JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
MAKOSA YA UCHAGUZI
Kwa mujibu wa kifungu cha 89A cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, sura ya 343 na kifungu cha 88A cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, sura ya 292, Maafisa Uchaguzi watakaofanya kwa makusudi vitendo vitakavyosababisha matokeo ya uchaguzi kutenguliwa watashtakiwa.
Iwapo watapatikana na hatia watapewa adhabu ya kifungo kisichopungua mwaka mmoja na kisichozidi miaka miwili au faini isiyopungua shilingi laki tano (500,000/=) na isiyozidi shilingi milioni moja (1,000,000/=) au vyote kwa pamoja.
Kwa mujibu wa kifungu cha 89B cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na kifungu 88B cha Sheria za Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, Afisa Uchaguzi atakayeisababishia Serikali hasara atatakiwa kufidia hasara hiyo kwa mujibu wa Sheria ya The Public Officers, (Recovery of Debts) Act, Cap. 76.
Kwa mujibu wa kifungu cha 89C cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na kifungu cha 88C cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, Maafisa Uchaguzi ni pamoja na:-
(i) Mratibu wa Uchaguzi wa Mkoa;
(ii) Msimamizi wa Uchaguzi;
(iii) Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi;
(iv) Msimamizi wa Kituo cha Kupigia Kura;
na (v) Msimamizi Msaidizi wa Kituo cha Kupigia Kura.
Pamoja na makosa tajwa hapo juu, Msimamizi wa Uchaguzi anatakiwa aelewe makosa mengine ya uchaguzi ambayo ni pamoja na:-
(i) Afisa wa Umma kutumia wadhifa wake kumkatisha tamaa mtu anayetaka kugombea;
(ii) Makosa yanayohusiana na fomu za uteuzi, karatasi za kura na masanduku ya kura kwa mfano:-
(a) Kuharibu karatasi za uteuzi kwa makusudi;
(b) Kughushi fomu za uteuzi;
c) Kughushi Karatasi ya Kura;
(d) Kuharibu Karatasi ya Kura kwa makusudi;
(e) Msimamizi wa kituo cha kupigia kura kuacha kugonga muhuri wa kituo kwenye karatasi ya kura kwa uzembe;
(f) Kutoa karatasi ya kura kwa mtu asiyehusika kinyume cha sheria;
(g) Kufungua sanduku la kura kinyume cha sheria;
(h) Kutangaza kwa makosa kujitoa kwa mgombea;
(i) Kutoa kiapo cha uongo; na
(j) Kutoa au kupokea rushwa.
Mtu yeyote atakayepatikana na hatia atapewa adhabu zilizotajwa katika Sheria za nchi.

Upvote
4