Kuna team kataa shule nzuri hapo JF kwa hizo ulizowatajia lazima wazikatae
Sio mbaya kama kila mtu akifanya kile kinachomfurahisha 😅😅😅ili mradi tu awe na Akili timamu
 
Mtoto kama unaweza msomesha shule nzuri msomeshe. Nimesema shule nzuri siyo shule ya gharama. Hata kama ni ya serikali ila nzuri, tumia gharama kuhakikisha anasoma hapo.

NB: Shule za kisasa si za kukariri miguu ya panzi kama kipindi chetu. Wazazi tufahamu mahitaji ya kisasa, Halafu shule siyo kujua kingereza tu. Kingereza ni lugha.
Kizuri gharama, ila sio vya gharama vyote ni vizuri.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Watu badala ya kuwekeza kwenye viwanja na assets nyingine baadae watoto wao wakimaliza chuo wawape mitaji kwa kuuza baadhi ya hizo assets mijitu inaishi maisha ya kufake( FASHION LIFESTLE) haya tukutane uzeeni.

Ambapo wasomesha watoto English medium watakuwa wanalialia hovyo kuwa serikali itoe ajira😄😄😄😄 huku mitoto yao mibroila ikiwa bado haijatoka majumbani bado wapo wanakula kulala kwa wazazi.

Watanzania shtukeni acheni kupoteza pesa na kutajirisha wamiliki wa hizi shule. Na bado mitoto inatoka huko english medium unaingia garama tena za tuition😄😄😄na ENGLISH YAO BROCKEN.

1.Huo muda wa pre form 1 na pre form 5 wakati wa LIKIZO ZA KUSUBIRI MATOKEO pelekeni watoto VETA.Huko wachukue ujuzi utakao wasaidia wakishamaliza hizo elimu zao za chuo.

2.Pesa mnazoenda kutupa huko English medium wekezeni kwenye assets kama viwanja,mashamba, kununua bond za serikali na hisa katika kampuni zisizopata hasara😄😄😄 acheni UBINAFSI na uchoyo kama nyie hamkuandaliwa URITHI basi jitaida WATOTO wako na vijukuu na vitukuu vije vikukumbuke hiyo ndo legacy💪💪💪

Kuna shule nyingi tu ada chini ya millioni 1 zingatia zenye ufaulu wa wastani kupanda juu kama huko huwezi mpeleke kayumba ila ongeza usimamizi na mwalimu wa ziada wa kumboost.

#kumpa mtoto Elimu ni wajibu,elimu sio urithi!!!
 
Aseeh niwe mkweli....... watoto waliosoma English medium sijui ama private zinaelewa zinafanya watoto wake kwenye kuongea aseeh humkamatii .........

Nina mifano tele...... nimemaliza karibuni tuu chuo lakini utakuta kwenye presentation mnatafuta wanao flow fluent english regardless hajui lakini lazima muwaandae ili kuonekana vizuri 👊

St kayumba fluent English ujitoe kweli kwanza honestly mtu umesoma uchagani form one mpk fom four..... Japo masomo ni English lkn ukitoka hapo ni kichaga tuu ........ ama kii raqw ama kisukuma sana sana tunaweza kiingereza cha ku ji defend kwenye mtihan Ila tufanye seriously convo ndo tunaishia yeah..... no

wakati hizo hazitakiwi kujua english ni jambo jingine na kupata maarifa ya shuleni ni jambo jingine.....

kama english sio kivutio mweke hapo mtoto wa feza primary na bunge primary magogoni uone shoo......

Kikubwa mtoto apate elimu nzuri kwa uwezo ulionao basii....
My friend Lugha yoyote duniani unajifunza muda wowote na lugha ni kuongea.Nakuhakikishia hata leo ukitaka kujifunza lugha mpya yoyote unaweza ila jitihada zako katika kuiongea ndo itafanya uwe fluent.

Mimi nilikuwa najua kingereza cha kuombea maji ila nilifika hatua nikasema nataka nijue kingereza chenyewe na niwe fluent na pia niwe na confidence ya kutosha nikaweka mikakati ya kujifunza misamiati mipya na ya kisasa na kutafuta watu wa kuongea nao kupasua yai hahahaa na nimefanikiwa.

Mademu ni wazuri sana wa lugha so kama vipi unaweza ukawatumia kujibrashbrash lugha inase kichwani pia kama unamarafiki wa nje ya nchi nao jitahidi uwe unaongea nao kujiboresha zaidi.

#kupanga ni kuchagua!!!
 
Naunga mkono hoja ndo maana nikasema....... lazima ujitoe hasa hapo juu
 
Kwa Ras lion kuna maabara na practical tools/apparatus?

Kwa Ras lion kuna Mwl. wa hesabu,kiswahili,sayansi,uraia,historia n.k.?

Kwa Ras lion kuna Mwl. wa nidhamu,michezo,patron na matron?

Kwa hiyo jibu ni kwamba wewe ndio hauna uelewa.
Hivyo vitu ulivyotaja havipo kwenye shule za serikali?
Kwa Ras Simba nimeongelea issue ya English language
 
Back
Top Bottom