Kuchinja watu
Hata kama ni adhabu, kitendo cha kuchinja watu hadhalani sio jambo jema hata kidogo.
Nchi nyingi wanapo nyonga watu hufanya kwa kificho wasiohusika wasione
Nakumbuka kitendo cha Sadam Hussein kunyongwa na kuonesha mubashara kwenye TV, kulilalamikiwa sana na mashirika ya kutetea haki za binadamu
Ivi unapochinja watu mbele ya watoto unawafundisha nini, kuwa wawe makatili, waone jambo hilo ni la kawaida tu, waweze kujaribu katika michezo yao, waweze kuwasimulia wenzao wasioona jambo hilo
Huyo mchinjaji mwenyewe ni katili.
Inaaminika nchi yetu yaani watawala wetu wanaogopa hata kuidhinisha adhabu ya kuwanyonga watu waliohukumiwa adhabu hiyo.
Inasemekana aliyenyongwa ni mmoja tu aliyemuua kwa kumpiga risasi Mkuu wa mkoa aliyejulikana kama Dr. Kreluu. Mkulima aliyeitwa Mwamwindi
Ona jinsi baadhi ya Serikali zinavyoogopa kunyonga watu.
Sasa Nchi inachinja wakosaji hadharani tena kwa uwingi (mass behadings) ni ukatili usiotakiwa kushabikiwa.
Halafu kuna tendo la mtu kuhukumiwa kifo kwa makosa,
au kwa kushindwa kujitetea au kwa kusingiziwa au kwa visa vya chuki binafsi
Kama atakaa muda fulani anapata fulsa ya kukata rufaa na kuweza kushinda rufaa yake hivyo kukwepa kifo
Kama mtu anahukumiwa, halafu adhabu ya kumyonga kufanyika harakaharaka basi wako watuhumiwa wengi walio chinjwa kimakosa, hivyo kuuawa kwa kuonewa, au jambo hilo linafanyika kwa hila.
Nadhani mashirika ya kutetea haki za binadamu ambayo yanapinga adhabu hiyo yamekata tamaa kukemea jambo hilo kwani yanapuuzwa na mamlaka ya nchi hiyo
Poleni wananchi wa Saudi Arabia,
mimi siendi Saudi Arabia naogopa naweza nikasingiziwa kosa au nikafananishwa na mkosaji nikawa BEHADED
Chao.