PostGE2025 Adui wa Tanganyika sio Samia, sio CCM, ni mfumo tulioulea wenyewe

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Mudawote

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2013
Posts
11,612
Reaction score
16,189
Watanganyika tumejenga tabia ya kutafuta mchawi wa matatizo yetu kila kukicha — tukimlenga kiongozi, chama, au mtu fulani. Wengi leo wanamlaumu Dkt. Samia, wengine CCM, wengine wafanyabiashara, na wengine polisi. Lakini ukweli mchungu ni kwamba adu yetu kama nchi siyo Dkt. Samia, siyo CCM, siyo serikali wala siyo polisi — adui wetu ni MFUMO TULIOULEA NA KUUENDELEZA WENYEWE.

Mfumo huu haukuja kwa pupa; umeota mizizi polepole katika kila familia, kila kijiji, kila ofisi, kila chuo, na kila kanisa au msikiti. Ni mfumo wa udanganyifu, uzembe, tamaa na hila. Mfumo unaomfanya Mtanganyika ajivunie wizi, ajione mjanja akipora, na ajione mshindi anapodanganya.

Mfumo wetu ni ule unaomlea mtoto aamini kwamba mafanikio hayaji kwa kazi, bali kwa ujanja. Tumejenga jamii inayopenda maisha mazuri bila kufanya kazi. Kila mtu anataka gari, nyumba, simu ya kisasa — lakini si kwa jasho lake. Tuna ndoto kubwa, lakini hatutaki jasho jingi.

Mfumo huu umetufanya tujifunze kupenda “kujipanga” badala ya kupanga kazi. Tunapenda “shortcut.” Tunaishi kwa misemo kama “toa hela mambo yanaenda,” “kila kitu ni connection,” “mjanja ni yule anayecheza system.” Haya ni maneno madogo, lakini yameua roho ya Taifa.

Angalia sekta ya elimu: mtu yuko tayari atoe hela aitwe Dokta bila hata kufanya utafiti au kusoma ipasavyo. Hii ndiyo maana marehemu Dkt. Magufuli aliwahi kusema wazi — “tunapenda vyeo kuliko kazi.” Alitufunulia kwamba mfumo huu wa heshima bandia na elimu ya kulipia umetufanya taifa la majina bila matendo.

Mfumo huu umezaa kizazi kinachopenda matokeo, siyo mchakato. Tunataka pesa bila uzalishaji, cheo bila uwezo, heshima bila kujituma, na maendeleo bila nidhamu.

Ndiyo maana hata mauaji, vurugu, na machafuko tunayoona leo Tanzania si matokeo ya mtu mmoja. Ni zao la mfumo mbovu tuliolea kwa miaka mingi. Polisi wanaoua raia siyo kwa sababu wana roho mbaya; bali ni kwa sababu na wao ni wahanga wa mfumo uleule — mishahara midogo, mazingira duni, kukosa matumaini. Wamegeuzwa silaha dhidi ya ndugu zao wanaoteseka kama wao. Mwisho wa siku, Watanganyika tunauana sisi kwa sisi kwa ajili ya mfumo mbovu tulioutengeneza wenyewe.

Tusiendelee kutafuta mchawi kwenye kivuli cha majengo ya serikali, wala kwenye sura za viongozi. Adui yupo ndani ya kila nyumba, kila kaya, kila moyo unaosema “acheni wivu, huyu kachomoka.” Adui yupo kwenye vichekesho vyetu, kwenye nyimbo, kwenye mitandao ya kijamii tunapopongeza ujanja, siyo kazi.

Dkt. Samia siyo adui wetu. CCM siyo adui wetu. Polisi siyo adui wetu. Wafanyabiashara siyo adui wetu. Adui ni mfumo wa kimaadili na kiutamaduni tulioutengeneza wenyewe — mfumo unaokumbatia rushwa, uvivu, unafiki, na tamaa.

Na mpaka tutakapothubutu kuvunja mfumo huu, tutaendelea kulalamika, kuandamana, na kuumia — lakini tutabaki watumwa wa mazao ya roho zetu wenyewe.

Watanganyika, tusipobadilika ndani, hatutabadilika nje. Mfumo wetu ndio unaotuua, siyo viongozi wetu.

Nguvu ya kweli ya mapinduzi ya taifa haipo barabarani, ipo kwenye mioyo ya wale wanaothubutu kubadilisha fikra.

#MfumoDioAdui #TanganyikaMpya #BadilikaWewe
 
Tutaweza kuubadili mfumo bila ya kuweka mechanisms za accountability? Watu wanajua upigaji deal ni njia sahihi kwa sababu hakuna accountability!
 
Mfymo unapunguzwa kwa kuundoa vibaraka wa ccm mpaka sasa wamekua na hofu
 
Jiwe mwenyewe alikuwa na Phd ya mchongo. So siyo mtu wa kumuhusisha na mambo sahihi kwa upande wa elimu. Mengine naona kama uko sahihi sana
 
Wewe jamaa kipindi cha JPM ulitamba hapa jamii forums
Ulitukana mno
Ulitetea utekaji na mauaji ya JPM.
Ulitetea na kuishabikia uchaguzi haramu wa 2019 na 2020
Ulishamgilia mno Lissu alivopigwa risasi
Ulifurahia mno uhuni wa Bashite Sabaya

Nisiwe mnafiki Huwa nakuchukia mno.
Sasa somo umelipata
 
Ewe Gen Z nisamehe 7 mara Sabini. Nilishaandika uzi humu wa kutubu dhambi zangu zote. Tulikosea sana kudhani ilikuwa sahihi watu kuuawa, kutekwa. Tulidanganywa na kitu ita eti kulinda maslahi kumbe wahuni walitumia huo mwanya kuumiza watu wengi. Hata Dkt Magufuli nakuhakikishia hakujua kabisa anahujumiwa. Hivyo wewe mu Gen Z niombee msahama kwa wengine pia.
 
Ben alipotea kwa sababu hiyo
Ben hakika inauma sana kijana mdogo kupotea. Ila suala la PhD siku zote ni ngumu sana kudanganya, niamini ninafahamu mifumo. Waliomuua Ben watakuwa walitaka tu kumpunguzia usumbufu rais labda. Ila PhD ya Dkt Magufuli haiwezi kuwa fake kabisa lasivyo UDSM wangefutiwa usajili kama chuo. Hivyo elewa hata wewe ukienda kusoma UDSM ikitokea umepata nafasi ya kumaliza elewa degree yako haiwezi kuwa fake
 
Ewe Gen Z nisamehe 7 mara Sabini. Nilishaandika uzi humu wa kutubu dhambi zangu zote. Tulikosea sana kudhani ilikuwa sahihi watu kuuawa, kutekwa. Tulidanganywa na kitu ita eti kulinda maslahi kumbe wahuni walitumia huo mwanya kuumiza watu wengi. Hata Dkt Magufuli nakuhakikishia hakujua kabisa anahujumiwa. Hivyo wewe mu Gen Z niombee msahama kwa wengine pia.
Mkuu Mudawote kweli kuna nguvu katk msamaha

Enzi zile mimi nisingeamini kwamba kuna siku ningekusamehe, ila tangu ulipotubu humu wazi wazi mbele ya Mungu na Wanadamu sina neno tena juu yako. Ubarikiwe sana kwa kuamaua kuwa mtu mwema
 
Kwani mfumo si ndio viongozi wenyeww?
Na wana urithi huo mfumo wa kijinga, ndiyo maana hata leo tukikuweka pale Bush Dokta hautawaza ya Gen Z, bali utakuwa mtu wa kulinda mfumo. Si unaona Dkt Samia alivyoingia akawa ana mbagaza Dkt Magufuli, ila cheki mwisho wake kawa mbaya zaidi kupita marais wote
 
Mkuu Mudawote kweli kuna nguvu katk msamaha

Enzi zile mimi nisingeamini kwamba kuna siku ningekusamehe, ila tangu ulipotubu humu wazi wazi mbele ya Mungu na Wanadamu sina neno tena juu yako. Ubarikiwe sana kwa kuamaua kuwa mtu mwema
Bush Dokta nashukuru sana. Hii nchi yetu sote, kila mmoja ana haki ya kutoa mawazo na kusikilizwa na kila mmoja wetu ana haki ya kuishi. Iko siku wale wote waliotekwa watapata haki zao
 
Na wana urithi huo mfumo wa kijinga, ndiyo maana hata leo tukikuweka pale Bush Dokta hautawaza ya Gen Z, bali utakuwa mtu wa kulinda mfumo. Si unaona Dkt Samia alivyoingia akawa ana mbagaza Dkt Magufuli, ila cheki mwisho wake kawa mbaya zaidi kupita marais wote
Inasikitisha sana kwa kweli
 
Ccm na polisi ni tatizo kubwa la Tanganyika, wakifa wote nchi hii tuta kuwa peponi.

Ccm na mapolisi ni majizi, matekaji na mauaji, kwenye hili hawachomoki.

Na ccm na polisi wakifa wachomwe moto.

Hakuna mfumo tulioulea, kama kuna mfumo ni ccm na polisi wao.
 
Watanganyika tumejenga tabia ya kutafuta mchawi wa matatizo yetu kila kukicha — tukimlenga kiongozi, chama, au mtu fulani. Wengi leo wanamlaumu Dkt. Samia, wengine CCM, wengine wafanyabiashara, na wengine polisi. Lakini ukweli mchungu ni kwamba adu yetu kama nchi siyo Dkt. Samia, siyo CCM, siyo serikali wala siyo polisi — adui wetu ni MFUMO TULIOULEA NA KUUENDELEZA WENYEWE.

Mfumo huu haukuja kwa pupa; umeota mizizi polepole katika kila familia, kila kijiji, kila ofisi, kila chuo, na kila kanisa au msikiti. Ni mfumo wa udanganyifu, uzembe, tamaa na hila. Mfumo unaomfanya Mtanganyika ajivunie wizi, ajione mjanja akipora, na ajione mshindi anapodanganya.

Mfumo wetu ni ule unaomlea mtoto aamini kwamba mafanikio hayaji kwa kazi, bali kwa ujanja. Tumejenga jamii inayopenda maisha mazuri bila kufanya kazi. Kila mtu anataka gari, nyumba, simu ya kisasa — lakini si kwa jasho lake. Tuna ndoto kubwa, lakini hatutaki jasho jingi.

Mfumo huu umetufanya tujifunze kupenda “kujipanga” badala ya kupanga kazi. Tunapenda “shortcut.” Tunaishi kwa misemo kama “toa hela mambo yanaenda,” “kila kitu ni connection,” “mjanja ni yule anayecheza system.” Haya ni maneno madogo, lakini yameua roho ya Taifa.

Angalia sekta ya elimu: mtu yuko tayari atoe hela aitwe Dokta bila hata kufanya utafiti au kusoma ipasavyo. Hii ndiyo maana marehemu Dkt. Magufuli aliwahi kusema wazi — “tunapenda vyeo kuliko kazi.” Alitufunulia kwamba mfumo huu wa heshima bandia na elimu ya kulipia umetufanya taifa la majina bila matendo.

Mfumo huu umezaa kizazi kinachopenda matokeo, siyo mchakato. Tunataka pesa bila uzalishaji, cheo bila uwezo, heshima bila kujituma, na maendeleo bila nidhamu.

Ndiyo maana hata mauaji, vurugu, na machafuko tunayoona leo Tanzania si matokeo ya mtu mmoja. Ni zao la mfumo mbovu tuliolea kwa miaka mingi. Polisi wanaoua raia siyo kwa sababu wana roho mbaya; bali ni kwa sababu na wao ni wahanga wa mfumo uleule — mishahara midogo, mazingira duni, kukosa matumaini. Wamegeuzwa silaha dhidi ya ndugu zao wanaoteseka kama wao. Mwisho wa siku, Watanganyika tunauana sisi kwa sisi kwa ajili ya mfumo mbovu tulioutengeneza wenyewe.

Tusiendelee kutafuta mchawi kwenye kivuli cha majengo ya serikali, wala kwenye sura za viongozi. Adui yupo ndani ya kila nyumba, kila kaya, kila moyo unaosema “acheni wivu, huyu kachomoka.” Adui yupo kwenye vichekesho vyetu, kwenye nyimbo, kwenye mitandao ya kijamii tunapopongeza ujanja, siyo kazi.

Dkt. Samia siyo adui wetu. CCM siyo adui wetu. Polisi siyo adui wetu. Wafanyabiashara siyo adui wetu. Adui ni mfumo wa kimaadili na kiutamaduni tulioutengeneza wenyewe — mfumo unaokumbatia rushwa, uvivu, unafiki, na tamaa.

Na mpaka tutakapothubutu kuvunja mfumo huu, tutaendelea kulalamika, kuandamana, na kuumia — lakini tutabaki watumwa wa mazao ya roho zetu wenyewe.

Watanganyika, tusipobadilika ndani, hatutabadilika nje. Mfumo wetu ndio unaotuua, siyo viongozi wetu.

Nguvu ya kweli ya mapinduzi ya taifa haipo barabarani, ipo kwenye mioyo ya wale wanaothubutu kubadilisha fikra.

#MfumoDioAdui #TanganyikaMpya #BadilikaWewe
Kwenye huo mfano wako wa Magufuli,unamzugumzia Magufuli, yule aliyemuua Ben Saanane kwa kutoa andiko linalosema PhD ya Magufuli ni feki?
 
Ben alikuwa mjinga mjinga (Mungu anisamehe sana na wewe unisamehe), UDSM hawawezi to PhD fake. Hicho kitu hakipo kabisa. Ben alikuwa na mihemuko ya kijinga. Waliompoteza naamini nao ni wajinga tu kwa sababu Ben hakuwa na madhara ila alichokuwa anakipigania Ben hakikuwa na Maslahi kitaifa. Cheki wapambanaji wa ukweli ka akinq Lisu wapo pamoja na kupigwa risasi. Ndiyo maana nasema Gen Z wanapaswa kuelewa wawe na madai yenye maslahi na siyo kumuita Samia kilaza etc
 
Back
Top Bottom