Ado Shaibu: Nimeambiwa bado kuna matukio ya Watoto kupotea na vifo pia Kanda ya Ziwa, hatutakiwi kukaa kimya

Ado Shaibu: Nimeambiwa bado kuna matukio ya Watoto kupotea na vifo pia Kanda ya Ziwa, hatutakiwi kukaa kimya

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu ametuma tena Salamu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kulitazama suala la kupotea kwa Watoto kwa umakini zaidi.

Ado ameyasema hayo wakati anahutubia Wananchi wa Jimbo la Mbogwe Mkoani Geita, Septemba 29, 2024.

Amesema "Nilipokwenda Busega nimekuta Wanalima, Watoto wanapotea, hawajulikani wanapelekwa wapi, wanasema vifo vinaongezeka Watu wanaouawa.

“Nimekuja leo Mbogwe Watu wananieleza jambo hilohilo katika maeneo ya Kanda ya Ziwa kunaongezeka sana visa vya Watoto wanapotea na Watu wazima wanaouawa, visa hivyo nimevikuta maeneo mengi hapa Kanda ya Ziwa."

Aidha, Kiongozi huyo amemtaka Rais Samia kulitazama jambo hili kwa uzito mkubwa kutumia intelijensia ya Serikali kubaini Watoto wanakwenda wapi.

Wakati huohuo, Ado amerejea wito wa Chama chake kutaka hatua kubwa zaidi kuchukuliwa kufuatia matukio haya ya kutekwa, kuuawa na kupotea kwa watu nchini kwa kuundwa Tume ya Kijaji (Judicial Commission of Inquiry) ambayo itachunguza matukio yote ya aina hiyo.

Ameongeza kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Eng. Hamadi Masauni na Inspekta Jenerali wa Polisi wajiuzulu nafasi zao kama sehemu ya uwajibikaji.

Ado anaendelea na ziara ya chama hicho katika kanda ya ziwa Ambapo anapita mikoa ya Simiyu, Mara, Mwanza, Geita na Kagera kujiandaa chama hicho kusimamishwa wagombea wa serikali za Mitaa vijiji na vitongoji kote nchini.

Chanzo: ACT Wazalendo
 
Hivi Masauni na Wambura wakijiuzulu nyadhifa zao,mauaji na upotevu wa watoto utakwisha?
 
Back
Top Bottom