Pre GE2025 Ado Shaibu: ACT Wazalendo, CHADEMA na vyama vingine makini vya upinzani tuungane kuing'oa CCM madarakani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hivi hakuna mengine yenye kuwezekana kufanyika yakatiliwa juhudi zaidi hayo kuliko haya mawazo matupu ya kila siku ya kumtoa ccm madarakani?
Kama yapi bosi? Pengine wenzio hawafikiri vizuri, wape shule.
 

Mobutu na Gaddafi hawakuondoka wenyewe kwa kupenda.

Kuwasubiria hadi wafe wenyewe? Hivyo si ndiyo hata wao wangependa? Ya kwamba waachwe wajinafasi kwa starehe zao?

Kimsingi hilo ni sawa na kuwaacha nzige shambani, kwamba waacheni wale, wakishiba wataondoka.

CCM mbona wakae kwa kutulia tu? Suala si kuondoka bali kuondolewa!
 
Nyie si mna ndoa na CCM kule Zanzibar, na mmeunda nao Serikali ya Mapinduzi - sasa huo umoja wa kuishinda CCM ipi ndugu?
 
Uchaguzi wa serikali za mtaa wana simamia.TAMISEMI.
OFISI YA RAISπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚.kuna maigizo na vimbwanga.
 
Jambo la kuungana vyama siyo la kuhimizana, kuomba; bali ni jambo linalo patikana ikionekana kila chama kimefanya jitihadi ya kweli katika malengo yanayo piganiwa.
Wao kama ACT- wafanye juhudi kama chama, na CHADEMA nao wafanye kama chama; ikionekana huko mbele ya safari kuwepo uhitaji wa pamoja kumaliza kazi ya kuiangusha hiyo CCM; vyama hivyo vitaungana kama kufanya hivyo ndiyo lazima ya kuiangusha CCM. Kuungana sasa hivi ni kutafuta njia za kudhoofishana tu.
 
KWA HIYO CCM WAUNGANE KUING'OA CCM πŸ™„πŸ™„πŸ™„πŸ™„πŸ™„πŸ™„
 
Huyu jamaa bado ana siasa za vyuoni, nadhani anahitaji mentorship zaidi, Zitto amtafutie training huko ughaibuni.

ACT wazalendo zanzibar inajua inachofanya, nikimuona Jussa YouTube lazima nimsikilize
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…