Advocate Mtatiro: Polisi wamemtesa sana na kumuumiza Daktari aliyepigana na Traffic

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram ameandika:

"Kuna msamaria mwema ndani ya Jeshi la Polisi kanijulisha kwamba Doctor Conrad Agonza ambae alipigana na Traffic yupo kituo cha Polisi Oysterbay.

Anasema juzi baada ya Wanajeshi wa JWTZ kuachanisha ugomvi huo, walimchukua Dr. Conrad Agonza kisha wakamkabidhi mikono mwa Jeshi la Polisi, akiwa ni mzima kabisa na hakuna mwananchi wala JW ambae alimgusa.

Baada ya Wajeda kuondoka, Polisi walimtoa Dr. Conrad Agonza kwenye kituo cha Polisi akiwa amemfungwa kitambaa cheusi usoni kisha wakampeleka kwenye karakana yao ya kutesea watu, wakaanza kumpiga na kumpa mateso ya kila aina.🥹

Mtoa taarifa anasema kwamba tangu juzi Dr Conrad Agonza, amekuwa akipigwa na kupewa mateso ya kila aina mpaka mwili wake umevilia damu na hawezi kutembea vizuri anachechemea kwasababu walimtegua miguu yote miwili.

Hata zile nguo alizokuwa amevaa kwenye zile picha walimchania, akabaki na kivest cheupe na kibukta cha kaki ambacho kiliokotwa kwenye hiyo karakana then akapewa yeye avae.

Wakati Afande Muliro anatoa taarifa kwa Umma kwamba Dr. Conrad yupo Hospital anatibiwa kwasababu kapigwa na Wananchi alidanganya maana huo muda Dr. Conrad alikuwa huko kwenye karakana ya Polisi akiendelea kupewa mateso na kupigwa, hajawai kupelekwa Hospital wala Zahanati.

Polisi baada ya kuona kelele zimekua nyingi kwenye mitandao ya kijamii na huko kwenye korido za Madaktari, jana mida jioni hivi ndo walimtoa huko kwenye karakana yao na kumpeleka kituo cha Polisi Oysterbay."

Soma pia
 
Ni udhaifu tu wa hao Polisi, mbona hata Madaktari au Manesi hata Makarani wakimfunga mtu kwa kamba wanaweza wakampiga na kumtesa watakavyo.

Wanafanya yote hayo kwa kuwa wamejipa kinga, bila kinga. Bila ya hizo kinga walizojipa tungeona ukakamavu wao pale walipopigana wawili.

kutumia risasi za moto na mabomu ya machozi dhidi ya raia walio mikono mitupu huo na ndiyo ukakamavu?? Ukakamavu ni kuwatuliza kwa mikono au angalau kwa gari la maji.
 
Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram ameandika:

"Kuna msamaria mwema ndani ya Jeshi la Polisi kanijulisha kwamba Doctor Conrad Agonza ambae alipigana na Traffic yupo kituo cha Polisi Oysterbay.

Anasema juzi baada ya Wanajeshi wa JWTZ kuachanisha ugomvi huo, walimchukua Dr. Conrad Agonza kisha wakamkabidhi mikono mwa Jeshi la Polisi, akiwa ni mzima kabisa na hakuna mwananchi wala JW ambae alimgusa.

Baada ya Wajeda kuondoka, Polisi walimtoa Dr. Conrad Agonza kwenye kituo cha Polisi akiwa amemfungwa kitambaa cheusi usoni kisha wakampeleka kwenye karakana yao ya kutesea watu, wakaanza kumpiga na kumpa mateso ya kila aina.🥹

Mtoa taarifa anasema kwamba tangu juzi Dr Conrad Agonza, amekuwa akipigwa na kupewa mateso ya kila aina mpaka mwili wake umevilia damu na hawezi kutembea vizuri anachechemea kwasababu walimtegua miguu yote miwili.

Hata zile nguo alizokuwa amevaa kwenye zile picha walimchania, akabaki na kivest cheupe na kibukta cha kaki ambacho kiliokotwa kwenye hiyo karakana then akapewa yeye avae.

Wakati Afande Muliro anatoa taarifa kwa Umma kwamba Dr. Conrad yupo Hospital anatibiwa kwasababu kapigwa na Wananchi alidanganya maana huo muda Dr. Conrad alikuwa huko kwenye karakana ya Polisi akiendelea kupewa mateso na kupigwa, hajawai kupelekwa Hospital wala Zahanati.

Polisi baada ya kuona kelele zimekua nyingi kwenye mitandao ya kijamii na huko kwenye korido za Madaktari, jana mida jioni hivi ndo walimtoa huko kwenye karakana yao na kumpeleka kituo cha Polisi Oysterbay."

Soma pia
Mwoneni huyu mbwa amejitungia uzusgi wake bila ht haya
 
Back
Top Bottom