Pre GE2025 Ado Shaibu: Tunatakiwa kuangalia vyama vyetu ya Siasa vina maslahi gani dhidi ya Rushwa

Pre GE2025 Ado Shaibu: Tunatakiwa kuangalia vyama vyetu ya Siasa vina maslahi gani dhidi ya Rushwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Katibu Mkuu ACT Wazalendo Ado Shaibu akiwa kwenue mjadala wa X (Twitter ya JamiiForums) ametoa mchango wake kuhusu rushwa. Akitoa hoja hiyo anasema:

Tunatakiwa kuangalia vyama vyetu ya Siasa vina maslahi gani dhidi ya Rushwa, mfano huko nyuma Rais wa Awamu ya Tano aliwahi kutaka kurasimisha Rushwa inayoombwa na Askari wa Barabarani ni halali

Uchunguzi ukifanywa kwenye vyama vya Siasa utaonesha bado hatujawa na msukumo mkubwa wa kupambana na Rushwa

Huko nyuma Vyombo vya Habari vilikuwa vikiripoti sana kuhusu Rushwa, magazeti yaliandika na kuripoti matukio ya Rushwa ndogo na kubwa, hivyo bila kuwa na Vyombo vya Habari vyenye Uhuru itakuwa ngumu kupambana dhidi ya Rushwa


Tunatakiwa kuangalia hali ya Mahakama zetu, tukiziboresha zitasaidia Wananchi kupata haki na kuwa na imani na Mahakama, pia tunatakiwa kuangalia taasisi zetu za Kirasia, ni muhimu ziwe huru katika kufanya kazi zao

Nini kifanyike kudhibiti Rushwa? Hali ya Umma wenyewe inatakiwa kuangaliwa, inatakiwa kutambua jukuu hilo la kupambana na Rushwa ni lao pia isionekane ni jukumu la Watu fulani.

PIA SOMA
- LIVE - Je, nini kifanyike ili kuongeza Ushiriki wa Wananchi katika Mapambano dhidi ya Rushwa?
 
Back
Top Bottom