Adult Talks 2: Ukigombana na mpenzi/mume/mke wako usiwasimulie ndugu zako mabaya yake. Wewe unaweza kumsamehe ila pengine wao hawataweza

Hii mada ya kufungia mwaka.

Tuanze mwaka ujao na mada ingine.

Kiuhalisia umeongea ukweli mtupu.

Mwanzo wa ndoa nyingi zinaanza kuyumba baada ya upande wa pili kujua ukweli kuhusu wewe.

Hawatakuchukulia kama mwanzo, wakipata nafasi wataanza kukushughulikia.
 
tena ikiwa amekufanyia Yale mambo ambayo hayavumiliki,
Nakubaliana na wewe ila hapo juu ndo umejichanganya.

Sasa mtu kakufanyia mambo ambayo hayavumiliki kuna nini tena kama watu wamekosana na wakarudiana ina maana jambo hilo linavumilika. Kama halivumiliki ina maana ndo imeisha hiyo, kwa hiyo ni bora kuwaeleza watu wako wa karibu ukweli kabla yeye hajawaelezea uongo.

Kwenye mambo ya mahusiano jambo ambalo halivumiliki sio la kulilealea wala kujifariji saa ingine Mungu anakupa alert kwamba hapo umeingia chaka, ukipuuza yatakuja kujiri yatakayojiri.

Usijipe moyo kwa rafiki yako huyo kurudiana na mpenzi wake when sh*t hit the fan you will be suprised na utasema ni kheri angelijua kipindi kile angechukua hatua. Mapenzi kwenye real life sio sawa na kwenye tamthiliya za television.
 
Kuna wengine wanakwambia wenyew kwamba unatakiwa ushee tukio hilo na rafiki zako ili u free stress..sasa kama wenyew ndo wanakushauri unafikir kuwaambia kwamba labda nmeachan a na X c lazma watataka kujua sababu ya kuachana?
 

Mkuu, kwenye mahusiano mambo ambayo hayavumiliki tunayaona sisi tulio nje, ila wahusika huwa hawayaoni. Ndio maana wao wakisameheana, ndugu au jamaa wao Wa karibu wanabaki wanashangaa. Nina mama angu mdogo alikuwa anapigwa na mumewe mpaka sometime anazimia, ndugu zake wanamchukua, wanajaribu kumwambia hakuna mapenzi kazi yake na mumewe atakuja kuuliwa. Ila wakikaa nae hata mwezi, wakichati chati na jamaa utasikia anaomba kurudi kwa mumewe. Kuna kipindi alipigwa hadi akateguka mkono, akaachwa siku mbili ndani bila chakula.

Dada zake walivyojua wakamchukua tena alivyopatiwa matibabu, wakampora na simu ili asiwe na mawasiliano na mumewe. After a while jamaa akawa anakuja home route za usiku,mara avizie dukani as if ndo anatongoza, kumbe yule ni mke wake kabisa wa ndoa. Na chanzo cha ugomvi wao mara zote ni pombe na wanawake. Jamaa alikuwa akilewa anapotea home hata siku mbili, au akiwa home calls za wanawake kama zote,Maza mdogo akiuliza ndo anapewa kipigo.

Siku jamaa anafariki, asilimia kubwa ya ndugu wa mamdogo ile taarifa waliichukulia 50/50 maana ni waliona ni kama ahueni kwao.

Labda nikuulize wewe mkuu, ni vitu gani ambavyo wewe unaona havivumiliki?
 
Kuna wengine wanakwambia wenyew kwamba unatakiwa ushee tukio hilo na rafiki zako ili u free stress..sasa kama wenyew ndo wanakushauri unafikir kuwaambia kwamba labda nmeachan a na X c lazma watataka kujua sababu ya kuachana?
Ni sahihi hutakiwi kubeba mzigo mzito peke yako, ila sio Kila atakayeuliza kulikoni, basi yafaa amwagiwe mkanda wote mwanzo mwisho. Wapo wanaostahili kuambiwa tu kuwa mmegombana bila kudisclose details, na wapo ambao wanaostahili kuambiwa details before hata hawajauliza
 

[emoji2935][emoji2935][emoji2935][emoji2935] Sahihi mkuu. Ndo Ile mwanzoni walikuwa wanakuita shemeji au mkwe, ila after a while unaanza kuitwa kwa jina lako [emoji28]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
100%
 
Uko sahihi Sana Ila inaategemea na aina ya ugomvi,Kama wa ngumi ntasema wa maneno tu ntakaa kimya,wa kutishia kuuana ntashtaki
 
Kuna Mwamba tulikua tunasoma wote Chuo, Nilikua nmemuacha miaka 2 nyuma but tulikua washkaj cz tulikuwa tumepannga nje ya Chuo nyumba za karbu na Tulikuwa team moja ya Volleyball

Unajua mambo ya chuo mshakaj alijiongeza akawa anaishi na msichana, yule dada alikua na wivu na wote tulikua tunajua ila tuliwaacha wenyewe wapambane na hali zao

Siku moja kama kesho tunataka kurud home likzo usiku ananipigia simu niende kwake fasta nkaenda chap kufika nakuta anavuja damu kwenye paja kuuliza nn kumbe shemeji kamchoma na chupa

Huku na huku tukamuwahisha hosptal fasta akatibiwa fresh aliapa.na mizimu ya kwao yote kwamba nikirud semester ijayo napiga chini na sie wengne tunachangia tukijua mwana kaamua kwel

Tumerud semester inayofata tunakuta wanapika na kupakua kama sio yule jamaa alieapiza na mizimu nkasema tu huyu hata nikute anachinjwq hapo ntapita kama sjaona kitu kwa kifup nilibalance shobo mpka shemej alijua kwamba sina habari nao tena.
 
Ameeleza vizuri hapa,labda kama hujasoma vizuri 'Ikitokea unahitaji msaada wa kiushauri, mawazo na counseling, jitahidi kuwa mchaguzi wa watu wa kuwaambia, sio Kila anayekuuliza kulikoni'.....
 
Uko sahihi Sana Ila inaategemea na aina ya ugomvi,Kama wa ngumi ntasema wa maneno tu ntakaa kimya,wa kutishia kuuana ntashtaki
Ugomvi wa kupigana hata usiposema watu watajua tu, maana wataona hali Yako. Ila kuna Yale manyanyaso, dharau etc ambayo yanaumiza sana ndani kwa ndani, ila watu wa nje sio rahisi kuyajua
 
Ameeleza vizuri hapa,labda kama hujasoma vizuri 'Ikitokea unahitaji msaada wa kiushauri, mawazo na counseling, jitahidi kuwa mchaguzi wa watu wa kuwaambia, sio Kila anayekuuliza kulikoni'.....
Asante [emoji120]
 
Mapenzi ni kitu cha tofauti sana
 

Here We Go!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…