Adhabu ya kifo kwa kuchinjwa mbele ya kadamnasi (Tahadhari: maelezo, picha na video za ukatili)

Status
Not open for further replies.
Maswali yako mepesi sana,hilo la kwanza.Pili jaribu kutumia vyema tamko "dhana",sababu tamko dhana hutumika kuwasilisha au kutilia mkaso kitu ambacho huna uhakika nacho.Humu katika andiko naona umelitumia sana,mpaka mara ya kwanza nikapata ukakasi kukujibu.

Turudi katika nukta za muhimu kwazo maswali yako yamemili.Suala la kuomba msamaha katika dini ya kiislamu nimelitiliwa mkazo sana na mtume wetu amani ya Allah iwe juu yake,ametufundisha kuomba msamaha mara nyingi iwezekanavyo tena ametufundisha tuombe msamaha kwa makosa tunayojua tumefanya na yale ambayo hatujui kama tumeyafanya.

Makosa katika kuomba msamaha yapo katika namna mbili ila yote yanarudi katika msamaha mwisho.Kuna kosa lile ambalo umemkosea Mola wako moja kwa moja,mathalani kusengenya,kuzini,kusema uongo na mengine mengi na kuna makosa ambayo Allaha aliye juu hakusamehi mpaka kwanza umuombe msamaha yule uliyemkosea.Mathalani wewe umenikosea labda kwa kunitukana au kusema kwa dhuluma,wewe unapaswa kwanza uniombe mimi msamaha kisha umuombe Mola msamaha,hapo ndipo utasamehewa.

Dini ya waislamu sio dini ya waliokingwa na makosa na umekosea kusema kusema "watakatifu" kwa sababu hata nao wanakosea.

Katika hukumu hizo kama ya kuchinjwa,hukumu hii ipo kwa ajili ya kulinda maslahi ya umma na kuimakinisha jamii.Hata kama mtu huyo akiomba msamaha kwa Mola wake kwa kufata masharti ya toba anasamehewa lakini hukumu lazima itendeke yaani ifanyike,sababu watu waishio humo wanajua kabisa ya kuwa jambo fulani ukifanya unahukuwa kwa namna hii.kwa hiyo ikithibitika umefanya kweli unahukumiwa unavyostahiki na kabla ya hukumu unatakiwa umuombe toba Mola wako ili ukikutana nae uwe salama.Mola anajua zaidi.

Suala la hukumu kufanyika hadharani hiyo ndio stahiki yake na kuna hekima kubwa ndani yake,hukumu ile inafanyika kwa ajili ya kuwakumbusha na wengine ya kujua jambo mfano wake ni haramu na adhabu yake ni kuchinjwa na wala haifanyiki hivyo kwa lengo la kutishwa mtu.Leo hii ukiona tukio kama lile lazima mtu mwenye akili timamu utamakinika na kujilinda na hatimae kuiacha jamii ikiwa katika mstari,ustaarabu na heshima iliyopea kabisa.
 
Uislam unasema shoga, mwizi, kafiri etc wachinjwe hadharan
Saudia wanatimiza hilo

Utasemaje hamna uislam saudia?
Huon kama wanatimiza sharia za Allah?

Au wee unasemaje kuhusu hizo sharia, wamezitunga wenyewe?
Mimi siijui dini kihivyo labda ungeleta hayo maandiko kwanza.
 
Unanijua

Nimekuelewa ndugu.
Niliposema dhana, kweli sikuwa na uhakika ndo maana nimeuliza na umenifafanulia vizuri.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Basi bwana kumbe wee ni muislam jina kama ulijui hata hilo
Jifunze zaid dini yako uielewe vzr
Mi nikajua utaleta hayo maandiko kumbe mipasho katika Qur-an kila aya ilishuka kwa wakati na maana yake hatuwezi kuwa waislam wazuri eti kisa tunahukumiana kiislam ilhali Duniani tuna changamoto nyingi kama waislam kuna dhulma,vita na ukandamizaji mkubwa sana wa Uislam hao wanaohukumiana kwa Sharia hayo yote hawayaoni na wanawakumbatia haohao Wamagharibi wakandamizaji wa dini. Kabla ya kufanya haya kama waislam tuna mengi ya kufanya kuliko kuchinjana huko saudi ni nchi ya kifalme tu wengi wao wanauliwa kwa sababu za kisiasa.

Tuache kufanya kila wafanyalo waarabu ni katika dini kama kuchinja hata Isil wanachinja kwa mgongo wa dini vipi nao unawaunga mkono? Waarabu ni waislamu lakini kila siku wanapingana sasa tumshikilie nani na tumuache nani.
 
Mkuu The bold... Nataka kujua kwa undani aina ya Ulinzi anaopewa Muhammad al-Beshi na Familia yake kwa ujumla..Ninaamini sio kila familia ama mwana ndugu ataridhishwa na hukumu hizi.. Yes,adui namba moja labda anaweza kuwa ni Serikali lakini mtu wa haraka wa kuweza kuiambia serikali hatujapendezwa ni kuidhuru familia ya huyu bwana! Vipi maisha ya watoto wawapo shuleni ama hata vyuoni?! Je, ni kila mtoto hupendezwa na kazi ya Baba? Wale wasiopendezwa wanafanyaje kuibeba hii hali?! Ufafanuzi hapo kidogo...
 
Mkuu ni ajabu sana hii hali. Ila tu napenda niulize hii ni sheria ya kiislamu au ya serikali na kama ni uislamu basi mimi nitakuwa wa kwanza kuhamia dhehebu jingine maana inatisha mkuu.
 
Mauaji mubashara, na watu wanashabikia kishenzy:
 
Asante @Thebold nimesoma mpaka nikajikuta machozi yananitoka.kuna nchi hazifa kuishi kabisa asee.
Na kuna watu wana roho za ajabu,Kama huyo mchinjaji.
Yaani baada ya kusoma hii nimezidi kuchukia nchi za kiarabu
 
The Bold...big up sana kwa makala zako....kazi nzuri kuelimisha jamii.

Nimeipenda sana ile thread yako ya "Behind the Scene September 11"

Naomba uni-tag ktk makala zako.
 
Yaani mtu ana ujasiri wa kuchinja binadamu mwenzake na bado anajiona si katili!!! Dini hizi jamani!!!
Kwani dada polisi akiua jambazi utamwita katili? suala la nani tumwite katili na yupi tusimwite katili ni mitazamo yetu tu.
 
The Bold...big up sana kwa makala zako....kazi nzuri kuelimisha jamii.

Nimeipenda sana ile thread yako ya "Behind the Scene September 11"

Naomba uni-tag ktk makala zako.
Shukrani mkuu... Tayari nimekuongeza kwenye taglist
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…