Ado Shaibu: Bungeni hakuna kambi rasmi ya upinzani, tuko 11 tu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
WhatsApp Image 2026-10-03 at 18.37.34.jpeg
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, amesema bunge la sasa halina kambi rasmi ya upinzani kwa sababu wabunge wa upande wa wachache ni 11 tu, sawa na asilimia tatu.

Alitoa kauli hiyo jana katika mkutano wa hadhara wilayani Tandahimba, kata ya Kitama, mkoani Mtwara.

Ado alisema mwaka 2015 upande wa wachache ulikuwa na wabunge zaidi ya 100, lakini sasa wamebaki 11. Kwa mujibu wake, ili kuwa na kambi rasmi ya upinzani inahitajika angalau asilimia 20 ya wabunge.

“Ukigeuka upande huu unaona CCM, ukigeuka upande ule unaona CCM,” alisema.

Alieleza kuwa waliwahi kuwa na mjadala mkali kama waende bungeni au la, baadhi wakisema CCM hawana haya na wakiwachwa peke yao hakutakuwa na mtu wa kupaza sauti kutetea wananchi, barabara, kuibua ufisadi au kupinga utekaji.

Hatimaye walikubaliana kwenda bungeni si kuuza sura wala kupanga meza, bali kupaza sauti kwa niaba ya raia wa Tanzania.

“Sisi wachache tutaunguruma kama mia. Pengine wataona haya japo kidogo. Bunge ni uwanja wa mapambano na ushindi wake ni kuibua madudu, kuzungumza mambo ambayo hawatarajii,” alisisitiza Ado.
 
Ado yuko sahihi, lakini uhalisia wa hilo bunge tunaujua, hoja zinazoachwa kujadiliwa ni zile zinazotakiwa na serekali, hizo nyingine zinaharibiwa na taarifa, sijui muongozo na ubabe wa spika. Katika mazingira hayo Ado atafanya nini? Sana sana anajaribu kuhalalisha uwepo wake bungeni maana anajua wataka mabadiliko wa kweli wamelipuuza hilo bunge kibogoyo.
 
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, amesema bunge la sasa halina kambi rasmi ya upinzani kwa sababu wabunge wa upande wa wachache ni 11 tu, sawa na asilimia tatu.

Alitoa kauli hiyo jana katika mkutano wa hadhara wilayani Tandahimba, kata ya Kitama, mkoani Mtwara.

Ado alisema mwaka 2015 upande wa wachache ulikuwa na wabunge zaidi ya 100, lakini sasa wamebaki 11. Kwa mujibu wake, ili kuwa na kambi rasmi ya upinzani inahitajika angalau asilimia 20 ya wabunge.

“Ukigeuka upande huu unaona CCM, ukigeuka upande ule unaona CCM,” alisema.

Alieleza kuwa waliwahi kuwa na mjadala mkali kama waende bungeni au la, baadhi wakisema CCM hawana haya na wakiwachwa peke yao hakutakuwa na mtu wa kupaza sauti kutetea wananchi, barabara, kuibua ufisadi au kupinga utekaji.

Hatimaye walikubaliana kwenda bungeni si kuuza sura wala kupanga meza, bali kupaza sauti kwa niaba ya raia wa Tanzania.

“Sisi wachache tutaunguruma kama mia. Pengine wataona haya japo kidogo. Bunge ni uwanja wa mapambano na ushindi wake ni kuibua madudu, kuzungumza mambo ambayo hawatarajii,” alisisitiza Ado.
Amesahau kwamba wao ni wapambe tu wa mtawala?
 
Huyu naye atulie, mbona anaanza kujistukia? Nani asiyejua wao ni CCM B.
Lol
 
Back
Top Bottom