Adult Talks 2: Ukigombana na mpenzi/mume/mke wako usiwasimulie ndugu zako mabaya yake. Wewe unaweza kumsamehe ila pengine wao hawataweza

Mkuu, kuna jamaa hapa pemben amesema nikuulze kitu
 
Mkuu, kwenye mahusiano mambo ambayo hayavumiliki tunayaona sisi tulio nje, ila wahusika huwa hawayaoni. Ndio maana wao wakisameheana, ndugu au jamaa wao Wa karibu wanabaki wanashangaa. Nina mama angu mdogo alikuwa
Basi hapo mkuu shida ni kwa mwanake ndiye hawezi kumuacha mumewe either anahisi hatopata mwingine au hatopata utamu anopewa kwingine hapo ujue jamaa alikuwa anamuwezea ila yeye alikuwa haridhiki naye ndio maana haachi kutafuta wengine.

Kwa hiyo huyo mwanamke alikuwa anadeal na vitu visivyovumilika ila alikuwa navilealea au anajifariji ipo siku vitabadilika lakini yasingetokea mapenzi ya Mungu mwisho wake angeletewa magonjwa au angetiwa kilema cha maisha kama sio kupoteza pumzi.
 
Ikitokea unahitaji msaada wa kiushauri, mawazo na counseling, jitahidi kuwa mchaguzi wa watu wa kuwaambia, sio Kila anayekuuliza kulikoni? Basi wewe unammwagia file Zima la mtu wako alichofanya. Kuna watu wanabeba matatizo yetu kwa uzito sana.
Nadhani Watu hawa ndio umewazungumzia.....

Wasomaji mnapochagua wa kuwaeleza matatizo ya wenza wenu,, hawa aliowasema mleta uzi muwe mnawazingatia....
 
Mimi hili jambo niliwahi kulishuhudia Kwa jirani yangu tena nikiwa ndo mtetezi namba Moja

Ilikua jamaa alikua na kawaida anaporudi kwake akiwa tungi yeye kazi yake ilikua ni kutukana matusi Kwa mkewe yan alafu Kwa sauti kubwa majirani wote tunaskia, binafsi nilikua sipendi hii tabia na alipokua anatukana mkewe nae anamjibu Kwa matusi yaan vita vita. Sasa ikionekana matusi wamechoka wanaanza kupigana, mwanamke anadundwa weee mwishowe anaanza Kulia majirani tumsaidie kumtetea

Na ukiangalia jamaa afanyi matunzo mazuri Kwa mkewe na mtoto wake
Kwa mujibu wa maelezo ya mkewe anasema anapotoka aachi chochote alafu akirudi anataka ale apo ndo ugomvi na matusi yanaanza

Majirani tukamshauri yule binti ikiwezekana we achana nae tafuta vijikazi vya kuingiza chochote kitu ikusaidie hata kula ya wewe na mtoto. Siku nakumbuka tumetoka kumwambia jion yake tukaskia kipigo aisee siku hiyo alidundwa sana mpaka nkajawa na Imani ikabidi niende kumsaidia asipigwe, mpalangano ulikua sio wa kitoto niling'atwa na meno mkononi Hadi akaniachia jeraha kubwa jamaa yule ndo kubahatika kumfunga kamba Kwa nyuma asiyumbe yumbe ndo majiran wengine kuanza kumsihi aachane na upumbavu ye Kila siku pombe nyumban aachi chochote bado na mke anampiga bila sababu. Ndo jamaa yule kuelewa na tangu siku hiyo na pombe akapunguza ndo kumuokoa dada yule

Kwa hiyo wakati mwingine watu wa karibu ni muhimu kujua inakua inakupa ahueni kama Kuna jambo lolote Baya linaweza kutokea

Japo hili swala binafsi siwezi kurudia kutetea huu upuuzi mana unaweza ukasababishiwa ukilema huku wao wanaendelea kufurahia maisha Yao Kila mtu apambane na mambo yake
 
True
 
Binafsi siwezi kumlaumu maana mapenzi yanakuwaga na surprise sana. Unaweza ukamchukia mtu, ila aliyesababisha umchukie, yeye upendo wake ukawa umerudi
 
Mkuu kabla ya kuingilia ugomvi wa mapenzi, chukua kwanza taadhari. Unaweza kwenda kugombelezea ukaishia kupigwa wewe [emoji28]
 
Nadhani Watu hawa ndio umewazungumzia.....

Wasomaji mnapochagua wa kuwaeleza matatizo ya wenza wenu,, hawa aliowasema mleta uzi muwe mnawazingatia....
Yeah sure mkuu.
 
Uko sahihi kabisa.Nina mfano hai.

Mke wa bro alilala nje, alivyorudi bro alishindwa kustahimili alitaka kumpiga risasi na yeye ajiue.Ndugu walisuluhisha hadi hali ikawa shwari. Ni mwaka Sasa tangu tukio lilipotokea.Bro na mkewe mahusiano yako yamerudi Kama zamani ila mkewe kila mtu hapa nyumbani anamuona Kama adui.
 
Watu wetu wa karibu wanaumia zaidi kuliko hata sisi, kwa mambo yanayotukuta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…