Pre GE2025 Ado Shaibu: ACT Wazalendo, CHADEMA na vyama vingine makini vya upinzani tuungane kuing'oa CCM madarakani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu ametoa rai kwa CHADEMA na vyama vingine makini vya upinzani nchini kuungana kupigania mazingira ya kidemokrasia ikiwemo Katiba mpya, Tume Huru ya Uchaguzi, mageuzi ya Jeshi la Polisi na uhuru wa vyama vya siasa kufanya shughuli zake, ambapo amesema kuwa kuwa chama hicho kipo tayari kushirikiana ili kuhakikisha CCM inaondoka madarakani

"Sisi tuna itikadi, falsafa na sera tofauti, tuna mikakati tofauti, sisi tunachuana katika kinyang'anyiro cha madaraka au sio, tukienda hapo sisi ni vyama tofauti lakini ukweli ni kwamba ni muhimu sana kwa vyama vya upinzani, vyama makini vya upinzani kama tunataka kuiondosha CCM, kama tunataka kuimaliza mapema CCM ni lazima sisi tushirikiane kwa pamoja kama vyama vya upinzani"

Katibu Mkuu huyo amefafanua maeneo ya kuanzia kwa vyama vya upinzani kuungana na kushirikian ambapo amesema, "ni lazima tushikamane kupigania Katiba mpya, Katiba mpya sio ajenda ya chama kimoja cha siasa ni lazima tushikamane, tushikamane tupiganie Tume Huru ya Uchaguzi, ni lazima tushikamane kupigania mageuzi katika uendeshaji wa Jeshi la Polisi na vyombo vya Ulinzi na Usalama, ni lazima tushikamane, ni lazima tushikane kupigania uhuru wa kisiasa za Tanzania"

Katika kusisitiza azma hiyo Ado Shaibu amesema kuwa chama hicho kipo tayari kuungana, "ACT Wazalendo tupo teyari kufanya kazi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na vyama vingine vya upinzani ambavyo ni makini katika agenda hizi za kupigania demokrasia ya Tanzania"

Kauli hiyo ameitoa akihitimisha ziara ya kuyafikia majimbo 214 ya Tanzania Bara jimboni Muleba Kusini, mkoani Kagera Septemba 03.2024.

Jambo
Kuungana na ACT Wazalendo ni upumbavu!
 
Kwamba ccm ndio inasera Kwa akili yako haya tuambie sera ya ccm ni ipi tofauti na kuteka na kuuwa watu.
Unajitoa ufahamu tu, shibe inayotokana na sera nzuri ndio inayokufanya upate muda wa kuweka makalio yako na kuandika utumbo.
 
Kwani wao si wameshaungana na ccm huko zenji?!
Sasa wanatakantena waungane na chadema kuiondoa ccm ambayo wapo kwenye muungano nao.?!
 
Tatizo wananchi hatujui sera zao, watatuleteaje maendeleo. Kuutwa vyama pinzani wanasubiri matukio ili wapite nayo kama upepo. Upinzani tunaweza kuwaita ni wakosoaji wa CCM, wasiojua wanataka kufanya nini. Nawashauri kabla ya kuwaza kuungana wajitafakari waeleze sera zao badala yakua makundi ya amsha amsha!
Wewe unazijua sera za ccm?
 
Umoja ni muhimu sana ktk mapambano lakini kwa tahazali kubwa,maaàna kuna mapindikizi cha CHAMA tawala
 
Kwanini haya ya mapandikizi hatuyasikii Kenya, Uganda ila Tanzania tu?

Kweli Siasa ni sayansi na kwetu tumepigwa bao la kisigino.
 
Kwa akili za mboga mboga political party huyu mwamba lazma akaokotwe ununio kwa azma yake hio
 
CCM itang'olewa 2025 kwa aibu sana, Lakini Chadema haitaungana na wanafiki na Mamluki

Kuiondoa CCM bila kuungana labda kupitia vyama vyenye imani kali za kidini, kikabila au kikanda ambavyo ni marufuku.

Option pekee inabaki ni kusuka tabaka thabiti la "waumini kindaki ndaki katika haki."

Humo watavutika watu wenye itikadi thabiti hiyo kutokea kokote na across the board.

Vinginevyo tutacheza mno ngoma ya CCM bila kujua.

Angalizo : itunze post yako, tukijaaliwa tuonane hapa dec 1, 2025.

joka kuu, binti kiziwi, imhotep, Extrovert, Proved na wale wengine au nasema uongo ndugu zangu?
 
Kuiondoa CCM bila kuungana labda kupitia vyama vyenye imani kali za kidini, kikabila au kikanda ambavyo ni marufuku.

Option pekee inabaki ni kusuka tabaka thabiti la "waumini kindaki ndaki katika haki."

Humo watavutika watu wenye itikadi thabiti hiyo kutokea kote.

Vinginevyo bila kujua tutacheza mno ngoma ya CCM bila kujua.

Angalizo : itunze post yako, tukijaaliwa tuonane hapa dec 1, 2025.

joka kuu, binti kiziwi, imhotep na wale wengine au nasema uongo ndugu zangu?
Chadema itaungana na Wananchi, haitaungana na Mamluki
 
CCM wanapenda kusikia hivyo.

Hawataki umoja wowote dhidi yao.

Zingatia mamluki hawana alama na kina Nassari, Msigwa, Katambi, Makene, na wengi wengine nani aliwajua kabla?

Bila kuacha kukumbusha, Kwa misimamo kama hii tunza posts zako for Dec 1, 2025.
 
CCM ilipofanikiwa mno ni kuhakikisha wapinzani hawakaribiani kwenye lolote
Shida ni hao vigeugeu! Manaanza vizuri wakifika katikati wanajiondoa kwenye muungano! Kila mtu apambane kivyake!
 
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu ametoa rai kwa CHADEMA na vyama vingine makini vya upinzani nchini kuungana kupigania mazingira ya kidemokrasia ikiwemo Katiba mpya, Tume Huru ya Uchaguzi, mageuzi ya Jeshi la Polisi na uhuru wa vyama vya siasa kufanya shughuli zake, ambapo amesema kuwa kuwa chama hicho kipo tayari kushirikiana ili kuhakikisha CCM inaondoka madarakani

"Sisi tuna itikadi, falsafa na sera tofauti, tuna mikakati tofauti, sisi tunachuana katika kinyang'anyiro cha madaraka au sio, tukienda hapo sisi ni vyama tofauti lakini ukweli ni kwamba ni muhimu sana kwa vyama vya upinzani, vyama makini vya upinzani kama tunataka kuiondosha CCM, kama tunataka kuimaliza mapema CCM ni lazima sisi tushirikiane kwa pamoja kama vyama vya upinzani"

Katibu Mkuu huyo amefafanua maeneo ya kuanzia kwa vyama vya upinzani kuungana na kushirikian ambapo amesema, "ni lazima tushikamane kupigania Katiba mpya, Katiba mpya sio ajenda ya chama kimoja cha siasa ni lazima tushikamane, tushikamane tupiganie Tume Huru ya Uchaguzi, ni lazima tushikamane kupigania mageuzi katika uendeshaji wa Jeshi la Polisi na vyombo vya Ulinzi na Usalama, ni lazima tushikamane, ni lazima tushikane kupigania uhuru wa kisiasa za Tanzania"

Katika kusisitiza azma hiyo Ado Shaibu amesema kuwa chama hicho kipo tayari kuungana, "ACT Wazalendo tupo teyari kufanya kazi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na vyama vingine vya upinzani ambavyo ni makini katika agenda hizi za kupigania demokrasia ya Tanzania"

Kauli hiyo ameitoa akihitimisha ziara ya kuyafikia majimbo 214 ya Tanzania Bara jimboni Muleba Kusini, mkoani Kagera Septemba 03.2024.

Jambo
Hawa mawakalawa CCM wanatumia mbinu za kizamani sana.
 
Waungane na NCCR Mageuzi labda
 
Hivyo vyama vingine hakuna, maana hivyo vingine vyote ni vya ccm

Haipo shaka CCM akiona kauli kama hizo ana furaha sana.

Hii ya vyama kama hivyo mbona si Kenya au Uganda?

Vipi kupata wanachama walioiva kama wamasai yaani wakabila, wadini au wakanda?

Kuna hatari ya kuwa tunadhani CCM anaweza kupigwa chini kidijitali.
 
Back
Top Bottom