Adhabu ya kunyonga hadi kufa imepitwa na wakati?

Adhabu ya kunyonga hadi kufa imepitwa na wakati?

This has always been a difficult topic in the legal world. Mimi nassuport death sentence kwa sababu hizi:-

1. Inategemea unserve life imprisonment sentence wapi, kwa mfano nchi za uarabuni maisha ya jela ni ya raha kuliko maisha ya mtanzania aliye huru. Ndani kuna TV, kuna saloons, a lot of physical activities and games, internet access, libraries etc...oh na hamna hard labor. So ni kula kulala, watanzania wangapi watapigania kwenda dubai au Qatar kusave life sentence?

2. Nadhani sababu muhimu nyuma ya death penalty siyo kuwaogopesha watu kutokutenda makosa hayo (ingelikuwa hivyo watu wasingetenda haya kwa kuogopa moto wa kiama) bali ni kuipa amani familia iliyoathirika na vitendo hivyo such as the family of the deceased, inawapa hali ya kuona justice has been served.

3. Kama ni issue ya human rights, kwamba kunyonga, lethal injection, electrical chair etc ni inhuman na zinasababisha maumivu makali basi solution ipo ndugu zetu waislam wanayo...kifo kwa kukatwa kichwa na mapanga PROBLEM SOLVED
 
Kwa kweli hukumu ya kifo ndio hukumu hasa inayofaa kwa kosa la kuua, ukizingatia kua Duniani kote viongozi wa Serikali na wale wa taasisi binafsi, na wale wadini wanapambana kila leo kudumisha na kusisitiza haki za binamu.

Ikiwa haki ya msingi ni ile ya Mtu kuheshimiwa uhai wake, hii inamaana kwamba ni mwiko kwa yeyote yule kuthubutu kuhatarisha uhai wa mwenziwe kwakua anahaki sawa na yeye.

Ikitokea mmoja amemuua mwenziwe, maanayake ameiingilia haki yake ya msingi yakuishi kwa kumuondoa Duniani bilasababu ya msingi.

Kwakua tu ameweza kuthubutu kwa makusudi kuharamisha haki ya mwenziwe kuishi nae nihalali kwake KUADHIBIWA ADHABU YA KIFO.

Kwa hapa Tanzania ningekuomba urejee katika KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA 1977, Ibara ya 14 ina guarantee haki ya kuishi, na mwisho ibara ya 30 ambayo inaonyesha mipaka dhidi ya mtu kutumia hakizake za msing
 
namalizia kwa kusema kua ibara ya 30 ya katiba ya Jamhuri ya Tanzania inaweka mipaka katika kutekeleza haki ya kuishi, soma vizuri ibara 30.-(2) (a) hadi (f)

Hivyo basi hukumu ya kunyongwa haija pitwa na wakati kwakua kufanya hivyo ni kuonya na kulinda haki ya mtu mwengine isipotee burebure
 
hii hukumu hata mimi nafikiri ni rahisi sana,ukizingatia mtu ana rest in peace bila taabu

Tena unampa na muda wa kutubu anaenda zake Eden one way, noooo, sio fair. Mtu muuaji anatakiwa akabiliwe na libeneke la life yake yote mpaka aombe poo. Kumuua ni kumsifia tu kwa kuwa wote tutakufa. Kama kufa ni adhabu ambao hawajaua wanakuwa wamekosa nini
 
Prince Ismail

Hakuna aliyekataa kwamba ipo kwenye katiba yetu mkuu punguza maneno marefu, tunazungumzia impact yake katika kuwafanya watu wasifanye makosa. Adhabu kazi yake ni kuonya, lkn kama muonywaji hapati cha kujifunza na muda wa kujutia makosa, funzo gani lipo? Ukumbuke kuna watu hawaogopi kufa.

Mtu akiua halafu adhabu yake ikawa kazi ngumu tena zinazoonekana wazi na jamii, nadhani wengine wasingethubutu kuua. Lakini hii iliopo ni sawa na kusema mtu akiiba na yeye aibiwe. Au mtu akibaka na yeye abakwe
 
Last edited by a moderator:
hii hukumu hata mimi nafikiri ni rahisi sana,ukizingatia mtu ana rest in peace bila taabu
inatisha sana kwa mtuhumiwa. Huwezi kujenga uchumi kama huna adhabu ya kifo hapa africa. Huwezi kuwapa maisha bora wananchi wako kama huna adhabu ya kifo hapa Tanzania. Pesa zilizofichwa Uswiss zilikuwa zinaweza kucreate 100,000.00 jobs na kubadili hali ya maisha ya watu katika mikoa yote ya kusini na Rukwa. Lakini kwa sababu hakuna adhabu ya kifo, hela hizo kachukua mtu tatu tuu na kujinufaisha yeyey na familia yao. Sasa what sayest art thee?
 
kama u7nataka kujenga nguvu za chama bora kupita uchumi, wewe pinga adhabu ya kifo. lakini kama unataka kujenga uchumi imara na kuwapa watu faida ya matunda ya uhuru, adhabu ya kifo ni nzuri sana kupita hata zipu kwa suruali ya bwana harusi.
 
namalizia kwa kusema kua ibara ya 30 ya katiba ya Jamhuri ya Tanzania inaweka mipaka katika kutekeleza haki ya kuishi, soma vizuri ibara 30.-(2) (a) hadi (f)

Hivyo basi hukumu ya kunyongwa haija pitwa na wakati kwakua kufanya hivyo ni kuonya na kulinda haki ya mtu mwengine isipotee burebure.

Majaji, Mahakimu,Mawakili na Wanasheria wenzangu tutekeleze hukumu hii kwa kua ndio suluhisho pekee
 
Kwa upande wangu kwa kweli sikubaliani na hukumu ya kifo na sidhani kama inaleta nidhamu kwenye jamii, kwamba wengine wataogopa kufanya mauaji! Mabadiliko ya mtu hayatokani na hofu, bali inahitajika badiliko la ndani kujua kuwa kuua ni vibaya, na sipaswi kufanywa hivyo!

Naomba uwe makini kwa mifano nitakayotoa hapa chini, adhabu ya kifo ilikuwa inatolewa kimila miaka mimgi sana nyuma baada ya hapo vikaja vitabu vya dini ya kikristo na kiislamu vyote viliruhusu adhabu ya kifo kwa atakayemwaga damu ya mwenzake BILA HATIA

'KITABU CHA TORATI" Ambacho pia ni hichohicho kimetumika pia kwa waislamu kuwaagiza atakaye muuwa mtu bila hatia naye auawe hivyo ndivyo utakavyoondoa ubaya kwa watu wangu Israel, kwa asili binadamu ni mjeuri na ni mhalifu hivyo haiwezekani maisha ya binadamu akaishi kwa amani na mwenzake bila kuwa na utisho wa mambo anayoyafanya kama yakileta madhara upande wa pili, kwa mfano familia ya baba mkali huwa inaheshimika kuliko familia ya baba dhaifu anayekubali kila kitu kwa sababu kuanznia majirani mpaka watoto hujua kuwa kuchezea familia ya mtu mkali ni kubeep matatizo wakati familia ya mtu dhaifu huonewa kila wakati haya yote hutokea kwa hofu kwamba huyu mkali reaction yake itakuwa mbaya kama akiguswa kwa hiyo nataishi kwa kuogopwa kutokana na ukali wake na huyu anayesema kila kitu Mungu atalipa huishi kwa shida muda wake wote awapo duniani.

Mwanafunzi mvivu hayuko tayari kusoma kama hakuna utisho wa viboko lakini kwa viboko mwanafunzi hyuyhuyu anafaulu vizuri sana. Mimi nasema adhabu ya kifo ni sashihi kwa muuaji kwani hakuna mbadala wa uhai na atakaponyongwa hapa hata wengine wenye mawazo ya kuuwa wenzao wataghairi nia zao badala ya kumfunga maisha ataongeza ghrama kwa serikali na akiugua atatibiwa kwa gharama pia kwa hiyo ataendelea ku-enjoy wakati alishamtoa roho mwenzake na pia ataiona familia yake wakati aliyemtoa roho hawezi kufanya hayo, na pia atakuwa na uwezo wa kuiongoza na kuipa maelekezo familia yake wakati marehemu hawezi fanya hivyo kifupi ni kwamba "uhai kwa uhai jino kwa jino" hiyo ni Biblia siyo mimi.

Marekani kwenyewe ambako wasadikika wengi wanasadiki kuwa ndiko chimbuko la Binadamu adhabu hii bado inatumika jiulize ni kwa nini? Tena mimi naona ingelikuwa tamu zaidi watu hawa wakanyongwa hadharani ili watu wajue kifo si mchezo kwa mfano wanaouwa albino hawastahili kuishi hata kidogo. wabakaji na wengineo ndiyo wafungwe maisha kwa kuwa hawajatoa roho ya mtu.
 
Kwa upande wangu kwa kweli sikubaliani na hukumu ya kifo na sidhani kama inaleta nidhamu kwenye jamii, kwamba wengine wataogopa kufanya mauaji! Mabadiliko ya mtu hayatokani na hofu, bali inahitajika badiliko la ndani kujua kuwa kuua ni vibaya, na sipaswi kufanywa hivyo!

Kuna adhabu inayoleta nidhamu kwenye jamii?
 
Hakuna aliyekataa kwamba ipo kwenye katiba yetu mkuu punguza maneno marefu, tunazungumzia impact yake katika kuwafanya watu wasifanye makosa. Adhabu kazi yake ni kuonya, lkn kama muonywaji hapati cha kujifunza na muda wa kujutia makosa, funzo gani lipo? Ukumbuke kuna watu hawaogopi kufa.

Kazi ya adhabu ni kuonya? Hiyo dhana umeitoa wapi wewe? Kazi ya adhabu ni pamoja na kutenda haki pia. Mimi ukiniulia mpendwa wangu haki pekee ambayo nitaona mpendwa wangu pamoja na mimi tunatendewa ni wewe kuuliwa.

Siwezi kuendelea kuishi kwa amani huku nikijua wewe upo gerezani unavuta oksijeni ya bure. Ni ufe tu. Ila usife haraka baada ya kuhukumiwa. Nitapendelea ukae miaka kadhaa ukisubiri siku yako ya kunyongwa, kudungwa sindano, au kukaangwa katika kiti cha umeme.

Mtu akiua halafu adhabu yake ikawa kazi ngumu tena zinazoonekana wazi na jamii, nadhani wengine wasingethubutu kuua. Lakini hii iliopo ni sawa na kusema mtu akiiba na yeye aibiwe. Au mtu akibaka na yeye abakwe

Mimi nadhani adhabu ya kifo iendelee kuwepo ila kabla ya waendesha mashitaka hawajaamua kwamba wata seek hiyo adhabu, ni vyema wakashauriana na ndugu wa marehemu kuona kwamba kama wanaridhia. Kama wanaridhia basi na wai-seek hiyo adhabu. Kama hawairidhii basi na wa-seek kifungo cha maisha na kazi ngumu.

Binafsi naiunga mkono adhabu ya kifo na ningependa hiyo option iwepo kama ikitokea mpendwa wangu atauwawa kikatili na katu sitafikiria mara mbili. Nitaichagua in a heartbeat.
 
Japo katiba ya Jamhuri ya muungano inakinzana na sheria namba 16 ya makosa ya jinai juu ya adhabu ya kifo...kwangu mimi Adhabu ya kifo iwepo palepale kutokana na makosa ya jinai yanayostahili adhabu hiyo ikiwemo mauaji ya vikongwe,Mauaji ya albino,armed robery... Pia yapo makosa kama uhaini.. haya yote yastahili adhabu ya kifo..Pia ningependelea na kosa la rushwa/ufisadi liongezwe ktk makosa hayo ili kuwepo na uwajibikaji...
 
kifo sio adhabu kwasababu anaekufa hajifunzi chochote na pia wakosefu watarajiwa wala hawana habari ya hukumu wala utekelezwaji wake. Hivyo hukumu ya kifo haimrekebishi mhukumiwa, haizuii wengine kutenda kosa husika na wale haitoi fidia kwa aliyekosewa. Hizo ndizo sifa tatu za adhabu ya kiungwana. Kwa kuwa adhabu ya kifo haitoshelezi yoyote kati ya sifa hizo basi haifai. lengo la adhabu ya kifo ni kulipa kisasi.

Wastaarabu hawalipi kisasi. yafaa nini kumwua aliyemwua babangu na kuongeza yatima duniani? Tena ikiwa utamwua mke wangu kwa vile alimwua kimada wangu mimi Napata faraja gani? Hebu acheni ushabiki mtafakari na kasha muamue kuikataa sharia isiyo na manufaa kwa walio hai. Hii sharia ya kulipia wafu kisasi tuikatae maana haiwafai wafu na haisaidii walio hai. HAIFAI, HAIFAI KABISA!!!!!!!!!!
 
Mi naona kupoteza maisha ya mtu sio vizuri ,bali wawe wanapewa adhabu ya kufanya kazi bila malipo.kama injinia anapewa kufanya kazi ya uinjinia kama adhabu,labda.ila mtu kumkatisha mwenzake maisha naona inaumiza kwa ndugu wa mtendwa,wengi hatujui makali wanayowapata watendwa ndo maana tunatetea wauwaji kutonyongwa.da mtu anakata binadam mwenzake kama mnyama huko tarime.da
 
kifo sio adhabu kwasababu anaekufa hajifunzi chochote na pia wakosefu watarajiwa wala hawana habari ya hukumu wala utekelezwaji wake. Hivyo hukumu ya kifo haimrekebishi mhukumiwa, haizuii wengine kutenda kosa husika na wale haitoi fidia kwa aliyekosewa. Hizo ndizo sifa tatu za adhabu ya kiungwana. Kwa kuwa adhabu ya kifo haitoshelezi yoyote kati ya sifa hizo basi haifai. lengo la adhabu ya kifo ni kulipa kisasi. Wastaarabu hawalipi kisasi. yafaa nini kumwua aliyemwua babangu na kuongeza yatima duniani? Tena ikiwa utamwua mke wangu kwa vile alimwua kimada wangu mimi Napata faraja gani? Hebu acheni ushabiki mtafakari na kasha muamue kuikataa sharia isiyo na manufaa kwa walio hai. Hii sharia ya kulipia wafu kisasi tuikatae maana haiwafai wafu na haisaidii walio hai. HAIFAI, HAIFAI KABISA!!!!!!!!!!

kwani muuaji akifungwa inamsaidia nin mtendwa?muuaji ni kama mnyama hafai kuishi na binaadam wengine kabisa.tena wale wanaoua kwa kukusudia hawafai.
 
VoiceOfReason;

Why do we Kill People who Kill People to Show that Killing People is Wrong?

We kill people who kill people to show that killing people is wrong because killing is subject to the killer to be killed as well!!!
 
Last edited by a moderator:
"Mosi imepitwa na wakati kutokana na kukua kwa teknologia za ulinzi ujenzi na social psychology pia utamaduni ambao dunia inaanza kuubeba(haki za binadam,iman za dini na world orders). Kama ambaye ushahidi haukutosha aachiwa japo kaua iweje huyu aliekutwa na hatia awe tofauti na wengine?Sion sababu ya kuwaua ila wawe expkoited bure na taifa kutokana na vipaji vyao maovu kwahiyo ni njia nzuri au ni kuonyesha hata sisi hatuna tofauti na waliofanya hayo maovu?

I can argue kwamba huenda hukumu ya kifo ni adhabu rahisi sababu badala ya kumfanya mtu kusuffer kwa kosa lake, tunampumzisha.Je sio vema kumfunga mtu maisha na kumfanyisha kazi ngumu kwa maisha yake yaliyobaki na kila alichonacho au atakachokitengeneza kiende kwa wale aliowatenda.

What do you think?."Mosi imepitwa na wakati kutokana na teknologia tuliofikia na utamaduni ambao dunia inaanza kuubeba(haki za binadam,iman za dini na world orders). Kama ambaye ushahidi haukutosha aachiwa japo kaua iweje huyu aliekutwa na hatia awe tofauti na wengine?
 
Ckuzote aliye uwa nayd anahitajika afe ila kabla mahakama haijatoa hukumu hiyo inabidi m2 huyo apimwe akili kama zipo sawa bac lazima naye afa pia tukio lililo tokea alikusudia au kwa mimi adhabu iko sahihi kama mahakama itaitumia ipasavyo
 
Binafsi nafikiri badala ya adhabu ya kifo kuondolewa isiondolewi bali iwe inatekelezwa! Haiwezekani mtu akafanya unyama kama huu hapa chini, (Fungua link hapo chini) bado tuendelee kuishi nae! Huyu hana tofauti na simba, mamba au mnyama yoyote anayeuwa binadamu ambaye mwisho wa siku atatafutwa na askari wanyama pori na kuuwawa. Kumfunga maisha ni kuongeza mzigo tu kwa serikali wa kuhudumia wafungwa pasipo sababu za msingi, hii itakuwa ni fundisho kwa wale wengine watakaobaki.Kama ni haki za binadamu ni haki gani anahitaji mtu anayeuwa binadamu wenzie aanze yeye kuitekeleza haki kwa wenzie kabla ya wengine kumtekelezea.

Ebu tujaribu kuuva ubaba au umama wa mtoto huyu mtoto aliyeuwawa halafu tujiulize ungekuwa wewe umebahatika kuonana na huyu aliyemfanyia hivi mwanao ungefanyaje?

KINGOTANZANIA:: HABARI, PICHA NA MATANGAZO: MTOTO LISTA MWAKANYAMALE MIAKA NANE MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI SHULE YA MSINGI YA ISANGE MWAKALELI WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA AUAWA KIKATILI KWA KUKATWA KICHWA NA KUTOLEWA VIUNGO VINGINE NA MWILI WAKE K
 
Back
Top Bottom