Pre GE2025 Ado Shaibu: ACT Wazalendo, CHADEMA na vyama vingine makini vya upinzani tuungane kuing'oa CCM madarakani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu ametoa rai kwa CHADEMA na vyama vingine makini vya upinzani nchini kuungana kupigania mazingira ya kidemokrasia ikiwemo Katiba mpya, Tume Huru ya Uchaguzi, mageuzi ya Jeshi la Polisi na uhuru wa vyama vya siasa kufanya shughuli zake, ambapo amesema kuwa kuwa chama hicho kipo tayari kushirikiana ili kuhakikisha CCM inaondoka madarakani

"Sisi tuna itikadi, falsafa na sera tofauti, tuna mikakati tofauti, sisi tunachuana katika kinyang'anyiro cha madaraka au sio, tukienda hapo sisi ni vyama tofauti lakini ukweli ni kwamba ni muhimu sana kwa vyama vya upinzani, vyama makini vya upinzani kama tunataka kuiondosha CCM, kama tunataka kuimaliza mapema CCM ni lazima sisi tushirikiane kwa pamoja kama vyama vya upinzani"

Katibu Mkuu huyo amefafanua maeneo ya kuanzia kwa vyama vya upinzani kuungana na kushirikian ambapo amesema, "ni lazima tushikamane kupigania Katiba mpya, Katiba mpya sio ajenda ya chama kimoja cha siasa ni lazima tushikamane, tushikamane tupiganie Tume Huru ya Uchaguzi, ni lazima tushikamane kupigania mageuzi katika uendeshaji wa Jeshi la Polisi na vyombo vya Ulinzi na Usalama, ni lazima tushikamane, ni lazima tushikane kupigania uhuru wa kisiasa za Tanzania"

Katika kusisitiza azma hiyo Ado Shaibu amesema kuwa chama hicho kipo tayari kuungana, "ACT Wazalendo tupo teyari kufanya kazi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na vyama vingine vya upinzani ambavyo ni makini katika agenda hizi za kupigania demokrasia ya Tanzania"

Kauli hiyo ameitoa akihitimisha ziara ya kuyafikia majimbo 214 ya Tanzania Bara jimboni Muleba Kusini, mkoani Kagera Septemba 03.2024.

Jambo
 
Hivi hakuna mengine yenye kuwezekana kufanyika yakatiliwa juhudi zaidi hayo kuliko haya mawazo matupu ya kila siku ya kumtoa ccm madarakani?
 
Ccm hawatatoka madarakani kwa vyama kuungana, bali watatoka kwa machafuko ama mapinduzi ya kijeshi. Ifahamike ccm haikai madarakani kwa njia ya kura, bali kwa mbeleko ya vyombo vya dola.
 
Ndio tatizo lenu watanzania mnafikiri negatively sana na mnadhani CCM ni mlima Kilimanjaro hakuna siku itaondoshwa. Nani alifikiri KANU, ZANU na vyama vikongwe Africa vingekuwa historia siku moja? ANC nayo ipo mbioni kuondoka.

Hamtoa ushirikiano wowote wa hali wala wa mali kazi kufikiri CCM itabaki milele. Mnashindwa hata kuona kwamba mbuyu hata uweje wakishindwa watu kuung’oa ipo siku utakufa na kuondoka wenyewe? CCM itaondoka tu hata kabla hamjafa ni suala la muda tu. Wako wapi akina Mobutu, Ghaddafi, na madikteta wengine Afrika na vyama vyao?
Anaota mchana kweupe mbuzi wanakula majani!

Hivi hakuna mengine yenye kuwezekana kufanyika yakatiliwa juhudi zaidi hayo kuliko haya mawazo matupu ya kila siku ya kumtoa ccm madarakani?

Don't trust hizi mbwa
 
Ndio tatizo lenu watanzania mnafikiri negatively sana na mnadhani CCM ni mlima Kilimanjaro hakuna siku itaondoshwa. Nani alifikiri KANU, ZANU na vyama vikongwe Africa vingekuwa historia siku moja? ANC nayo ipo mbioni kuondoka.

Hamtoa ushirikiano wowote wa hali wala wa mali kazi kufikiri CCM itabaki milele. Mnashindwa hata kuona kwamba mbuyu hata uweje wakishindwa watu kuung’oa ipo siku utakufa na kuondoka wenyewe? CCM itaondoka tu ninyi kabla hamjafa ni suala la muda tu. Wako wapi akina Mobutu, Ghaddafi, na madikteta wengine Afrika na vyama vyao?
Wataondoshwa hiyo ni lazima ila si kuamini kwa njia ya ACT
 
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu ametoa rai kwa CHADEMA na vyama vingine makini vya upinzani nchini kuungana kupigania mazingira ya kidemokrasia ikiwemo Katiba mpya, Tume Huru ya Uchaguzi, mageuzi ya Jeshi la Polisi na uhuru wa vyama vya siasa kufanya shughuli zake, ambapo amesema kuwa kuwa chama hicho kipo tayari kushirikiana ili kuhakikisha CCM inaondoka madarakani

"Sisi tuna itikadi, falsafa na sera tofauti, tuna mikakati tofauti, sisi tunachuana katika kinyang'anyiro cha madaraka au sio, tukienda hapo sisi ni vyama tofauti lakini ukweli ni kwamba ni muhimu sana kwa vyama vya upinzani, vyama makini vya upinzani kama tunataka kuiondosha CCM, kama tunataka kuimaliza mapema CCM ni lazima sisi tushirikiane kwa pamoja kama vyama vya upinzani"

Katibu Mkuu huyo amefafanua maeneo ya kuanzia kwa vyama vya upinzani kuungana na kushirikian ambapo amesema, "ni lazima tushikamane kupigania Katiba mpya, Katiba mpya sio ajenda ya chama kimoja cha siasa ni lazima tushikamane, tushikamane tupiganie Tume Huru ya Uchaguzi, ni lazima tushikamane kupigania mageuzi katika uendeshaji wa Jeshi la Polisi na vyombo vya Ulinzi na Usalama, ni lazima tushikamane, ni lazima tushikane kupigania uhuru wa kisiasa za Tanzania"

Katika kusisitiza azma hiyo Ado Shaibu amesema kuwa chama hicho kipo tayari kuungana, "ACT Wazalendo tupo teyari kufanya kazi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na vyama vingine vya upinzani ambavyo ni makini katika agenda hizi za kupigania demokrasia ya Tanzania"

Kauli hiyo ameitoa akihitimisha ziara ya kuyafikia majimbo 214 ya Tanzania Bara jimboni Muleba Kusini, mkoani Kagera Septemba 03.2024.

Jambo
Tatizo wananchi hatujui sera zao, watatuleteaje maendeleo. Kuutwa vyama pinzani wanasubiri matukio ili wapite nayo kama upepo. Upinzani tunaweza kuwaita ni wakosoaji wa CCM, wasiojua wanataka kufanya nini. Nawashauri kabla ya kuwaza kuungana wajitafakari waeleze sera zao badala yakua makundi ya amsha amsha!
 
Ndio tatizo lenu watanzania mnafikiri negatively sana na mnadhani CCM ni mlima Kilimanjaro hakuna siku itaondoshwa. Nani alifikiri KANU, ZANU na vyama vikongwe Africa vingekuwa historia siku moja? ANC nayo ipo mbioni kuondoka.

Hamtoa ushirikiano wowote wa hali wala wa mali kazi kufikiri CCM itabaki milele. Mnashindwa hata kuona kwamba mbuyu hata uweje wakishindwa watu kuung’oa ipo siku utakufa na kuondoka wenyewe? CCM itaondoka tu hata kabla hamjafa ni suala la muda tu. Wako wapi akina Mobutu, Ghaddafi, na madikteta wengine Afrika na vyama vyao?
Kwanza pole sana kwa vidonda vya tumbo vinavyokusumbua ushauri wa dokta kunywa juice ya pili pili kichaa utapona maradhi yako ya chuki na roho mbaya pili hivyo vyama vyako havina uwezo wala nia thabiti kuiondoa ccm hata wewe ni mnafiki mmoja wapo kwenye ukweli tarehe 23/9/24 tulimuona mbowe na mwanawe tu wewe ulikuwa wapi?
 
Akili ndogo ni tatizo kubwa kwa watanzania wengi.
 
Ccm hawatatoka madarakani kwa vyama kuungana, bali watatoka kwa machafuko ama mapinduzi ya kijeshi. Ifahamike ccm haikai madarakani kwa njia ya kura, bali kwa mbeleko ya vyombo vya dola.
Uko nchi gani ndugu yangu unayehamasisha machafuko?
 
Ndio tatizo lenu watanzania mnafikiri negatively sana na mnadhani CCM ni mlima Kilimanjaro hakuna siku itaondoshwa. Nani alifikiri KANU, ZANU na vyama vikongwe Africa vingekuwa historia siku moja? ANC nayo ipo mbioni kuondoka.

Hamtoa ushirikiano wowote wa hali wala wa mali kazi kufikiri CCM itabaki milele. Mnashindwa hata kuona kwamba mbuyu hata uweje wakishindwa watu kuung’oa ipo siku utakufa na kuondoka wenyewe? CCM itaondoka tu hata kabla hamjafa ni suala la muda tu. Wako wapi akina Mobutu, Ghaddafi, na madikteta wengine Afrika na vyama vyao?
Kuondoka itaondoka tu hakuna kinachobaki milele ila kwa sasa hakuna juhudi zozote za dhati za kuiondoa zaidi ya matamanio matupu ya kutaka kuona ccm inaondoka madarakani, kinachoendelea sasa ni kelele tu ambazo tushazichoka.

Kama mtaendelea hivi hivi kufanya yale yale basi matokeo yatabaki hayo hayo siku zote hadi pale ccm itakapojifia yenyewe, ndio maana nasema bora mfanye yanayowezekana kufanyika kuliko kupiga kelele huku mitandaoni za matamanio ya kuondoa ccm.
 
Kuondoka itaondoka tu hakuna kinachobaki milele ila kwa sasa hakuna juhudi zozote za dhati za kuiondoa zaidi ya matamanio matupu ya kutaka kuona ccm inaondoka madarakani, kinachoendelea sasa ni kelele tu ambazo tushazichoka.
Watanzania ni watu wa kuchoka tu labda kitu hawachoki ni kubeti.
 
Ccm hawatatoka madarakani kwa vyama kuungana, bali watatoka kwa machafuko ama mapinduzi ya kijeshi. Ifahamike ccm haikai madarakani kwa njia ya kura, bali kwa mbeleko ya vyombo vya dola.
Hao wa kufanya machafuko mkuu ndio nyie mnaoshinda humu mitandaoni au wale wa huku mitaani mnaosema ni wajinga kisa wanashabikia simba na yanga na kuacha kufutilia mambo ya msingi? Mkuu katika hii nchi ccm sio mzizi wa tatizo bali ni sehemu tu ya madhara ya tatizo ya hilo tatizo.
 
Tatizo wananchi hatujui sera zao, watatuleteaje maendeleo. Kuutwa vyama pinzani wanasubiri matukio ili wapite nayo kama upepo. Upinzani tunaweza kuwaita ni wakosoaji wa CCM, wasiojua wanataka kufanya nini. Nawashauri kabla ya kuwaza kuungana wajitafakari waeleze sera zao badala yakua makundi ya amsha amsha!
Kwamba ccm ndio inasera Kwa akili yako haya tuambie sera ya ccm ni ipi tofauti na kuteka na kuuwa watu.
 
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu ametoa rai kwa CHADEMA na vyama vingine makini vya upinzani nchini kuungana kupigania mazingira ya kidemokrasia ikiwemo Katiba mpya, Tume Huru ya Uchaguzi, mageuzi ya Jeshi la Polisi na uhuru wa vyama vya siasa kufanya shughuli zake, ambapo amesema kuwa kuwa chama hicho kipo tayari kushirikiana ili kuhakikisha CCM inaondoka madarakani

"Sisi tuna itikadi, falsafa na sera tofauti, tuna mikakati tofauti, sisi tunachuana katika kinyang'anyiro cha madaraka au sio, tukienda hapo sisi ni vyama tofauti lakini ukweli ni kwamba ni muhimu sana kwa vyama vya upinzani, vyama makini vya upinzani kama tunataka kuiondosha CCM, kama tunataka kuimaliza mapema CCM ni lazima sisi tushirikiane kwa pamoja kama vyama vya upinzani"

Katibu Mkuu huyo amefafanua maeneo ya kuanzia kwa vyama vya upinzani kuungana na kushirikian ambapo amesema, "ni lazima tushikamane kupigania Katiba mpya, Katiba mpya sio ajenda ya chama kimoja cha siasa ni lazima tushikamane, tushikamane tupiganie Tume Huru ya Uchaguzi, ni lazima tushikamane kupigania mageuzi katika uendeshaji wa Jeshi la Polisi na vyombo vya Ulinzi na Usalama, ni lazima tushikamane, ni lazima tushikane kupigania uhuru wa kisiasa za Tanzania"

Katika kusisitiza azma hiyo Ado Shaibu amesema kuwa chama hicho kipo tayari kuungana, "ACT Wazalendo tupo teyari kufanya kazi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na vyama vingine vya upinzani ambavyo ni makini katika agenda hizi za kupigania demokrasia ya Tanzania"

Kauli hiyo ameitoa akihitimisha ziara ya kuyafikia majimbo 214 ya Tanzania Bara jimboni Muleba Kusini, mkoani Kagera Septemba 03.2024.

Jambo
Kwani lazima ACT waungane na CDM?Waungane na NLD.
 
Watanzania ni watu wa kuchoka tu labda kitu hawachoki ni kubeti.
Sio kubet tu na kupiga umbeya wa kisiasa humu huwa hawachoki, wanabadilisha umbeya huu mara ule leo anajadiliwa huyu kesho wanajadili jambo lile mwisho wa siku hakuna cha maana.
 
Back
Top Bottom