Adhabu ya Bunge kwa Mpina inatoa taswira halisi jinsi gani Bunge na serikali ya Tanzania inavyowaona wananchi

Naomba kuuliza hata asipohudhuria, ila posho ya kila kikao si anapata km kawaida au?
 
M
Ukiona mwenge unakuja mjini kwako kimbia halaka eneo hilo
 
Dawa yao ni kuwapiga chini wote 2025
 
Hapo ndo unagundua mpina alikua sahihi kuidrop ile report kwa Uma. Kwa sababu alijua hakuna hatua, bunge/Mahakama/Rais wangechukua.

Kwa akili ndogo, Serikali inapuuza report ya CAG na mapendekezo yake ya wazi, ndo ije itetereke na report ya mpina 🤣

Sijawai kuandamana. Ila wangesema tuandamane kulishinikiza bunge, kumrudisha bungeni mpina ningeandamana.
 
Kwahiyo ushahidi wa Mpina umezimwa! Hautajadiliwa.
Hilo ni lazima lilikuwa na maagizo, na Mpina kuongea na waandishi ilikuwa ni loop hole waliyoipata. These people are so so so evil!

Mtu kama Jerry Rawlings wa Ghana alipokamata madaraka alipiga sana risasi watu, akidai walihusika na mambo kama yanayofanyika sasa Tanzania. Akazua mjadala mkali kama alichofanya ni sahihi au la. Siku zote nilimlaumu Rawlings kwa alichofanya, lakini sasa naanza kuona kama he had a point
 
Dawa yao ni kuwapiga chini wote 2025
Sio kwa wapiga kura wa Kitanzania. Umeona signature yangu inavyosema? Nilishasema humu ndani kwamba tatizo la Tanzania ni kwamba karibu 70% ya wapiga kura ni political semi-illiterates, na karibu 80% ya political literates hawapigi kura. Sasa kwa hiyo hesabu tu, CCM hata kabla ya uchaguzi wana kura karibu 60%, wakichukua wale 50% ya literates wanaopiga kura.

Kama vyama vya upinzani wana nia ya kuwaondoa CCM, wabadilishe meseji yao kwa wananchi - waanze kutoa ahadi za mambo watakawafanyia watu wakiiondoa CCM madarakani. Wasidanganywe kwamba wanapaswa kuuza sera. Kuwaambia wananchi tuaanzisha serikali za majimbo wakati hawajui maana ya jimbo haisaidii.

Waambie watu tutawazesha kupata mikopo, hadi mama Ntilie watapika kwa gesi,. Bei ya sukari itakuwa Shs 1500. Umeme utashuka bei na kila mtu atapata umeme. Tutaweka bei maalumu ya umeme kwa watu wasio na kipato, ikibidi wataumia bure kwa ajili ya taa na TV (cross subsidization). Daladala hamtapigwa faini tena za uonevu na trafiki. Haturaruhusu tochi za trafiki barabarani. Tutahakikisha barabara hazina shimo hata moja. Tutamwaga mabasi ya mwendokasi hadi yawe yanatembea bila watu, na tutaleta mwendokasi mikoani, nk, hii ndio lugha wapiga kura wa Tanzania wanaelewa, sio kutanganza Nyerere alikosea muungano sijui, mawaziri ni mafisadi nk. Wanachi hawaelewi hiyo lugha.
 
Mwisho niseme wazi, Bunge na serikali wanapaswa kutambua kwamba haya mambo yana mwisho wake, na mwisho wanaotulazimisha wazalendo halisi wa nchi hii tuutafute, hautakuwa mzuri kwao. Hilo ni dhahiri kabisa.
Acheni mikwara nyie waswahili....hamna cha kufanya.
 
Tumeona walichofanya wabunge tunajiandaa kuchukua hatua kama kwa wenzetu Kenya
 
Bunge limejaa waovu. Hata siku moja hawawezi kupambana na uovu.
 
Exactly, wezi wanalindana na wakati mwingine wanatumia fedha kulindana.
 
Yaan hata CAG asingekuwa mteuliwa wa serikali angetimuliwa na Tulia.Na angeambiwa mawazir wanafanya,kazi nzuri ww unasema wanaiba. Chezea, shibe wewe. Shibe mwanamalevya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…