Tetesi: Adaiwa kuficha tani tele za sukari Moshi

Tetesi: Adaiwa kuficha tani tele za sukari Moshi

hamna mwenye jeuri hiyo maana biashara ya chakula market size yake ni kubwa zaidi ya bakhressa na gulam dewji wa METL
Lakini mpaka hapo naamini kuwa amepata mbadala wa kumfanyia kazi huyu jamaa. Kaua watu wengi sana, huyu jamaa anajulikana kwa kuagiza sukari mbovu na ndiye nadhani magufuli alikua anamzungumzia. Huko nyuma sukari yake iliunguzwa moto lakini watu walikufa pia katika mazingira ya kutatanisha, kuanzia mkemia na hata maaskari huyu ni Mafia ila moto huu wa Magufuii lazima ataungua nao.
 
Wasaalam wana jamvi!
Kwanza nianze kumpongeza Rais wangu mpende John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anayo endelea kuifanya!

Ikumbukwe kwamba lengo la Rais kusitisha uingizwaji wa Sukari kiholela ilikuwa ni kulinda viwanda vya ndani na kulinda uchumi wa ndani pia!
Lakini pamoja na juhudi hizo za Rais kuna kikundi kisicho itakia mema nchi hii kimekuwa kikificha sukari ili kuonesha kuna uhaba na hivyo wananchi waichukie sekari yao!
Baada ya Rais kusema wazi ata hakikisha anapambana na wafanya biashara wanao jaribu kuhujumu uchumi na kuihujumu serikali kwa kuficha sukari ...leo hii Rais akiongea na wana Arusha amesisitiza tena asipewe lawama atapo washughulikia wahujumu uchumi hasa wanao ficha sukari ili serikali ionekane ni mbaya na haiwapendi wananchi wake..

Rais Magufuli amesema wazi kuwa leo hii atakamatwa mfanya biashara mwingine mkubwa huko Arusha kwa kuficha sukari nyingi sana na amesema amesha wakabidhi jeshi la polisi jukumu hilo kuhakikisha wana wakamata wote wanao ficha sukari!

Pia Rais amesema serikali haitoshindwa kamwe na hawashindwi kuagiza sukari lakini hawawezi kuwaacha watu wachache wahujumu uchumi kwa kuficha sukari na ameahidi kupambana na wahujumu uchumi!

Mwisho nampongeza tena Rais kwa kuendelea kuwanyoosha watu na kuto muonea huruma yeyote asiye itakia mema nchi hii..Mimi naomba ikiwezekana wanao kamatwa wafutiwe kabisa leseni za kufanya biashara ya aina yeyote kabisa hapa nchini!

Mungu ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais John Pombe Magufuli!

Karibuni wana jamvi
Swali kuntu ni je ataweza kupambana na MO??
 
Nilikupuuzia kwa kuwa ulikuwa haujibu hoja zangu. Bila kujali Tanzania ipo katika mfumo gani wa uchumi, iwe capitalism, socialism au mixed economic system, ni vyema ujue mfumo wowote huwa unalazimishwa na sheria zilizopo. Huwezi ukawa unajiita kuwa upo na socialism wakati sheria za nchi hazilazimishi huo mfumo, the same to capitalism and mixed economic systems. Ndio maana wakati wa ujamaa na kujitegemea kulianzishwa Azimio la Arusha ili sheria ziendane na lengo.

Sasa nakuja kwenye hoja yangu ambayo hupendi kuijibu wala kuisikia. Je, kwa mfumo wa uchumi tulionao (bila kujali ni upi), sheria zake zinakataza mtu kuhifadhi katika ghala lake shehena ya bidhaa au malighafi anayoitumia kutengenezea bidhaa nyingine? Je, kuna sheria inayowakataza watengenezaji wa juisi, lambalamba na tamutamu nyingine kuhifadhi katika ghala zao sukari ambayo ni malighafi ya kutengenezea bidhaa zao? Naomba jibu uniwekee kifungu cha sheria, sio uniwekee definition ya economy system
1462611681406-jpg.345374


Maswali yako yote yanajibiwa na article hiyo hapo juu
 
Maswali yako yote yanajibiwa na article hiyo hapo juu
Haya, baada ya kuonekana kuna sheria, ni nani mwenye mamlaka ya kuthibitisha kuwa sheria imevunjwa? Ni nani anayethibitisha kuwa huyu ameitunza sukari ili aje aiuze kwa bei ya juu AU ni kwa ajili ya malighafi ya bidhaa anazozalisha? Ni nani mwenye mamlaka ya kutoa adhabu kwa mkosaji? Nani anathibitisha kuwa sukari ipo stocked lawful or unlawful? Kugawiwa bure kwa sukari sio hukumu na adhabu hiyo? Nasubiri jibu
 
Kauze yako! Mbona una akili primitive namna hiyo?! Kwenye biashara hakuna neno jamii: kuna bidhaa, wateja, na soko na ukipenda sema kuna bidhaa na soko tu! Badilika! Chukua hii misemo ikusaidie: 1. "simple minds discuss people" .2. "Ordinary minds discuss events" .3. "Great minds discuss ideas" .4. "Great minds turn problems into opportunities".

Kasome kitu kinaitwa "Commodity Hoarding" and "Laws and Economy of commodity hoarding" haswa kwenye food commodities..
 
Uenyekiti si ndo huo JK kang'ang'ania???. Pagumu sana huko ccm.... CCM ina wenyewe na JPM hajawahi kuwa kwenye hilo kundi la wenyewe.....
......Ila AKIINGIA atakuwa Mwenyewe wa Chama na WENYEWE orijino hawatakuwa tena WENYEWE..
 
Kauze yako! Mbona una akili primitive namna hiyo?! Kwenye biashara hakuna neno jamii: kuna bidhaa, wateja, na soko na ukipenda sema kuna bidhaa na soko tu! Badilika! Chukua hii misemo ikusaidie: 1. "simple minds discuss people" .2. "Ordinary minds discuss events" .3. "Great minds discuss ideas" .4. "Great minds turn problems into opportunities".

Mtatafuta nchi ya kwenda kufanya huo upuuzi wenu. Walah naapa mtahama msipokubaliana nasheria za nchi hii. Siyo lazima mfanye biashara hapa kwetu.
 
Mkuu wewe nahisi haupo kwenye hii biashara ndio utaona kama bla bla,mimi nina duka la jumla na anaye supply bidhaa kwenye duka langu ni mo,zakaria,bakhresa,sayona(matosun group etc na naletewa bidhaa na hao kupitia mobile truck zao mwezi wa pili sasa wanasema sukari hawana,je kama umeangalia clip ya mhe.rais anavyowahutubia wananchi wa katesh unahisi wanaongelewa walioficha sukari kule mbagala na yule aliyelipia sukari kilombelo ila ataki kuuza kwa wananchi? Unahisi wewe na rais nani anajua mwenendo mzima wa hii ishu? Msipende kupinga kila kitu,rais kaongea vitu sisi wengine tulikuwa atuvijui,sasa katufungua masikio na tunajua wanaomhujumu,eti matajiri wengine wanajigamba kwenye majarida ya forbes,hadi tunaambiwa bilionea kijana wa afrika ukiangalia utajiri wao wakimagumashi,wahujumu uchumi,wakwepaji kodi wakubwa,wazajilishaji na wahuzaji vitu fake....

Umezungumza vema ndugu yangu
 
Kwani ni lazima kuuza? Kama ana mpango wa kuiuza nje ya nchi kwa nini alazimishwe? Mbona Bakhresa anasafirisha unga wa ngano nje ya nchi? Huu ni utawala wa kisheria, enzi za Ujamaa na Kujitegemea zilishazikwa na Azimio la Zanzibar, acheni watu wawe huru kuuza na kununua au kuhifadhi kadri wanavyotaka. Si tumeambiwa kuna shehena inakuja, au nahodha amebadili gia katikati ya bahari?
Mkuu wakati mwingine ni vyema kukaa kimya kuliko kuchangia,unajua sheria inasema nini kuhusu commodity hoarding during scarcity? Unataka utawala wa sheria wakati unatetea uvunjifu wa sheria!
 
Atakimbizana na sukari kwa miezi mitatu hadi minne, akishtuka mwaka umekatika na huku mtaani "afadhali ya jana"

Mwambieni jpm kwa upole kabisa kuwa huu mchezo hautaki hasira. samaki alishakauka kitaaambo asifanye jitihada za kumkunja, aangalie namna ya kumkaanga bila kumkunja.
mkuu we ndo huna ujualo....nadhani ii ishu ni very minor we huoni ishu kama hii anaitolea tamko huko barabarani na watekelezaji wake ni kamati za usalama za mkoa....kifupi Tanzania sio kichaka cha bush beparis tunataka modern ambao wanatambua social responsibilities!!
 
1: MO kutokana na uchache wa sukari ya ndani amekuwa akitegemea sana kuuza sukari ya kutoka Thailand, Brazil na India na sukari yake huiuza bei ya chini kidogo kuliko wengine, baada ya vibali kusitishwa Mo amekua akiuza sukari ya TPC pekee maana Mtibwa ilipotea tangu february.
3: Kwa wafanyabiashara wengine sijui lakini Mo haleti sukari ilio expire watu wasiingize siasa katika hili imagine sukari inashushwa bandarini hadharania wakiwepo watu wa TFDA na TBS, inasombwa kupelekwa kwenye maghala hadharani na godowns za Mo hazina usiri wowote. Mtoa mada atueleze ni godown au ma godown yapi sukari ilipofichwa ili mimi nimsaidie yeye au mwingine atakaependa kuingia katika ghala hilo na ajithibitishie kwamba sukari haijafichwa. NB: usitake kujua mimi ni nani MeTL.

Mydear Ni kweli sukari iliyo expire iliingia nchini na hao TFDA na TBS wakiwepo na ilitumiwa na watanzania nikiwemo Mimi Kwa bei unayoita Ni rahisi kabisa na tulitumia sukari za viwandani (pipi na vinywaji) Kwa kutumia Kwa chai Kwa sababu zilimwagwa hovyo mitaani na hao TBS na TFDA walitumia pia majumbani kwao
Na bandari inayopitisha mizigo yote Ndio Hiyo Hiyo ilinuka kabisa ukwepaji kodi wa hadharani ambako na Hiyo sukari ilipita. Ni utetezi hafifu Sana umejitahidi kutoa Kwenye hili ndugu Ni wazi hawa afanyabiashara wakubwa wa sukari wasigeuze shingo zao kujifanya hayawahusu wanahusika na yote haya na hadi sasa wameificha Kwa sababu zao bado watanzania wanahangaika na bei ya 2700 -3000 elfu Kwa kilo wao wanaona burudani kabisa Kwa kuwa wenye shida, taabu na mateso Ni sisi

Kwa niaba ya unaowatetea waambie Asante Sana wamefanikiwa kututesa waendelee hivyo hivyo wafiche hadi chumvi na mafuta.
 
Mkuu wakati mwingine ni vyema kukaa kimya kuliko kuchangia,unajua sheria inasema nini kuhusu commodity hoarding during scarcity? Unataka utawala wa sheria wakati unatetea uvunjifu wa sheria!
Unathibitisha vipi kama mwenye shehena ni muuzaji au mtumiaji; kwa kumpeleka mahakamani au kwa kuigawa bure hiyo sukari yake? Haya basi tupeni sheria na utaratibu wa kugawiwa bure hiyo sukari
 
Back
Top Bottom