Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Basi hapo mkuu shida ni kwa mwanake ndiye hawezi kumuacha mumewe either anahisi hatopata mwingine au hatopata utamu anopewa kwingine hapo ujue jamaa alikuwa anamuwezea ila yeye alikuwa haridhiki naye ndio maana haachi kutafuta wengine.Mkuu, kwenye mahusiano mambo ambayo hayavumiliki tunayaona sisi tulio nje, ila wahusika huwa hawayaoni. Ndio maana wao wakisameheana, ndugu au jamaa wao Wa karibu wanabaki wanashangaa. Nina mama angu mdogo alikuwa
Nadhani Watu hawa ndio umewazungumzia.....Ikitokea unahitaji msaada wa kiushauri, mawazo na counseling, jitahidi kuwa mchaguzi wa watu wa kuwaambia, sio Kila anayekuuliza kulikoni? Basi wewe unammwagia file Zima la mtu wako alichofanya. Kuna watu wanabeba matatizo yetu kwa uzito sana.
TrueUnajua mahusiano yanachangamoto nyingi sana, na hazifanani. Kila mmoja kwa sehemu yake anapitia changamoto katika mahusiano. Sasa inapotokea umefanyiwa mabaya na mtu uliyenae kwenye mahusiano, sio jambo zuri kuyaweka wazi mabaya yake hasa kwa ndugu zako au watu wako wa karibu sana.
Unajua mapenzi yana nguvu sana, kuna baadhi ya scenarios zinatokea kwa watu hadi unajisemea kwamba "its over between these two" lakini unakuja kuwa surprised after awhile unakuta wako pamoja as if nothing happened.
Nina jamaa yangu ashawahi mkuta mpenz wake amebananishwa uchochoroni na jamaa, ilikuwa usiku tunatoka kuangalia mpira, na kama tungechelewa kidogo tungekuta wanafanya mapenzi. Jamaa alikuwa disappointed sana kiasi kwamba nikajua ndo mwisho wa penzi lao, ila after siku kadhaa naona wako pamoja as if nothing happened. Sikumshangaa jamaa,japo yule Shem wangu Wala simchangamkii kama ilivyokuwa zamani.
Point ya kuandika huu uzi ni kwamba, ikitokea umegombana na mtu ambae uko nae katika serious relationship, tena ikiwa amekufanyia Yale mambo ambayo hayavumiliki, nakusihi hutakiwi kuyaanika mabaya yake Kila sehemu, maana kesho ni fumbo.
Ikitokea unahitaji msaada wa kiushauri, mawazo na counseling, jitahidi kuwa mchaguzi wa watu wa kuwaambia, sio Kila anayekuuliza kulikoni? Basi wewe unammwagia file Zima la mtu wako alichofanya. Kuna watu wanabeba matatizo yetu kwa uzito sana.
Kuna wale watu ambao kipindi upo kwenye mapito ndio waliokuwa faraja Yako, ndio waliokuwa wanahakikisha hujidhuru, wanahakikisha furaha yako inarudi, so ikitokea wewe umemsamehe, wao wanaweza wasimsamehe. Na kutomsamehe kwao kunatokana na kumbukumbu zao jinsi ulivyokuwa unapitia hali ngumu sababu ya huyo mtu wako. Au jinsi wao walivyokuwa hawafanyi mambo yao kwa uhuru ilimradi kuhakikisha wanakufariji wewe.
Wewe utampa second chance,ila wao hawatakaa wampe hiyo nafasi. Na inawezekana wasimpe tena ule uzito waliokuwa wanampa awali.
That's All (Ni hayo Tu).
Analyse
Binafsi siwezi kumlaumu maana mapenzi yanakuwaga na surprise sana. Unaweza ukamchukia mtu, ila aliyesababisha umchukie, yeye upendo wake ukawa umerudiBasi hapo mkuu shida ni kwa mwanake ndiye hawezi kumuacha mumewe either anahisi hatopata mwingine au hatopata utamu anopewa kwingine hapo ujue jamaa alikuwa anamuwezea ila yeye alikuwa haridhiki naye ndio maana haachi kutafuta wengine.
Kwa hiyo huyo mwanamke alikuwa anadeal na vitu visivyovumilika ila alikuwa navilealea au anajifariji ipo siku vitabadilika lakini yasingetokea mapenzi ya Mungu mwisho wake angeletewa magonjwa au angetiwa kilema cha maisha kama sio kupoteza pumzi.
Mkuu kabla ya kuingilia ugomvi wa mapenzi, chukua kwanza taadhari. Unaweza kwenda kugombelezea ukaishia kupigwa wewe [emoji28]Mimi hili jambo niliwahi kulishuhudia Kwa jirani yangu tena nikiwa ndo mtetezi namba Moja
Ilikua jamaa alikua na kawaida anaporudi kwake akiwa tungi yeye kazi yake ilikua ni kutukana matusi Kwa mkewe yan alafu Kwa sauti kubwa majirani wote tunaskia, binafsi nilikua sipendi hii tabia na alipokua anatukana mkewe nae anamjibu Kwa matusi yaan vita vita
Sasa ikionekana matusi wamechoka wanaanza kupigana, mwanamke anadundwa weee mwishowe anaanza Kulia majirani tumsaidie kumtetea
Na ukiangalia jamaa afanyi matunzo mazuri Kwa mkewe na mtoto wake
Kwa mujibu wa maelezo ya mkewe anasema anapotoka aachi chochote alafu akirudi anataka ale apo ndo ugomvi na matusi yanaanza
Majirani tukamshauri yule binti ikiwezekana we achana nae tafuta vijikazi vya kuingiza chochote kitu ikusaidie hata kula ya wewe na mtoto
Siku nakumbuka tumetoka kumwambia jion yake tukaskia kipigo aisee siku hiyo alidundwa sana mpaka nkajawa na Imani ikabidi niende kumsaidia asipigwe, mpalangano ulikua sio wa kitoto niling'atwa na meno mkononi Hadi akaniachia jeraha kubwa jamaa yule ndo kubahatika kumfunga kamba Kwa nyuma asiyumbe yumbe ndo majiran wengine kuanza kumsihi aachane na upumbavu ye Kila siku pombe nyumban aachi chochote bado na mke anampiga bila sababu
Ndo jamaa yule kuelewa na tangu siku hiyo na pombe akapunguza ndo kumuokoa dada yule
Kwa hiyo wakati mwingine watu wa karibu ni muhimu kujua inakua inakupa ahueni kama Kuna jambo lolote Baya linaweza kutokea
Japo hili swala binafsi siwezi kurudia kutetea huu upuuzi mana unaweza ukasababishiwa ukilema huku wao wanaendelea kufurahia maisha Yao Kila mtu apambane na mambo yake
Hiyo ni fact sipingiBinafsi siwezi kumlaumu maana mapenzi yanakuwaga na surprise sana. Unaweza ukamchukia mtu, ila aliyesababisha umchukie, yeye upendo wake ukawa umerudi
Nimekuelewa.....Ameeleza vizuri hapa,labda kama hujasoma vizuri 'Ikitokea unahitaji msaada wa kiushauri, mawazo na counseling, jitahidi kuwa mchaguzi wa watu wa kuwaambia, sio Kila anayekuuliza kulikoni'.....
Watu wetu wa karibu wanaumia zaidi kuliko hata sisi, kwa mambo yanayotukutaUko sahihi kabisa.Nina mfano hai.
Mke wa bro alilala nje, alivyorudi bro alishindwa kustahimili alitaka kumpiga risasi na yeye ajiue.Ndugu walisuluhisha hadi hali ikawa shwari. Ni mwaka Sasa tangu tukio lilipotokea.Bro na mkewe mahusiano yako yamerudi Kama zamani ila mkewe kila mtu hapa nyumbani anamuona Kama adui.
Kweli tupu , ngoja niishie hapaMambo ya chumbani kwa wanandoa yanabakia chumbani...
Ukishirikisha tu ndugu, yani mtu wa tatu...
Umekaribisha ugomvi usioisha...