Adhabu za Bodi Ya Ligi Tanzania(TPBL) zinaacha Maswali Mengi Sana Kwenye Tasnia Ya Mpira Wa Miguu

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
Wakuu Nimekuwa Nikiona Adhabu Nyingi Za Bodi Ya Ligi Tanzania (TPBL) Ni Kama za Kukoa Timu fulani. Hivi Ni Wakati gani ambapo Team Husika Inaitwa kujitetea Mbele ya Bodi Husika Kuhusu makosa yaliyofanywa na Team Husika?.

Nadhani Hii Adhabu Ya Bodi Ya Ligi Kwa Yanga Ni Namna Gani bado Tff wana Hasira na Mechi Ya Juzi.

Naanza Kuamini Kwamba Yanga Haikuwafunga Simba Pekee Bali Walifungwa Tff,Bodi ya Ligi, Wizara Husika.

Timu zifuate utaratibu na sheria, faini hazitakuwepo.
 
Mkuu, ni Wakati gani ambapo Team Husika Inaitwa kujitetea Mbele ya Bodi Husika Kuhusu makosa yaliyofanywa na Team Husika?.
Sasa Mkuu unajua kabisa kufanya jambo flani ni kosa uitwe kujitetea au kusikilizwa tena,angalia hayo makosa waliyoyafanya Yanga, hapo utawaita kuwasikiliza?
 
Sasa Mkuu unajua kabisa kufanya jambo flani ni kosa uitwe kujitetea au kusikilizwa tena,angalia hayo makosa waliyoyafanya Yanga,hapo utawaita kuwasikiliza?
Hata Mahakamani conviction Uwaga inatoka baada ya parties Wote Kutoa utetezi Wao Mbele ya Jaji, Hakimu na Sio Hawa Ambao Hata Mlalamikiwa Wala hapewi nafasi ya Kujitetea Wa Nini ameyafanya Haya, Hizi Ni Kanuni za Hovyo Sana
 
Tusiendekeze ujinga Mkuu,timu kubwa kabisa inavunja sheria,timu inavunja mageti na makufuri,timu inaenda kubadirisha nguo kwenye chumba cha wafanya usafi,timu inaingilia Mlango wa wandishi wa habari halafu uiite kuisikiliza?
 
Jambo la kushangaza sana kwa timu kama yanga kufanya mambo ayo

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Tusiendekeze ujinga Mkuu,timu kubwa kabisa inavunja sheria,timu inavunja mageti na makufuri,timu inaenda kubadirisha nguo kwenye chumba cha wafanya usafi,timu inaingilia Mlango wa wandishi wa habari halafu uiite kuisikiliza?
Mkuu Wala sitetei unaouita Ujinga, Ndio Maana Hata Mahakamani Mtu alieua na anashitakiwa na Jamhuri Ila Huyo Jamahuri Ndio anamwekea Wakili Wa Kumtetea.

Mkuu, Mshitakiwa anaweza kuwa ametenda kosa la jinai, na mahakama kumtia hatiani, lakini kutenda kwake kosa hilo kunaweza kuwa kumesababishwa na sababu ambazo sheria inatambua kuwa ni utetezi katika kosa hilo.

Utetezi huo ukikubaliwa mshitakiwa anaweza kufutiwa adhabu, akapunguziwa adhabu au kutopatikana na hatia.

Mpaka Yanga Anafanya aliyoyafanya alishagundua Kuna Jambo so Kabla ya Adhabu Husika walipashwa Wawaite Yanga Wawaulize Ni Kwa Nini Walipitia Kwenye Njia Ambayo Sio Rasmi.
 
Mkuu Wala sitetei unaouita Ujinga, Ndio Maana Hata Mahakamani Mtu alieua na anashitakiwa na Jamhuri Ila Huyo Jamahuri Ndio anamwekea Wakili Wa Kumtetea...
Tatizo lao wanaamini sana kwenye ushirikina ndo kinachowasumbua hao unaowatetea!
 
Tusiendekeze ujinga Mkuu,timu kubwa kabisa inavunja sheria,timu inavunja mageti na makufuri,timu inaenda kubadirisha nguo kwenye chumba cha wafanya usafi,timu inaingilia Mlango wa wandishi wa habari halafu uiite kuisikiliza?
Bodi ya ligi walipaswa kujiuliza kwanza hayo maswali kabla ya kutoa adhabu...walipaswa kujiuliza na kujua kwann timu iende kubadili nguo chumba tofauti..kutoa tu adhabu hakusaidii...vipi kama kwenye chumba rasmi cha kubadili nguo kulikua na tatizo
 
Yanga walipotenda makosa hayo walikua wanajua kwamba kanuni zilizopo haziruhusu wao kujitetea kabla ya kupewa adhabu, kinachotakiwa ni kulalamika kama wameadhibiwa kinyume na kanuni.
 
hata mimi nimeishangaa bodi ya ligi kumwacha mwamuzi aliyevurunda akiwa na amani na hongo aliyopewa.
 
Bodi ya ligi walipaswa kujiuliza kwanza hayo maswali kabla ya kutoa adhabu...walipaswa kujiuliza na kujua kwann timu iende kubadili nguo chumba tofauti..kutoa tu adhabu hakusaidii...vipi kama kwenye chumba rasmi cha kubadili nguo kulikua na tatizo

Yanga ndiyo Walipaswa kuliripoti tatizo sio wasubiri waulizwe na Bodi ya Ligi. Ni sawa na kusimamishwa Kazi kwa kutoa kuripoti kazini Wiki Moja halafu ukajitetea ulikuwa unaumwa! Kwanini hukutoa taarifa mwanzo kwa Mwajiri wako kuwa unaumwa hutoweza kufika kazini?
Tuwe na logic kwenye kujenga hoja.
 
Wewe jamaa hujui chochote kuhusu mpira na sheria zake lakini umekomaa na ubishi tu.

Hivi Bodi ya Ligi ni kama Mahakama? Unajua tofauti ya Bodi ya Ligi na Kamati ya saa 72 na ile ya Maadili?

  • Ukikatiwa Rufaa utaitwa kujitetea
  • Ukipelekwa kwenye kamati ya Maadili utaitwa kujitetea

Lakini unavunja Mageti uitwe kujitetea? Serious? Mbona washabiki wa Simba walipong'oa Viti Taifa tulilipa Faini Vizuri tu na wala hatukulalamika kuwa hatujaitwa tukajitetee?

Usikomalie kutetea ujinga ndugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…