Adult Talks 2: Ukigombana na mpenzi/mume/mke wako usiwasimulie ndugu zako mabaya yake. Wewe unaweza kumsamehe ila pengine wao hawataweza

Adult Talks 2: Ukigombana na mpenzi/mume/mke wako usiwasimulie ndugu zako mabaya yake. Wewe unaweza kumsamehe ila pengine wao hawataweza

Hii mada ya kufungia mwaka.

Tuanze mwaka ujao na mada ingine.

Kiuhalisia umeongea ukweli mtupu.

Mwanzo wa ndoa nyingi zinaanza kuyumba baada ya upande wa pili kujua ukweli kuhusu wewe.

Hawatakuchukulia kama mwanzo, wakipata nafasi wataanza kukushughulikia.
 
tena ikiwa amekufanyia Yale mambo ambayo hayavumiliki,
Nakubaliana na wewe ila hapo juu ndo umejichanganya.

Sasa mtu kakufanyia mambo ambayo hayavumiliki kuna nini tena kama watu wamekosana na wakarudiana ina maana jambo hilo linavumilika. Kama halivumiliki ina maana ndo imeisha hiyo, kwa hiyo ni bora kuwaeleza watu wako wa karibu ukweli kabla yeye hajawaelezea uongo.

Kwenye mambo ya mahusiano jambo ambalo halivumiliki sio la kulilealea wala kujifariji saa ingine Mungu anakupa alert kwamba hapo umeingia chaka, ukipuuza yatakuja kujiri yatakayojiri.

Usijipe moyo kwa rafiki yako huyo kurudiana na mpenzi wake when sh*t hit the fan you will be suprised na utasema ni kheri angelijua kipindi kile angechukua hatua. Mapenzi kwenye real life sio sawa na kwenye tamthiliya za television.
 
Kuna wengine wanakwambia wenyew kwamba unatakiwa ushee tukio hilo na rafiki zako ili u free stress..sasa kama wenyew ndo wanakushauri unafikir kuwaambia kwamba labda nmeachan a na X c lazma watataka kujua sababu ya kuachana?
 
Nakubaliana na wewe ila hapo juu ndo umejichanganya.

Sasa mtu kakufanyia mambo ambayo hayavumiliki kuna nini tena kama watu wamekosana na wakarudiana ina maana jambo hilo linavumilika.
Kama halivumiliki ina maana ndo imeisha hiyo, kwa hiyo ni bora kuwaeleza watu wako wa karibu ukweli kabla yeye hajawaelezea uongo.

Kwenye mambo ya mahusiano jambo ambalo halivumiliki sio la kulilealea wala kujifariji saa ingine Mungu anakupa alert kwamba hapo umeingia chaka, ukipuuza yatakuja kujiri yatakayojiri.

Usijipe moyo kwa rafiki yako huyo kurudiana na mpenzi wake when sh*t hit the fan you will be suprised na utasema ni kheri angelijua kipindi kile angechukua hatua. Mapenzi kwenye real life sio sawa na kwenye tamthiliya za television.

Mkuu, kwenye mahusiano mambo ambayo hayavumiliki tunayaona sisi tulio nje, ila wahusika huwa hawayaoni. Ndio maana wao wakisameheana, ndugu au jamaa wao Wa karibu wanabaki wanashangaa. Nina mama angu mdogo alikuwa anapigwa na mumewe mpaka sometime anazimia, ndugu zake wanamchukua, wanajaribu kumwambia hakuna mapenzi kazi yake na mumewe atakuja kuuliwa. Ila wakikaa nae hata mwezi, wakichati chati na jamaa utasikia anaomba kurudi kwa mumewe. Kuna kipindi alipigwa hadi akateguka mkono, akaachwa siku mbili ndani bila chakula.

Dada zake walivyojua wakamchukua tena alivyopatiwa matibabu, wakampora na simu ili asiwe na mawasiliano na mumewe. After a while jamaa akawa anakuja home route za usiku,mara avizie dukani as if ndo anatongoza, kumbe yule ni mke wake kabisa wa ndoa. Na chanzo cha ugomvi wao mara zote ni pombe na wanawake. Jamaa alikuwa akilewa anapotea home hata siku mbili, au akiwa home calls za wanawake kama zote,Maza mdogo akiuliza ndo anapewa kipigo.

Siku jamaa anafariki, asilimia kubwa ya ndugu wa mamdogo ile taarifa waliichukulia 50/50 maana ni waliona ni kama ahueni kwao.

Labda nikuulize wewe mkuu, ni vitu gani ambavyo wewe unaona havivumiliki?
 
Kuna wengine wanakwambia wenyew kwamba unatakiwa ushee tukio hilo na rafiki zako ili u free stress..sasa kama wenyew ndo wanakushauri unafikir kuwaambia kwamba labda nmeachan a na X c lazma watataka kujua sababu ya kuachana?
Ni sahihi hutakiwi kubeba mzigo mzito peke yako, ila sio Kila atakayeuliza kulikoni, basi yafaa amwagiwe mkanda wote mwanzo mwisho. Wapo wanaostahili kuambiwa tu kuwa mmegombana bila kudisclose details, na wapo ambao wanaostahili kuambiwa details before hata hawajauliza
 
Hii mada ya kufungia mwaka.

Tuanze mwaka ujao na mada ingine.

Kiuhalisia umeongea ukweli mtupu.

Mwanzo wa ndoa nyingi zinaanza kuyumba baada ya upande wa pili kujua ukweli kuhusu wewe.

Hawatakuchukulia kama mwanzo, wakipata nafasi wataanza kukushughulikia.

[emoji2935][emoji2935][emoji2935][emoji2935] Sahihi mkuu. Ndo Ile mwanzoni walikuwa wanakuita shemeji au mkwe, ila after a while unaanza kuitwa kwa jina lako [emoji28]
 
Hii mada ya kufungia mwaka.

Tuanze mwaka ujao na mada ingine.

Kiuhalisia umeongea ukweli mtupu.

Mwanzo wa ndoa nyingi zinaanza kuyumba baada ya upande wa pili kujua ukweli kuhusu wewe.

Hawatakuchukulia kama mwanzo, wakipata nafasi wataanza kukushughulikia.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Unajua mahusiano yanachangamoto nyingi sana, na hazifanani. Kila mmoja kwa sehemu yake anapitia changamoto katika mahusiano. Sasa inapotokea umefanyiwa mabaya na mtu uliyenae kwenye mahusiano, sio jambo zuri kuyaweka wazi mabaya yake hasa kwa ndugu zako au watu wako wa karibu sana.

Unajua mapenzi yana nguvu sana, kuna baadhi ya scenarios zinatokea kwa watu hadi unajisemea kwamba "its over between these two" lakini unakuja kuwa surprised after awhile unakuta wako pamoja as if nothing happened. Nina jamaa yangu ashawahi mkuta mpenz wake amebananishwa uchochoroni na jamaa, ilikuwa usiku tunatoka kuangalia mpira, na kama tungechelewa kidogo tungekuta wanafanya mapenzi. Jamaa alikuwa disappointed sana kiasi kwamba nikajua ndo mwisho wa penzi lao, ila after siku kadhaa naona wako pamoja as if nothing happened. Sikumshangaa jamaa,japo yule Shem wangu Wala simchangamkii kama ilivyokuwa zamani.

Point ya kuandika huu uzi ni kwamba, ikitokea umegombana na mtu ambae uko nae katika serious relationship, tena ikiwa amekufanyia Yale mambo ambayo hayavumiliki, nakusihi hutakiwi kuyaanika mabaya yake Kila sehemu, maana kesho ni fumbo.

Ikitokea unahitaji msaada wa kiushauri, mawazo na counseling, jitahidi kuwa mchaguzi wa watu wa kuwaambia, sio Kila anayekuuliza kulikoni? Basi wewe unammwagia file Zima la mtu wako alichofanya. Kuna watu wanabeba matatizo yetu kwa uzito sana. Kuna wale watu ambao kipindi upo kwenye mapito ndio waliokuwa faraja Yako, ndio waliokuwa wanahakikisha hujidhuru, wanahakikisha furaha yako inarudi, so ikitokea wewe umemsamehe, wao wanaweza wasimsamehe. Na kutomsamehe kwao kunatokana na kumbukumbu zao jinsi ulivyokuwa unapitia hali ngumu sababu ya huyo mtu wako. Au jinsi wao walivyokuwa hawafanyi mambo yao kwa uhuru ilimradi kuhakikisha wanakufariji wewe.

Wewe utampa second chance,ila wao hawatakaa wampe hiyo nafasi. Na inawezekana wasimpe tena ule uzito waliokuwa wanampa awali.

That's All (Ni hayo Tu).

Analyse
100%
 
Uko sahihi Sana Ila inaategemea na aina ya ugomvi,Kama wa ngumi ntasema wa maneno tu ntakaa kimya,wa kutishia kuuana ntashtaki
 
Kuna Mwamba tulikua tunasoma wote Chuo, Nilikua nmemuacha miaka 2 nyuma but tulikua washkaj cz tulikuwa tumepannga nje ya Chuo nyumba za karbu na Tulikuwa team moja ya Volleyball

Unajua mambo ya chuo mshakaj alijiongeza akawa anaishi na msichana, yule dada alikua na wivu na wote tulikua tunajua ila tuliwaacha wenyewe wapambane na hali zao

Siku moja kama kesho tunataka kurud home likzo usiku ananipigia simu niende kwake fasta nkaenda chap kufika nakuta anavuja damu kwenye paja kuuliza nn kumbe shemeji kamchoma na chupa

Huku na huku tukamuwahisha hosptal fasta akatibiwa fresh aliapa.na mizimu ya kwao yote kwamba nikirud semester ijayo napiga chini na sie wengne tunachangia tukijua mwana kaamua kwel

Tumerud semester inayofata tunakuta wanapika na kupakua kama sio yule jamaa alieapiza na mizimu nkasema tu huyu hata nikute anachinjwq hapo ntapita kama sjaona kitu kwa kifup nilibalance shobo mpka shemej alijua kwamba sina habari nao tena.
 
Faida za kuwa elezea ni nyingi kuliko hasara.

Iwapo wataona haina haja ya kusamehe kutokana na madhara au damages wanazoziona zinazoweza mfika siku zijazo wakati wowote ndugu yao ni bora kutorejea.

Mauaji mengi ya wanandoa hususa wake mara nyingi ziliamza dalili na ishara za wazi lakini zikapuuzwa bila kuamua kukaa mbali mwanamke au bila kushirikisha
Wazazi na ndugu wa damu ili kushauriwa kuondoka kabla ya kumfika mazito.

Akumulikae mchana usiku atakuchoma.
Ameeleza vizuri hapa,labda kama hujasoma vizuri 'Ikitokea unahitaji msaada wa kiushauri, mawazo na counseling, jitahidi kuwa mchaguzi wa watu wa kuwaambia, sio Kila anayekuuliza kulikoni'.....
 
Uko sahihi Sana Ila inaategemea na aina ya ugomvi,Kama wa ngumi ntasema wa maneno tu ntakaa kimya,wa kutishia kuuana ntashtaki
Ugomvi wa kupigana hata usiposema watu watajua tu, maana wataona hali Yako. Ila kuna Yale manyanyaso, dharau etc ambayo yanaumiza sana ndani kwa ndani, ila watu wa nje sio rahisi kuyajua
 
Ameeleza vizuri hapa,labda kama hujasoma vizuri 'Ikitokea unahitaji msaada wa kiushauri, mawazo na counseling, jitahidi kuwa mchaguzi wa watu wa kuwaambia, sio Kila anayekuuliza kulikoni'.....
Asante [emoji120]
 
Kuna Mwamba tulikua tunasoma wote Chuo, Nilikua nmemuacha miaka 2 nyuma but tulikua washkaj cz tulikuwa tumepannga nje ya Chuo nyumba za karbu na Tulikuwa team moja ya Volleyball

Unajua mambo ya chuo mshakaj alijiongeza akawa anaishi na msichana, yule dada alikua na wivu na wote tulikua tunajua ila tuliwaacha wenyewe wapambane na hali zao

Siku moja kama kesho tunataka kurud home likzo usiku ananipigia simu niende kwake fasta nkaenda chap kufika nakuta anavuja damu kwenye paja kuuliza nn kumbe shemeji kamchoma na chupa

Huku na huku tukamuwahisha hosptal fasta akatibiwa fresh aliapa.na mizimu ya kwao yote kwamba nikirud semester ijayo napiga chini na sie wengne tunachangia tukijua mwana kaamua kwel

Tumerud semester inayofata tunakuta wanapika na kupakua kama sio yule jamaa alieapiza na mizimu nkasema tu huyu hata nikute anachinjwq hapo ntapita kama sjaona kitu kwa kifup nilibalance shobo mpka shemej alijua kwamba sina habari nao tena.
Mapenzi ni kitu cha tofauti sana
 
Unajua mahusiano yanachangamoto nyingi sana, na hazifanani. Kila mmoja kwa sehemu yake anapitia changamoto katika mahusiano. Sasa inapotokea umefanyiwa mabaya na mtu uliyenae kwenye mahusiano, sio jambo zuri kuyaweka wazi mabaya yake hasa kwa ndugu zako au watu wako wa karibu sana.

Unajua mapenzi yana nguvu sana, kuna baadhi ya scenarios zinatokea kwa watu hadi unajisemea kwamba "its over between these two" lakini unakuja kuwa surprised after awhile unakuta wako pamoja as if nothing happened.

Nina jamaa yangu ashawahi mkuta mpenz wake amebananishwa uchochoroni na jamaa, ilikuwa usiku tunatoka kuangalia mpira, na kama tungechelewa kidogo tungekuta wanafanya mapenzi. Jamaa alikuwa disappointed sana kiasi kwamba nikajua ndo mwisho wa penzi lao, ila after siku kadhaa naona wako pamoja as if nothing happened. Sikumshangaa jamaa,japo yule Shem wangu Wala simchangamkii kama ilivyokuwa zamani.

Point ya kuandika huu uzi ni kwamba, ikitokea umegombana na mtu ambae uko nae katika serious relationship, tena ikiwa amekufanyia Yale mambo ambayo hayavumiliki, nakusihi hutakiwi kuyaanika mabaya yake Kila sehemu, maana kesho ni fumbo.

Ikitokea unahitaji msaada wa kiushauri, mawazo na counseling, jitahidi kuwa mchaguzi wa watu wa kuwaambia, sio Kila anayekuuliza kulikoni? Basi wewe unammwagia file Zima la mtu wako alichofanya. Kuna watu wanabeba matatizo yetu kwa uzito sana.

Kuna wale watu ambao kipindi upo kwenye mapito ndio waliokuwa faraja Yako, ndio waliokuwa wanahakikisha hujidhuru, wanahakikisha furaha yako inarudi, so ikitokea wewe umemsamehe, wao wanaweza wasimsamehe. Na kutomsamehe kwao kunatokana na kumbukumbu zao jinsi ulivyokuwa unapitia hali ngumu sababu ya huyo mtu wako. Au jinsi wao walivyokuwa hawafanyi mambo yao kwa uhuru ilimradi kuhakikisha wanakufariji wewe.

Wewe utampa second chance,ila wao hawatakaa wampe hiyo nafasi. Na inawezekana wasimpe tena ule uzito waliokuwa wanampa awali.

That's All (Ni hayo Tu).

Analyse

Here We Go!
 
Back
Top Bottom