Adinani Hussein hajapatikana licha ya Polisi kupokea Tsh 13 Million kutoka kwa ndugu

Adinani Hussein hajapatikana licha ya Polisi kupokea Tsh 13 Million kutoka kwa ndugu

Kutoka Ukurasa wa Boniface Jacob Mtandao wa X: SIKU 280 TANGU APOTEE ADINANI HUSSEIN MBEZI MIKONONI MWA POLISI

Maarufu kama (ADAM),umri wa miaka 32,mkazi wa Kinyerezi,mtaa wa Faru,Jimbo la Segerea,Baba wa watoto wanne.

1. Adinan Hussein Mbezi alipotea tarehe 12 September 2023 alipokuwa safarini Mwanza

2. Adinani Hussein Mbezi alizaliwa mwaka 1992 ni mfanyabiashara anaye miliki vituo 11 vya kuoshea magari Dar es saalam vya "ONE TOUCH" Pia ni mwanasiasa ambaye alishawahi kuwa CCM baadae akagombea udiwani kupitia ACT WAZALENDO uchaguzi wa 2020 kata ya Yombo Vituka.

3. Tarehe 12 September 2013 ADINANI alipiga simu kwa mke wake ROSEMERRY MASSAWE kumtaarifu kuwa amekamatwa na Polisi,kwamba wapo njiani kurudi Dar es saalam atamjulisha kituo watakacho mpeleka baada ya kufika Dar es saalam.

4. Tarehe 19 September 2023 ADINANI alipiga simu kwa Mama yake mlezi anayeishi maeneo ya ZOO,Chanika,Dar es saalam kwa kupitia namba ya simu 0659167082

Akimueleza Mama yake kuwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo cha Polisi cha Tazara,akaomba Mama yake amsaidie kumpatia namba ya Kaka yake aitwaye SAMIR HUSSEIN MBEZI

Pia aliomba Mama yake ampe taarifa rafiki yake aitwaye AMIR KHALID NASIBU (SAM) mwenye namba za simu 0711959432
ambaye amekuwa akishirikiana na familia katika kumfuatilia ADINANI kwa kila hatua.

5. ADINANI alijitahidi sana kufanya mawasiliano na ndugu zake kila kituo alichokuwa anapelekwa Jijini Dar es saalam tangu akamatwe Mwanza.

Alipiga simu akiwa Central Police Station,alipiga simu akiwa Kituo cha polisi Stakishari na simu ya mwisho alipiga kwa mke wake ROSEMERRY MASSAWE akiwa Tazara kupitia simu ya Polisi nambari 0659167082

Sasa akimtaarifu mke wake kuwa amepigwa sana,anahali mbaya ambayo mke wake aligundua hali ya mme wake kuwa yupo katika mateso

ADINANI aliomba mke wake atume kiasi cha Shillingi laki 5 katika namba 0659167082 ambayo alisema namba ya simu ya Polisi aliyekuwa naye wakati huo,kwa ahadi ya kiasi hicho kingesaidia asiendelee kuteswa zaidi.

Mke wake ROSEMERRY MASSAWE alitekeleza ombi la mume wake kwa kutuma laki tano.

6. Ndugu wa ADINANI walifika kituo cha Polisi Tazara,ambapo afande Kaduma mwenye namba 0757078736 alikana kumshikilia ADINANI kituo cha Tazara

Mwisho walienda Kituo cha Polisi Oysterbay ambapo walielekezwa waende Kituo cha polisi kati ofisi ya ZCO kandaa maalum DSM,kumuuliza Afande Mafwele kuhusu ndugu yao kushikiliwa na Polisi

ZCO Mafwele alikana kumshikilia ADINANI,aliwatolea orodha ya mahabusu wanaoshikiliwa kituoni pale, Jina la ndugu yao halikuwemo katika orodha ya mahabusu.

Pia aliwataarifu kuwa na wao Kanda maalum ya Dar es saalam wanamtafuta ADINANI kama mtuhumiwa,wakimpata wataitaarifu familia yake.

7. Ndugu wa ADINANI katika kumtafuta ndugu yao walifanikiwa kuonana na Kigogo mmoja wa Jeshi la Polisi,ambaye aliwathibitishia kuwa ndugu yao yupo Kituo cha Polisi Tazara,aliomba kiasi cha shillingi million 10 ilikuwasaidia kumaliza sakata la ndugu yao,

Ndugu walitoa kiasi cha shillingi million 10 kupitia dereva wake,lakini baada ya kutoa kiasi hicho,Kigogo huyo aligeuka kuwapa jibu kumbe ni majina tu ndiyo yanafanana,lakini ndugu yenu hayupo kituo cha polisi Tazara

8. Baada ya siku kadhaa kupita ndugu wa ADINANI walipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha ni Askari wa Kituo cha polisi Mburahati kupitia namba ya simu 0713440820

Askari huyo aliwaeleza Kuwa ADINANI yupo Kituo cha Polisi Mburahati na hali yake ni mbaya sana.
Askari huyo aliomba watumiwe kiasi cha Millioni 2 na laki 5 ili wasiendelee kumuadhibu na kumpa mateso ndugu yao.

Ndugu walipotuma shillingi million mbili na laki tano simu hiyo haikuwahi kupatikana tena.

9. ADINANI alikuwa na mpenzi wake mwingine Dodoma,ADINANI alimpigia mpenzi wake huyo kumjulisha kuwa amekamatwa na Polisi na kumtaarifu kuwa kama anamtafuta amtafute kupitia rafiki yake mwenye namba 0742866092

Alipompigia mtu huyo alikata simu ya kawaida akapiga video call na kuwataarifu ADINANI hayupo tena Duniani

10. Gari ya ADINANI yenye usajili T146 DPY imeonekana kituo cha Polisi Selander bridge.


View attachment 3040943
NIna hakika na jambo moja tu, ukiua mtu au ulishiriki kwenye mauaji lazima utakuja kulipa tu hapa hapa duniani kama so wewe basi kizazi chako kitalipia tu, watu wanajisahau kama kuna mungu wa haki, na wao pia hawataishi milele
 
Siku hizi ukiwa jambazi hasa wa kutumia silaha, polisi wanamalizana na ww mapema sana...

Huyu jamaa ndugu waseme kwa nini alienda kukamatiwa mwanza? Mwanza alifuata nini!
 
2. Adinani Hussein Mbezi alizaliwa mwaka 1992 ni mfanyabiashara anaye miliki vituo 11 vya kuoshea magari Dar es saalam vya "ONE TOUCH" Pia ni mwanasiasa ambaye alishawahi kuwa CCM baadae akagombea udiwani kupitia ACT WAZALENDO uchaguzi wa 2020 kata ya Yombo Vituka.
Hapa ndipo ilipoanzia shida
 
Hata kama alikuwa ana tuhuma za uhalifu, sheria itumike na apewe adhabu stahiki kwa mujibu wa sheria, sio kutekka na kuuwa watu hivyo aisee
Haya mambo mazito sana
Mkuu kuna watu wengine huwa wana malizana nao kimya kimya mkuu eidha kwenye kupata taarifa nk
Narudia tena,ukiona mtu anapelekwa tazara jua kuna jambo zito
Na haya mambo hayajaanza leo

Ova
 
Hapa naona kuna mambo mengi ndani yake. Kuna siasa, biashara, mchepuko. Huenda kuna kimoja kakikanyaga sicho. Pamoja na yote sheria zipo, ila kwakuwa kila mtu mbabe ndiyo haya yanatokea.

Polisi na rushwa hawa hizo hela wazirudishe, I wish ningewasaidia but undugu na kazi ni vitu viwili tofauti! Mwenyezi Mungu awape uvumilivu ndugu, katika kipindi hiki kigumu. Hakuna mtu anayepotea kama upepo, ukweli utajulikana tu.
 
Tanzania ni mchanganyiko wa demokrasia ya magharibi na mashariki. It is better to exercise restraint in many issues and act reasonable
 
Staki Shari sizani kama hawataki Shari polisi wa pale yaani wanatesaa afu kituo kinaitwa staki Shari
Tazara ndy mwisho wa matatizo
nkulize swali ulishawahi ona movement ya watu pale ukiwa unapita 😄 pako kimya sana
Staki shari pale sasa kulikuwa na muembe unaitwa msemakweli 😄 ukipelekwa pale utasema tu

ova
 
Back
Top Bottom