Adaiwa kutumia jina la William Lukuvi kujipatia Tsh. Milioni 2.1

Adaiwa kutumia jina la William Lukuvi kujipatia Tsh. Milioni 2.1

Yaani kaenda kufanyia utapeli wake ndani ya ukumbi wa polisi.
Kweli ana kipaji kizuri sana naamrisha ataifishwe kila alichonacho kuanzia mkewe hadi yeye mwenyewe awe mali ya wote (umma)
 
Mjinga akiingia kwenye 18 we piga tu

Ova
 
Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mtu mmoja aliyejifanya kutumia jina la aliyekuwa Waziri wa ardhi,William Lukuvi na kwamba amemtuma na kuendesha mafunzo ya ujasiriamali visivyo halali Mkoani Kilimanjaro katika ukumbi wa polisi Moshi na kujipatia Tsh. Milioni 2.1 kwa wanafunzi wajasiriamali kama gharama za cheti.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Simon Maigwa amethibitisha kukamatwa kwa mtu huyo, akisema alikuwa akijipatia Sh35,000 kwa kila mshiriki wa mafunzo hayo huku akiwaahidi kuwalipia kila mmoja Sh300,000 kama ada baada ya kuhitimu mafunzo hayo na kwamba atawapatia ajira.

Kamanda Maigwa amesema baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema wakati akiendesha mafunzo hayo katika ukumbi wa polisi Moshi, Jeshi la Polisi lilitumia mbinu za kumnasa mtu huyo.

"Baada ya kupata taarifa hizi jeshi la polisi tuliwasiliana na viongozi ambao mtuhumiwa huyu alikuwa akiwataja ambapo walimkana na kwamba hawamjui, hivyo tunaendelea kumshikilia kwa hatua zaidi," amesema Kamanda Maigwa.

Mtuhumiwa huyo amekuwa akiendesha mafunzo hayo ya ujasiriamali katika mikoa mbalimbali ya Dar es salaam, Tanga, Morogoro, Arusha, Mbeya na Tanga kwa kujipatia kipato isivyo halali.
Kaja kupiga somo ktk ukumbi wa polisi dah.
 
SEMA JAMAA KAWAFUNDISHA SOMO LA UJASIRI, HAO WAJASIARIAMALI
 
Back
Top Bottom