Akizungumza jana, Septemba 8, 2026, kwenye Mkutano wa Kitaifa wa Kutafakari Hali ya Kisiasa Nchini, Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu, amesisitiza kuwa mchakato wa maridhiano ya kisiasa nchini unahitaji mazingira na msingi sahihi ili uweze kuzaa matunda ya kweli.
Akitolea uzoefu wa Afrika Kusini na namna kuachiwa kwa Nelson Mandela kulivyokuwa ishara kuu ya maridhiano, Ado Shaibu amemtaja Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, kama muunganiko muhimu katika muktadha wa maridhiano ya Tanzania. Ameeleza kuwa kesi inayomkabili Lissu ni ya kisiasa na inapaswa kumalizwa kisiasa ili kujenga taswira ya kweli ya maridhiano na kutoa funzo la dhati la kiutawala nchini.