Adui mkubwa wa Manara ni wakati

Adui mkubwa wa Manara ni wakati

Haji Manara anaweza kudhani ana maadui wengi wanaomfanyia fitina, lakini ukweli ni kwamba adui wake mkuu kwa sasa ni wakati. Wakati unapobadilika dhidi yako, unaweza kushangazwa na mambo yanayotokea na kudhani watu wanakufanyia fitina.

Kwa upande wa Ally Kamwe, wakati unamfaa sana. Kila anachofanya kinakuwa rahisi na kukubalika kwake si jambo gumu. Ukweli ni kuwa, kwa kazi yoyote inayohitaji mitandao, kijana wa kizazi cha Z kama Ally anaweza kufanya kazi kwa urahisi zaidi kuliko watu wenye umri kama wa Manara, bila kujali uzoefu. Teknolojia inawapa nafasi vijana wanaoibukia pamoja na maendeleo ya teknolojia yenyewe.

Kama kazi ya usemaji ingekuwa bado inategemea zaidi redio na magazeti kama zamani, Manara angebaki kuwa bora. Lakini ukichanganya na matumizi ya mitandao ya kijamii, vijana kama Ally Kamwe ndio wanaoweza kustawi na kutamba zaidi. Inawezekana viongozi kama Hersi wanapata changamoto ya kujua nafasi sahihi ya kumweka Manara kwa sababu wakati umekuwa kikwazo kikubwa kwake. Zama zimeshabadili
ka.
Mkuu umesema kitu kikubwa sana.
Wakati ndio adui wa Manara.
Nakumbuka DJ Fetty alikuwa ni mmoja wa watangazaji waliokuwa wanapednwa sana na vijana katika kipindi cha XXL akiwa kama mtangazaji mkali wa kike. Kipindi akaacha utangazaji alipokuja kurejea akakuta vijana wa kike washachukua nafasi akawa kama irrelevant. Luckily aliondolewa kwenye kipindi hicho akapewa kipindi kinachomstahili.
Haji kwa sasa usemaji awaachie vijana na zama za usemaji kuwa wa matusi inaelekea watu hawautaki tena sasa hivi vijana wakikutana wanapigana vijembe vyenye kuchekesha kiasi kwamba kila mtu anabaki anafurahi sio kama vya manara.
 
Ashura Cheupe atafute kazi nyingine sio lazima uwe msemaji, kama vipi aende Pamba Jiji aone kama ata trend bila Simba na Yanga
 
Kwani kuna jambo Manara kalifanya zaidi ya kuwa msemaji wa bidhaa gani sijui ile ya tiGO?
 
Haji Manara ni mtu mwenye nongwa! Na kufanya kazi na mtu mwenye nongwa, kunahitaji uwe na moyo wa uvumilivu sana. Binafsi naunga mkono uongozi wa Yanga kumuweka pembeni huyo mamluki.
Mmesahau mema aliyowatendea Haji mpaka mnatamani atoswe?
 
Yule jamaa ana shida wee mtu gani kila mtu kwako awe mbaya?

Mtu alishaoa na kuacha wanawake zaidi ya watano.
Kwa maelezo yake wananwonea gerè anakuwa maarufu mno. Ile ya kuambiwa ni mwanachama wà kawaida pale yanga naona imemwuma na anamwona Hersi mtu mbaya sana, mzuri kwake ni Gharib tu. Ila ipo siku na Gharib atamfahamu tu.
 
Sasa Manara kamzidi umri Hersi...
Anataka Hersi amuweke kama mfagizi aje amlaani? 😃😃akae tuu kwa kutulia kashazeeka...
 
Kila kitu kina wakati wake

Lazima mtu ukubaliane na hilo

Ova
 
Back
Top Bottom