Adhabu kwa Simba

kidunula1

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2016
Posts
6,305
Reaction score
6,341
Nashauri ingekuwa hiviiii!!

Kwa kitendo cha Washabiki wa Simba kuharibu viti uwanja wa taifa ilihali havikuwa na uhusiano wowote na tukio lililotokea uwanjani, TFF wangewapiga fine Simba ya fedha tasilimu,pamoja na kuwapa adhabu ya kucheza michezo mitano au zaidi bila ya washabiki wao. Hivi vitendo vikifumbiwa macho na kutolewa vi fine uchwara hvi kuna siku atakufa mtu uwanjani!
 
Japo kuwa refa na rise man wake waliboronga jana,lkn hamna mahusiano kati ya kuboronga kwa refa na kutuharibia uwanja wetu. Simba hili tukio ni la pili ukiacha la kwanza na kagera sugar waling'oa viti na jana wanafanya hivyo hivyo. Wiki kama mbili walilalamika uwanja wa uhuru si mzuri kutokana na nyasi bandia wakakubaliwa kutumia uwanja wa taifa, sasa jana wamefanya uchizi wa kiwango cha PhD, mimi kama ningekuwa TFF ningewapiga marufuku kutumia uwanja wa taifa kwa msimu mzima, wakatumie uwanja ule wa uhuru na kitendo alichokifanya mkude cha kihuni, kwani yy ni professional lkn anatabia za wachezaji wa ndondo. Duniani kote marefa kukosea kitu cha kawaida (refa nae binadam) chukulia kama mechi ya msimu uliopita EPL London derby mechi kati ya chelsea na Arsenal, kitendo cha kihuni alichofanya Costa lkn kadi akapewa Gabriel, lkn kuanzia wachezaji mpaka mashabiki hawakureact kihuni kama jana walivyofanya mashabiki na wachezaji wa simba. Narudia tena Simba inabidi wapewe adhabu kali sana tena sana, iwe fundisho ili wasirudie tena na mwamuzi nae apewe adhabu kali kwani nae mechi ya pili hii anaboronga (aliboronga mechi msimu uliopita kati ya yanga na cost Union).
 
Unapotoa hukumu lazima ujiangalie na wewe mtoa hukumu kama huna makandokando ila kwa mechi ya jana TFF ndo wamebeba lawama na walistahili ndomana Simba wamepewa adhabu hiyo japo walichokifanya Simba si Uungwana lakini kwenye mpira hicho ni kitu cha kawaida mana kuna nchi zingine mashabiki wenye hasira za mbwa wanawekewa hadi nyavu mfano mzuri ligi ya Argentina,Italy na Uturuki kidogo
 
Wewe unayeitetea tff na kuikandamiza simba nina uhakika hujacheza mpira wala hupendi mpira toka moyoni au utakua uoande wa pili tofauti na simba, hivi kabla mashabiki hawajavunja viti lazima ujiulize kwa nini wavu je viti?? Goli lao halali limekataliwa, mtu anashika mpira kwa mkono kabsa na kila mtu ameliona jambo hilo refa na linesman wake ambao wte wawili wapo ndan ya nusu ya simba eti hawajaona na wanakubali ni goli.. Kma unapenda mpira kwa dhati unajua tempo ya mpira na ndo maan mashabk wa simba walifanya vile japokuwa hakuna anayesapoti kilochofanyika.. Ila kwa nini kimefanyika?? Kwann kila siku TFF na yanga tu?? Kuna maslahi gan hpo kati, na ndo maan watimu hta wakitoka nje wanaishia kututia aibu tu, we jiulize kwa nini kila siku yanga tu??
 
Kwenye Tennis hakunaga kuiba kijinga jinga kama hivi.

Football waige mfano huo.
 
Kufanya fujo kulichangiwa na maamuzi mabovu ya martin saanya na wasaidizi wake, kwakweli wametuangusha sana wapenda soka ila kuvunja viti ni kutojitambua kwa walengwa na waliohusika moja kwa moja .. Tff iwe na mfumo mzuri wa uteuzi wa waamizi kwa kuzingatia weledi na sifa na uwezo wa kumudu michezo mikubwa kama ule.
 
TFF wanaendesha Maisha yao kupitia hao simba, hawana jeuri ya kuban washabiki hata wangevunja viti vya uwanja mzima,
Uharibifu wa namna hii alitakiwa kulipa refa mwenyewe na tiefuefu wenyewe
 
Kama vipi na Martin Saanya apewe tuzo kama Jecha,si ndiyo utamaduni wetu wa kutoa tuzo kwa watu wanaobolonga mambo?Naiomba serikali yetu ya BOMBADIA iiagize TFF impe tuzo Saanya kama ilivyoiagiza Serikali ya ZNZ kumpa tuzo Jecha.
 
Mm ni shabiki wa mnyama Simba ila kile kitendo cha kung'oa viti sijakipenda. Sio ustaarabu kabisa,mambo yaliyotokea jana na refa kuruhusu goli la Yanga ni kawaida tu ktk michezo. Sijui sheria zinasemaje tukio km hilo likitokea. Tuwasubiri TFF
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…