Wananchi wa Kijiji cha Kidodoma, Tunduru, wamemtaka Katibu wa ACT Wazalendo na Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado kuendeleza kasi ya kuwasemea Wananchi na makundi mbalimbali, hususan katika masuala ya haki, utekaji na changamoto zinazowakabili wananchi.
Wamesema hayo Septemba 23, 2026, wakati Ado Shaibu kiendelea na ziara yake ya kijiji kwa kijiji katika Jimbo la Tunduru Kaskazini, yenye lengo la kusikiliza changamoto za Wananchi na kuzifikisha katika maeneo husika, ikiwemo Bunge.