Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Ndugu Ado Shaibu ameeleza kuwa yanayotokea sasa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kilitokea kwao pia mwaka 2019, wakati Msajili wa Vyama vya siasa alipokataa Uteuzi wa Maalim Seif na viongozi wengine waliokuwa wameteuliwa na Halmashauri kuu.
Ado kupitia ukurasa wake wa X ameandika kusema "Mwaka 2019, Maalim Seif alipojiunga na ACT Wazalendo, Msajili wa Vyama vya Siasa alikataa uteuzi wake na viongozi wengine kushikilia nafasi mbalimbali ndani ya ACT Wazalendo kwa hoja kwamba hawakuteuliwa na Halmashauri Kuu. Hatukukubaliana na hoja zake. Lakini, tuliamua kuimaliza mechi hiyo "kibingwa". Tuliitisha kikao cha Halmashauri Kuu upesi na kuwateua watu walewale aliowakataa. Mchezo uliishia hapo.
Ado amebainisha hayo wakati huu ambapo Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa akishikilia msimamo wa Ofisi yake na kubainisha kuwa hatambui uteuzi wa Viongozi mbalimbali wa Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema walioteuliwa na kuchaguliwa na Baraza kuu la Januari 22, 2025
Viongozi ambao hawatambuliwi na Ofisi ya Msajili ni Bwana John Mnyika, Amani Golugwa, Ali Ibrahim Juma, Godbless Lema, Dkt. Rugemeleza Nshala, Rose Mayemba, Salima Kasanzu na Hafidh Ali Salehe
Taarifa ya msajili pia ilisema Ofisi yake haiwatambui Viongozi na watendaji wote walioteuliwa na Viongozi waliopatikana kwenye Kikao cha Baraza kuu la Januari 22, 2025 pamoja na Viongozi na watendaji wote walioteuliwa kwa mamlaka za Chama kushauriana na Viongozi waliopatikana Januari 22, 2025.
Pia, Soma