Adhabu ninayoipata tangu nihamie chumba cha master, nipeni maujanja

Nimecheka sana leoπŸ˜›πŸ˜›πŸ˜›πŸ˜›πŸ˜›πŸ˜›πŸ˜›πŸ˜€
 
Tatizo sio choo,wewe itakua unakula sana maharage na dagaa
 
Mkuu, kama ukiweza mwambie mwenye nyumba abadikishe mfumo wa maji taka na aweke hiyo pipe Kama ni choo cha kuchuchumaa, lakini kama ni choo cha kukaa aweke cha kufanana na hiyo niliyo ambatanisha pichaView attachment 1591530View attachment 1591531
Nimewaelewa vizuri sana wakuu.

Isipokua me naona kama nimemuelewa mtoa mada tofauti.
Tatizo lake sio harufu kutoka kwenye shimo kurudi ndani, maana kwa ushauri wenu hapo juu, mmemshauri kutatua tatizo la harufu kutoka septic tank kurudi ndani.

Yeye anatatizo la harufu kutoka kwenye uchafu fresh kutoka tumboni ukiwa kwenye sink, kabla yakwenda kwenye septic tank. Kawaida hii harufu haitakiwi kurudi chumbani, inatakiwa kuisha ikitokea kwenye ventilation za chooni

Amesema hivi..
Kila akitoka kukata gogo harufu inarudi chumbani, sio harufu yakutoka kwenye shimo, ni harufu ya kinyesi kipya kinachokua kwenye sink, kabla hakijaenda kwenye shimo
 

hii P-trap au S Trap ni ya dongo ulaya wengine wanaita ceramic mtaani zipo nzuri za orange na bei yake haivuki 3,000 kote kwenye maHardware, unachotakiwa unakata kakipande kengine ka bomba hilo la upana wa inchi 4 angalau urefu wa inchi 4 unabandika juu yake halafu unaweka choo cha kuchuchumaa Eastern Type, hicho kilichoongezeka kinaficha mzigo uliouweka na hakihitaji maji mengi kuuondoa mzigo unakutana na maji ambapo maji hayo yanakata harufu kabisa CHOO HIKI HAKIFAI KWA MASTER KABISA
Choo cha kukaa Western Type ndio kinatakiwa kukaa kwenye master na majengo yote ya ghorofa P-Trap yake imejengewa mumo humo ili maji yatuwame kukata harufu, sasa hapo maji lazima yawe mengi ili kuflash

S or P Trap
An S-trap or P-trap refers to the water seal at the bottom of the toilet that stops sewer gases and smells escaping into your bathroom. The set out of a toilet outlet refers to the outlet drainage point location.
 
Sawasawa kabisa mkuu,na azingatie sana ulichokiandika hapo paragraph ya mwisho.
 
Zoea tu mkuu hii harufu ya kimba ndio how you smell in the inside
 
Nina mawazo ya tofauti kidogo mkuu, masink yote huwa yanasetiwa na kitu inaitwa P-trap au S -trap. Hii kazi yake ni kubakiza maji kwenye mfumo/njia nzima ya maji taka kati ya inlet na outlet(kwenye shimo au sewer). Hivyo hakuna harufu inayotoka kwenye sewer (bomba la maji taka la moja kwa moja bila septic tank) kurudi ndani ya nyumba.
Kwa ufupi ajitahidi tu usafi + perfume/air freshner. Zipo nyingi tu mbona.
 

Mkuu upo sawa kiasi but fanya uchunguzi wako vizuri, hakuna kinachoishinda harufu ya kinyesi, septic tank likichemka kisawa sawa mchana kutwa na jua la bongo linavyowaka kama hakuna njia ya kupumulia nje ya line ya kurudi ndani tule tumaji tunakobaki kwenye sink hugeuka uchafu na kutoa harufu mbaya kama shimo la choo limehamia ndani.

Na siku hizi ukikutana na mafundi wazuri wanashauri kuwekwa pipe line mbili kwa ajili ya shimo kupumua, moja kwenye shimo lenyewe na nyingine katikati ya chamber A&B, au hizi nyumba za kisasa tunazojenga zenye vyoo ndani bomba za kutoa harufu nje iwekwe moja kwenye septec tank yenyewe na moja katikati ya choo cha master na choo cha public au kama vyumba vyote vina choo pipe iwekwe kwenye chamber ndogo zinapokutana line zake pamoja na kwenye sink ziwekwe hizi P/S trap,hapo inakuwa shwari mno!
 
Tena wakati mwengine bila hata harufuu dawa ni maji mengi kama choo hakina tatizo
Kwanza shida kuu hapo hakuna P trap ya kudaka maji ili harufu from septic tank isije ndani. Pili kama ni choo cha kuchuchumaa jitahidi uwe kila mzigo ukidondoka mwaga maji ili harufu isisambae. Hapa ndiyo utaona faida ya choo cha kukaa maana mzigo ukishuka unatua kwenye maji kabla harufu haijasambaa.
 
Wengi hawajaelewa mada.

Anyway, suluhisho hapo ni kujitahidi kula matunda na maji kwa wingi. Pia jitahidi kupunguza kiwango cha chumvi kwenye chakula. Nadhani itasaidia
Acha uwongo, bora ungesema ale mbogamboga kwa wingi...
 
Tumia maji mengi Ku flash choo na pia nunua sabuni za chooni zinatosha tuu , Kama unaishi sehem maji ni ya shida, hama hapo haraka
ahsante mkuu japo nilitaman kujua aina ya sabun mnayotumia ninyi ili nami niitafute maana natumiaga deto ila naona kama sijarizika nayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…