Addiction ipi ina arosto kali ukiikosa hata kwa siku moja kiu yake ni ngumu kuikabili?

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
  • Kucheza kamari - Kubeti mpira siku zenye mechi, Kindege, n.k.
  • Pombe
  • Sex
  • Punyeto
  • Sigara
  • Bangi
  • Ugoro

Pombe nimewahi kushuhudia kuna jamaa hio siku arosto zilimkamata sana na hana pesa, akili zilifyatuka aliiba simu ya rafiki yake. hakupoteza muda, alienda kuiuza kwa bei ya kutupa, halafu akanyoosha moja kwa moja hadi kwenye viti virefu.

Rafiki yake alipotushirikisha na kuhakiki simu imeibiwa wala hakupanic. Ulianza msako wa kumsaka kwenye bar, alikutwa akiwa amelewa chakari.

Kesho yake alizinduka na kichapo cha maana, akaambiwa aonyeshe alipouza simu, kwa bahati nzuri hata walionunua walijua itafatwa tu, waliirudisha walipopewa hela yao
 
Sigara mtu wangu sigara, mtu anaweza sema kaacha akakaa hata miezi ila siku anakuja kuvuta tena na ina alosto ya ajabu .
unaona wengine wakiwasha sigara huku wamekinga njiti za viberiti kwa viganja zisipigwe na upepo… πŸ˜…

Vile tu sigara inawaka, wanavuta lile pafu ya kwanza na moshi unavyotoka wanaurudisha tena, hapo uvumilivu unaweza kuisha.
 
Pombe ndiyo yenye withdrawal/β€œarosto” kali zaidi na inaweza kuwa hatari kiafya kwa mtu aliyezoea kunywa sana. Sigara pia craving yake huwa kali, lakini withdrawal yake si hatari kama ya pombe. Kamari na punyeto zaidi ni utegemezi wa kisaikolojia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…