LGE2024 Ado Shaibu: ACT haturidhishwi na uandikishaji, Bila uandikishaji wa Haki, hakuna uchaguzi wa Haki

LGE2024 Ado Shaibu: ACT haturidhishwi na uandikishaji, Bila uandikishaji wa Haki, hakuna uchaguzi wa Haki

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema chama hicho haridhishwi na zoezi la uandikishaji wa Wapigakura linaloendelea hivi nchini.

Ado Shaibu ameyasema hayo leo Oktoba 13, 2024 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya ACT Wazalendo, Dar es salaam.

Amesema: "Bila uandikishaji wa haki, hakuna uchaguzi wa haki. Tumeona udanganyifu, upendeleo wa wazi kwa chama cha mapinduzi na kusuasua kwa TAMISEMI katika kuhakikisha hatua hii inapita kwa ufanisi."

Soma Pia: Ado Shaibu: Wasimamizi wa vituo vya uandikishaji wapiga kura kuwanyima mawakala kujua idadi ya waliojiandikisha ni bomu

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji utafanyika Novemba 27, 2024 na hivi sasa zoezi la uandikishaji linaendelea na litakamilika Oktoba 20, 2024.
 
Back
Top Bottom