Pre GE2025 Ado Shaibu: ACT Wazalendo, CHADEMA na vyama vingine makini vya upinzani tuungane kuing'oa CCM madarakani

Pre GE2025 Ado Shaibu: ACT Wazalendo, CHADEMA na vyama vingine makini vya upinzani tuungane kuing'oa CCM madarakani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hivi hakuna mengine yenye kuwezekana kufanyika yakatiliwa juhudi zaidi hayo kuliko haya mawazo matupu ya kila siku ya kumtoa ccm madarakani?
Kama yapi bosi? Pengine wenzio hawafikiri vizuri, wape shule.
 
Ndio tatizo lenu watanzania mnafikiri negatively sana na mnadhani CCM ni mlima Kilimanjaro hakuna siku itaondoshwa. Nani alifikiri KANU, ZANU na vyama vikongwe Africa vingekuwa historia siku moja? ANC nayo ipo mbioni kuondoka.

Hamtoa ushirikiano wowote wa hali wala wa mali kazi kufikiri CCM itabaki milele. Mnashindwa hata kuona kwamba mbuyu hata uweje wakishindwa watu kuung’oa ipo siku utakufa na kuondoka wenyewe? CCM itaondoka tu hata kabla hamjafa ni suala la muda tu. Wako wapi akina Mobutu, Ghaddafi, na madikteta wengine Afrika na vyama vyao?

Mobutu na Gaddafi hawakuondoka wenyewe kwa kupenda.

Kuwasubiria hadi wafe wenyewe? Hivyo si ndiyo hata wao wangependa? Ya kwamba waachwe wajinafasi kwa starehe zao?

Kimsingi hilo ni sawa na kuwaacha nzige shambani, kwamba waacheni wale, wakishiba wataondoka.

CCM mbona wakae kwa kutulia tu? Suala si kuondoka bali kuondolewa!
 
Nyie si mna ndoa na CCM kule Zanzibar, na mmeunda nao Serikali ya Mapinduzi - sasa huo umoja wa kuishinda CCM ipi ndugu?
 
Uchaguzi wa serikali za mtaa wana simamia.TAMISEMI.
OFISI YA RAIS😂😂😂.kuna maigizo na vimbwanga.
 
Katika kusisitiza azma hiyo Ado Shaibu amesema kuwa chama hicho kipo tayari kuungana, "ACT Wazalendo tupo teyari kufanya kazi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na vyama vingine vya upinzani ambavyo ni makini katika agenda hizi za kupigania demokrasia ya Tanzania"
Jambo la kuungana vyama siyo la kuhimizana, kuomba; bali ni jambo linalo patikana ikionekana kila chama kimefanya jitihadi ya kweli katika malengo yanayo piganiwa.
Wao kama ACT- wafanye juhudi kama chama, na CHADEMA nao wafanye kama chama; ikionekana huko mbele ya safari kuwepo uhitaji wa pamoja kumaliza kazi ya kuiangusha hiyo CCM; vyama hivyo vitaungana kama kufanya hivyo ndiyo lazima ya kuiangusha CCM. Kuungana sasa hivi ni kutafuta njia za kudhoofishana tu.
 
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu ametoa rai kwa CHADEMA na vyama vingine makini vya upinzani nchini kuungana kupigania mazingira ya kidemokrasia ikiwemo Katiba mpya, Tume Huru ya Uchaguzi, mageuzi ya Jeshi la Polisi na uhuru wa vyama vya siasa kufanya shughuli zake, ambapo amesema kuwa kuwa chama hicho kipo tayari kushirikiana ili kuhakikisha CCM inaondoka madarakani

"Sisi tuna itikadi, falsafa na sera tofauti, tuna mikakati tofauti, sisi tunachuana katika kinyang'anyiro cha madaraka au sio, tukienda hapo sisi ni vyama tofauti lakini ukweli ni kwamba ni muhimu sana kwa vyama vya upinzani, vyama makini vya upinzani kama tunataka kuiondosha CCM, kama tunataka kuimaliza mapema CCM ni lazima sisi tushirikiane kwa pamoja kama vyama vya upinzani"

Katibu Mkuu huyo amefafanua maeneo ya kuanzia kwa vyama vya upinzani kuungana na kushirikian ambapo amesema, "ni lazima tushikamane kupigania Katiba mpya, Katiba mpya sio ajenda ya chama kimoja cha siasa ni lazima tushikamane, tushikamane tupiganie Tume Huru ya Uchaguzi, ni lazima tushikamane kupigania mageuzi katika uendeshaji wa Jeshi la Polisi na vyombo vya Ulinzi na Usalama, ni lazima tushikamane, ni lazima tushikane kupigania uhuru wa kisiasa za Tanzania"

Katika kusisitiza azma hiyo Ado Shaibu amesema kuwa chama hicho kipo tayari kuungana, "ACT Wazalendo tupo teyari kufanya kazi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na vyama vingine vya upinzani ambavyo ni makini katika agenda hizi za kupigania demokrasia ya Tanzania"

Kauli hiyo ameitoa akihitimisha ziara ya kuyafikia majimbo 214 ya Tanzania Bara jimboni Muleba Kusini, mkoani Kagera Septemba 03.2024.

Jambo
KWA HIYO CCM WAUNGANE KUING'OA CCM 🙄🙄🙄🙄🙄🙄
 
Huyu jamaa bado ana siasa za vyuoni, nadhani anahitaji mentorship zaidi, Zitto amtafutie training huko ughaibuni.

ACT wazalendo zanzibar inajua inachofanya, nikimuona Jussa YouTube lazima nimsikilize
 
 
Back
Top Bottom