Lazima watu wajifunze kuishi, na kuwaacha wengine waishi. Upevu wa akili na ustaarabu ni pamoja na kukubali tofauti miongoni mwa watu.
Kuna vilema na walio wazima, kuna wakristo na waisilamu, kuna wapagani na wenye dini, kuna waabudu mizimu na wachawi, kuna warefu na wafupi, Kuna waarabu na wachina, kuna wazungu na waafrika.
Uvumilivu na upendo juu ya tofauti hizo ndio umeifanya dunia iwe hivi leo!!! Utu, heshima, haki, na wajibu ni nyenzo za msingi kuifanya dunia iwe sehemu salama ya kuishi.
Ubaguzi wa aina yoyote, chuki, hasira, husuda, unyanyapaa, na kunyooshea vidole wengine haviwezi kuijenga dunia yenye usalama.
Vizazi huja, vizazi huondoka, miongoni mwao mashoga wakiwemo. Watoto, wadogo zako, ndugu zako na wajukuu zako hawako salama sana kuuepuka ushoga. Mtu yeyeto anaweza kutokea kuwa shoga.
Mimi sifikirii kabisa kwamba ushoga ni jambo la kukera. Halikeri kwasababu halimuhusu wala halimdhuru asiyelifanya.
Watu wawili wenye utashi na maamuzi huru, wakikubaliana kupendana na kuitumia miili yao kwa namna wanayoitaka, kwanini imuumize mwingine!!!