SoC02 Adui mpya kwa wanaume aliyeibuka karne hii ya 21

SoC02 Adui mpya kwa wanaume aliyeibuka karne hii ya 21

Stories of Change - 2022 Competition

muhin

Member
Joined
Jul 16, 2021
Posts
7
Reaction score
6
Historia ya ulimwengu kuna nadharia za kiimani na za kisayansi ambazo zimetofautiana jinsi ya kuelezea kuumbwa kwa ulimwengu mzima na vilivyomo ndani ya ulimwengu huo.

Kwa mujibu wa sayansi ulimwengu ulitokea baada ya migandamizo na milipuko ya gesi mbalimbali na kuunda ulimwengu ambao miongoni mwa vitu vinavyopatikana ni hii dunia yetu ambayo ina vitu na viumbe ambavyo huwa vimegawanyika katika jinsia tofauti tofauti.

Ukija kiimani kuna imani nyingi duniani lakini nyingi kati ya imani hizo zinaeleza uwepo wa mungu mwenye nguvu ya kufanya lolote ambaye ni muanzilishi wa ulimwengu huu ambaye yeye ndo mtengenezaji wa ulimwengu na vilivyomo ndani hivyo kwa mujibu wa baadhi ya imani mungu mwenyezi baada ya kuumba ulimwengu alichagua sayari moja ambayo ni dunia na kuweka viumbe kwa jinsia tofauti tofauti na hapo ndipo kiumbe aliyeitwa binadamu alipojulikana kwenye uso huu wa sayari ya dunia.

Binadamu huyo baada ya kuumbwa alikua na jinsia ya kiume baadae mungu akafanya kwa uwezo wake na kumuumbia kiumbe kama yeye mwenye jinsia ya kike na kumfanya kiumbe huyo mwenye jinsia ya kike kua mke na yule mwenye jinsia ya kiume kua mume .

Zilipita karne na karne binadamu hao wawili ndo wakawa chanzo cha mimi na wewe kuwepo leo duniani lakini kama nilivyosema karne nyingi zimepita na kama tujuavyo kutoka kwenye vitabu tofauti tofauti kila watu kwenye zama zao walikua na mitihani iliyowakumba na walijitahidi kutumia akili,nguvu na uwezo wao wakiasili juu ya kupambana na matatizo ya zama husika.

Mpaka kufikia karne hii ya 21 miongoni mwa matatizo ya zama zetu hizi za karne ya 21 yapo maradhi ambayo kwa zama zilizopita huenda hayakuwepo kabisa au yalikuwepo kwa watu wachache na wa umri fulani na kwa karne yetu yapo maradhi kama hayo lakini katika wingi uliokithiri na kwa watu wa umri tofauti tofauti kinyume na hapo zamani.

kwa karne hii ya 21 kiukweli ni aibu yule kiumbe wa kwanza kabisa ambaye alipewa uwezo wa kusababisha mimi na wewe tuwepo ule uwezo wake wa kusababisha kujazwa kwa dunia hii kila baada ya siku husikika eti unapungua.

Upungufu wa nguvu za kiume ni janga kubwa kwenye karne hii kiukweli amekua adui ambaye huenda kwa miongo ijayo akazidi kama hatotafutiwa ufumbuzi wa haraka au kutopewa uzito unaostahili.

Uhalisia ulivyo kwenye jamii zetu kiumbe huyu mwenye jinsia ya kiume wa umri tofauti tofauti wengi hutafuta tatuzi la adui huyu kwa kufanya jitihada mbali mbali za kutatua tatizo hilo.

Wapo matabibu ambao hueleza sababu za tatizo ambazo ni nyingi mfano wa sababu hizo kwa mimi nionavyo hugawanyika kwenye makundi kama vile mfumo wa maisha wa mtu mwenyewe , magonjwa , mazingira pamoja na maendeleo ya sayansi na teknologia kwenye kubadilisha au kuboresha baadhi ya vitu au huduma ambazo hutumiwa na mwanadamu.

Hatua zipi tuchukue juu ya adui huyu ? kwa mujibu wa taratibu ni lazima tuzipitie sababu sabibishi za tatizo hili la upungufu wa nguvu za kiume kwa maana tufike kwenye vituo vya afya mtaalamu wa afya yeye ndiye atakayegundua sababu ipi iliyosabisha tatizo na atakuelekeza njia ipi utumie ya kutatua hilo.

Kwa hali ilivyo kwa ukubwa wa tatizo hili kuna haja kwa sasa kama yalivyo mapambano ya maaadui wengine tunaopambana nao kwenye zama zetu hizi ni muda sasa wa adui huyu naye awekewe jitihada mbadala na si kutibu tatizo tu waswahili husema kinga ni muhimu kuliko tiba.

Ni muda wa kusoma historia kuangalia watu wa karne za zamani waliishi vipi sababu watu wa zama hizo hakukuwepo na tatizo hili , kwa kufanya hivyo naamini huenda tukapiga hatua kadhaa juu ya kupambana na adui huyu.

Ni muda wa kupanga mbinu na taratibu mbalimbali haswa kwenye sekta ya afya na wadau mbalimbali kama yalivyo mapambano ya magonjwa mengine na si kuchukulia kawaida huenda tukazidi kuwa na vijana ambao wengi wakawa na tatizo hilo kwa siku za usoni.

Ni muda wa kuongeza elimu juu ya janga hili sababu wengi hushindwa kupata msaada au matibabu yanayopaswa kulingana na sababu sababishi ya adui huyo , wengi wana elimu ndogo juu ya adui huyu na pia wengi hufikiri kutafuta tiba ya tatizo hili kabla ya kuangalia sababu sababishi ya hili kwa sababu ya elimu ndogo juu ya hili , naamini tukizidisha elimu kama elimu tuitoayo kwenye malaria na UKIMWI huenda tukapiga hatua.

Ni muda wa kuzirudia mila na desturi zetu zenye faida kwa maana mila na desturi nyingi ambazo zilifanywa na babu zetu ambazo hazina athari mbaya wao kwa zama zao walimteketeza pakubwa adui huyu . Hivyo basi tuangalie mila zetu yenye manufaa tuyachukue na yale yasiyo na manufaa tuyaache.

Kwa kumalizia kama vidole jinsi vilivyo tofauti na ndivyo sisi wanadamu tulivyo tofauti hatufanani kwenye mambo tofauti tofauti mfano akili au uwezo wa uelewa upo tofauti baina ya watu , uzuri wa umbo na mwili tupo tofauti baina ya watu , muonekano tupo tofauti baina ya watu na hata nguvu tupo tofauti baina ya watu wapo wenye nguvu sana na wapo wenye nguvu za kawaida .

Hivyo basi kabla ya kutafuta mchawi wa janga hili la nguvu za kiume pengine tuliposahau ni hapa kwamba kama ilivyo ambavyo hatupo sawa kwa mengine kwa sababu tofauti tofauti ambazo zipo nje ya uwezo wetu na kwa nguvu za kiume pia nako tupo tofauti tofauti kwa watu tofauti tofauti.
 
Upvote 4
Back
Top Bottom