Adhabu ya kunyonga hadi kufa imepitwa na wakati?

Adhabu ya kunyonga hadi kufa imepitwa na wakati?

Nadhani tunakosea tunaposema "rest in peace". Hakuna kitu kiumbe chochote kinaogopa zaidi ya kifo, na katika nchi nyingine zinazotoa adhabu ya kifo, mtuhumiwa atafanya kila juhudi apate adhabu mbadala hata kama ni kifungo cha maisha na kazi ngumu. Nadhani mantiki ya adhabu ya kifo ni jamii kutoa tamko kuwa
  1. tabia kama hii hatuikubali kati ya wanajamii
  2. mtu atakayefanya hivi tutamfanyia hivi
  3. hili ulilolifanya limezidi mipaka
Pia notion kuwa ukristo unapinga adhabu ya kifo nadhani sio sahihi, maana inasema "hachukui upanga bure...." ikimaanisha serikali na kazi ya upanga tunaijua
 
Sidhani Kama haki ya mtu kuishi inakoma pale mtu huyo anapomuua Mwanzake ila inapotokea mtu katenda kosa hilo apewe adhabu itakayomfanya ajutie makosa yake na kama mtu ni hatari basi anazuiliwa mpaka hapo itakapothibitika sio hatari tena.
 
yap ni sawa kuwa na hukumu ya kifo....
(kwa watu kama mafataki na wabakaji)

(ingawa kwa upande wa Dini especially Christianity hairuhusiwi
kumuhukumu mtu)

Mie nadhani lengo la adhabu yoyote ni kumbadilisha mtu ili baadae iwe fundisho kwake na jamii nzima. Na jamii nzima ni pale anapomaliza kifungo na kusimulia kile kilochompata na wakati mwingine kuwasii watu wasifanye makosa. Lakini mtu ukimnyonga hakuna mtu aliedhibitisha ugumu wa adhabu ile kwa kuwa aliekufa hakupata nafasi ya kurudi kuonyesha ugumu wa adhabu hiyo
 
Mimi nakubaliana nayo anayeuwa makusudi sio kwa kujitetea basi na yeye auliwe na hii ni haki yawaliofiliwa ikiwa waliofiliwa hawatotaka damu ni kumsamehe basi hapo serikali inachukuwa hukumu yake ya kifungo n.k
 
kwa kweli inawezekana kutokana kutofanyiwa kazi kwa mda mrefu katika nchi yetu, lakini hata hivyo inatakiwa kuondolewa kwani kutoa uhai wa ni kosa kubwa kuliko.
 
Mi nadhani substentive part ya sheria pamoja nahukumu ya kifo inalenga kumfanya mkosaji kwanza kujaribu kurejesha hali ya umauti au magnitude ya maumivu au hali ya kukosa uhai ya aliyemuua. lakini pili inalenga kuweka mazingira ya public kuona ilivyo mbaya na yenye maumivu iwapo mtu atafanya kosa linalo amount death penalty.

kwa bahati mbaya kwa maoni yangu kibinadamu haiwezekani kutimiza dhima hiyo ya sheria hasa kwa kua hakuna kipimo cha magnitude ya kifo pia ni dhahiri kuua peke yake hakutoshi kuweka mazingira ogopeshi (kuogopesha) ili kuzuia wayu wasitende makosa hayo, Kwa maoni yangu adhabu ya kifo bado haileti tija inayotarajiwa badala yake inamweka mtekelezaji kwenye mazingira ya yeye pia kukosea, mi nadhani tunatakiwa kubuni mazingira yanayoweza kuleta effect inayoweza kuwafanya watu waache kuleta madhara ya kuuana. ili kuprove kuwa hukumu za kuua hazina jipya angalia nchi zinazotekeleza sheria za kuua je zimetulia

? ona nchi za kiarabu je sheria hiyo ina tija ? we better think otherwise.
 
Mimi naona bado ina nafasi kubwa na tunaihitaji na lengo kubwa la adhabu hii ni kuwatisha walio baki na hata ukisema wafanye kazi za kuzalisha haitasaidia sana kwani lengo la adhabu ni kuogopesha,kufanya mtenda kosa ajutie yale aliyofanya,asikie maumivu sawa na kosa alilofanya na pia kutoa adhabu itakayo waridhisha walio athirika na sababu nyingine nyingi ila tu wasiwasi wangu ni vyombo vinavyo shughulikia kesi hizi zinapata ushahidi wa kutosha?

kwani wapo waliopewa adhabu hii wakiwa c wahusika hasa kikubwa hapa ni haki na hii ni moja ya haki kuonekana
 
Even my self i think the aim of punshment is to make the offender to feel huge pains and if we kill a person without undergoing any kind of pains then that is not the aim of punshment let him or her to survive forever in prison so that to regret what he she has done
 
Jamani kuuwa si azabu bali ni kumtokomeza mtuumiwa. piya haifayi kuukum kifo inamaana sisi tuna hasira kuliko Mungu aliye muumba? angawa inauma sana kwa uwalifu na unyama wanao tenda
 
"Why do we Kill People who Kill People to Show that Killing People is Wrong ?"​

Je ni sawa kuwa na Hukumu ya Kifo?
Baada ya yule Chizi wa Norway kuua kadamnasi ya watu (ukizingatia Norway life Sentence ni limited kwa miaka 21 tu) Je ni muhimu kuwa na hukumu ya kifo? Ni nini hasa faida ya hukumu ya kifo?

Je hukumu ya kifo inafanya watu waogope kutenda maovu kwahiyo ni njia nzuri au ni kuonyesha hata sisi hatuna tofauti na waliofanya hayo maovu?

I can argue kwamba huenda hukumu ya kifo ni adhabu rahisi sababu badala ya kumfanya mtu ku-suffer kwa kosa lake, tunampumzisha...Je sio vema kumfunga mtu maisha na kumfanyisha kazi ngumu kwa maisha yake yaliyobaki na kila alichonacho au atakachokitengeneza kiende kwa wale aliowatenda....

What do you think?.....

Kwanza tujue kwamba mtu kuhukumiwa kifo ni mpaka awe kaua kwa kukusudia.

Then kuna wale watu roho zao sijui ni pepo au ni kitu gani, mtu kaua zaidi ya mara moja.

Then kuna mtu inawezekana kuua kwake siyo ishu kubwa, hata ukimpeleka gerezani akizinguliwa anaweza kuua pia.

Then kuna wahalifu siku hizi kuiba mtutu unatangulizwa kwanza mbele. Hawa kuua kwao ndo kabisa ni ishu za daily endapo watakutana na kizuizi.

I am not supporting watu kunyongwa ila duh! Kuna watu wengine hawafai
 
Kilakitu kinaendana na sheria inavyosema. Japo ibara ya 14 ya katiba ya 1977 marekebisho ya 2008 kinampa mtu haki ys kuishi lakini Ibara ya 15(1)b ya URTC kinasema kamamtu atafanya kosa linalopelekea oda ya mtuhuyo kutolewa na maakama kua anyongwe bac haki ya mtuhuyo kuish itaondoka.Hivyo kifungu cha pinocode no 196 na197 vitachukua nafasiyake.

Hii ni international ndiomana hata ikampelekea Sadam Hussein kunyongwa kwa sheria zakimataifa
 
jaman sheria ya kifo Tz ni bora isiwepo just imagine kama ndio wew umesomewa leo hukumu ya kifo alafu unaenda kuwekwa in custody ukisubiri unyongwe yan na kila cku hunyongwi ila uko pale ukijua kua unatakiwa unyongwe afu unakuja kunyongwa after 20years iv uyo mtu kipindi chote icho anachosubiri c anaweza akajiua coz wasiwas unamtawala mda wote akiona tu mlango unafunguliwa anajua ndio siku yake maskin kumbe kaletewa chakula!

Kitu kingne iyo adhabu inakua ngumu kutekelezeka coz hakuna mtu ambae anawez kubali mkono wake ubebe damu y watu ndio maana kila raisi anapita bila kuweka sahih yake kuhusu kunyonga sasa je wale wanaongoja kunyongwa je?
 
Hilo swala la hukumu ya kifo linatakiwa liangaliwe tena upya hapa Tanzania. Makosa yanayobeba hukumu hii yanatakiwa yachambuliwe kwa undani, kwa mfano mauaji ya kawaida yanatakiwa yabebe kifungo cha maisha (yaani muda usiozidi miaka 33 jela). Pale ambapo ni mauaji ya kinyama au ya zaidi ya mtu mmoja hapo inawezekana kufukiria hukumu ya kifo.

Tatizo la Tanzania ni kuwa wale waliohukumiwa kifo wanakuwa katika mazingira magumu gerezani, taa zinawashwa masaa 24 eti wasije wakajinyonga. Mimi ningependekeza wale wote wenye hukumu ya kifungo cha maisha na wale wenye hukumu ya kunyongwa wawe na vitanzi kwenye cell zao ili waweze kujinyonga kwa muda na staili yanayotaka. Hii itawapunguzia mateso na serekali pia itapunguza gharama.

Tanzania haijanyonga mtu tangu 1995 (kwa taarifa nilizonazo, labda si sahihi), Mkapa na Kikwete hawapitishi Death Warrant, kuna zaidi ya watu 280 wanasubiria kitanzi shingoni. Mtu anaponyongwa kitaalamu huwa anakufa chini ya dakika 6, na huwa hapati maumivu makali kwasababu anakuwa amepoteza fahamu. Lakini vile vile, kama mtu akinyongwa pole pole (kama wanavyofanya Iran), zoezi zima linaweza kudumu dakika 10 - 20 (Ken Sarowiwa wa Nigeria alichukua dakika 20 kukata roho).

Short Drop Hanging inamsababishia myongwaji kujitupatupa, kujisaidia, kutoa ulimi nje, kukodoa macho, kutoka mbegu za kiume nk. Haya huwa ni mateso. Kwa matiki hiyo tungeweka "moratorium" kwenye hukumu ya kifo ili kuwe na mjadala wa kitaifa kuhusu jambo hili, ikilazimika tupige kura za maoni (Referrendum).
 
Kwa maoni yangu ingawa nalaani tabia ya watu kuua wengine, ila napingana na hukumu ya kifo kwa mtu aliyeua kwani matokeo yake ni vifo viwili (kwa kumuua muuaji). Ni mategemeo yangu kuwa watunga sheria watabadilisha hiyo hukumu iwe LIFE SENTENCE.
 
  • .... Adhabu ya kummyonga mtu hadi kufa ikiwa ni hukumu kwa mkosaji ambaye imedhihirika wazi kwamba aliua sio kwa bagati mbaya .. bali alikusudui na inadhihirika hivyo kwa ushahidi wa dhati kabisa pasipo mashaka...mifano miwili au zaidi kama ifuatavyo.....


  • Kwamba alichukua silaha na amekutwa nayo.. kisha akavamia duka la muuza vocha .. akampiga risasi na kumuua pale pale....watu wakawazingira majambazi yale na kuwatia mbaroni........ na ushahidi wa silaha iliyotumika, na kumekutwa na kitambulisho/leseni ya mmoja wa majambazi wale katika eneo la tukio...



  • Kwamba Mtu amevamia nyumbani kwa mlemavu wa ngozi, usiku wa manane......akaingia ndani ya nyumba na kumkata mapanga mlemavu wa ngozi na kuondoka na sehemu ya kiungo cha mlemavu huyo . na watu wakawavizia majambazi hayo na kukimbizana nao maporini baada ya kuwakamata mmoja wao anakutwa na kiungo cha Mlemavu yule wa ngozi.. huku shati limejaa damu..


  • Mume anamtesa mkewe...na anaamua kumuua mkewe na watoto.. na yeye mwenyewe anajaribu kujiua lakini inashindikana... watu wanamuwahi...


  • Jamaa yuko safarini na familia yake mke na watoto jamaa wenye silaha wanawavamia wanaweka magogo barabarabi kufanya ujambazi na kumuua baba mbele ya familia yake... bahati mbaya gari la hao majambazi linapinduka hatua chache ... majambazi wanakamatwa.....

Mahakamani Judge anakubaliana na ushahidi na mwenendo mzima wa kesi .. kwamba mauaji yalifanyika katika ukatili mkubwa Judge anaamua mtuhumiwa/watuhumiwa kunyongwa hadi kufa...... BINASI NINAUNGA MKONO ADHABU YA KUNYONGWA MPAKA KUFA

Kwa hali yoyote ile.. iwapo Rais anaona huruma kutia sahihi watu wanyongwe, au ni katika kuhimiza kile kinachoitwa haki za binadamu za kuishi... lakini kwa watenda makosa ya dhahiri kama mifano hiyo hapo juu wanastahili kunyongwa...


  • Aidha Katika swala la kutenda kosa.. hapo inabakia kwamba umetenda kosa... hakuna la kujitetea..nini maana ya dhana ya sheria kuchukua mkondo wake...
  • Utawala unaoshindwa kunyonga wakosaji ni utawala dhaifu... kule China na nchi nyingine wananyongwa na watu wanaogopa kuendelea kutenda makosa.. na uhalifu unapungua... swala la kutokutekeleza haki kwa wakosaji kunazidisha uhalifu ........ na hata wanaotenda makosa mengine wanakuwa hawana hofu na hukumu mbalimbali zinazotolewa dhidi yao.
 
kwa maoni yangu hukumu ya kifo iendelee kuwepo hususani Tanzania. Iwepo hasa katika makosa ya kuhujumu uchumi ili tupunguze mafisadi wanaowauwa watanzania wengi kwa kushindwa kupata huduma muhimu kutokana na uwizi wao.
 
naunga mkono adhabu ya kunyogwa mpaka kufa tena ilibidi kuambatanisha adhabu mbili mateso makali kisha kunyongwa hadi kufa japo watu wa haki za binadamu wanapingana na hili nao wanatakiwa kuja na solution nzuri ambayo itazuia au kupunguza makosa ya mauji lakini hili la kifungo cha maisha sikubaliani nalo kwasababu mtu anaendelea kuishi japo anakuwa anakuwa in custody
 
Back
Top Bottom